Uimara wa nyumba yoyote ni msingi,nyumba ikiwa na msingi wa hovyo hata kimbunga kitaiangusha,malezi ndo msingi wa mwanadamu yoyote!Maisha unayoishi,namna unavyoiona dunia na mitazamo yako yote ni kutokana na malezi,kama unataka wanao wawe bora zingatia haya!

Hakika,nakubaliana na wewe 100%,Malezi Bora humweka mbali mtoto na Uovu na ndiyo mzizi wa kila kitu chema katika Maisha ya mtoto yote!!
Imeandikwa "Mfunze Mtoto NJIA IMPASAYO NAYE HATOIACHA HATA UZEE WAKE"......"TRAIN UP A CHILD IN THE WAY HE SHOULD GO AND HE WILL NOT DEPART FROM IT",Hii ndiyo Hekima ya Mungu ambaye ndiye Muasisi wa Familia na maisha kwa Ujumla!!
Tatizo wazazi tuliowengi hasa sisi wakina Baba hatu TRAIN watoto,mtoto anakuwa kama Mgomba tu,Hatupandi mbegu bora katka Mashamba yetu,as a result magugu yanaota!! Hii inasababishwa na Uvivu na Kukosa Maarifa!!
Hatuwafundishi kwa Bidii hata vitu vidogo tu kama Kushukuru,kusamehe,Kutoa,Kuomba Msamaha,Kuheshimu wengine hasa watu wazima,etc,wengi hatiufanyi,wengine wanaenda mbali zaidi,mtoto akikosa wala mzazi hamrudi wala kukalipia Uovu!!
Kama Masomo hayo mepesi tu tunashinda kuyashinikiza kuingiza katika vichwa na Mioyo ya watoto sembuse kuwafundisha KUJIHESHIMU,KUWA NA FAHARI,UVUMILIVU,KIASI(SELF-CONTROL)etc!!
Mtu ambaye wazazi wake wamemfundisha na kusimamia MAADILI kwa BIDII hawezi kufanya Uasi au kutumia Uchi wake kama nyenzo ya kujipatia kipato,hata uza hata karanga ili haweze kujikimu,hata fanya Ngono na Mtu akisukumwa na Upendo sio Tumbo!!
Chanzo cha Matatizo yote haya ni Wazazi wengi hasa wanaume hatutimizi Majukumu yetu,tupo bize na Mpira,Pombe na Umalaya!!
Lets Change and Make the World a better place to Live!!