Bikis
Member
- Feb 23, 2019
- 52
- 74
Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi, imesema itajibu vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya, bila ya kuanisha moja kwa moja hatua inayolenga kuchukua. Umoja wa Ulaya ulitangaza siku ya Ijumaa kuongeza idadi ya raia nane wa Urusi, wakiwemo maafisa wa ngazi ya juu wa usalama na jeshi, kwenye orodha yake ya vikwazo kutokana na mzozo kati ya Urusi na Ukraine kwenye bahari ya Azov. Umoja wa Ulaya unawatuhumu maafisa hao kuzuia meli za Ukraine kuzifikia bandari za bahari ya Azov. Katika taarifa yake iliyochapishwa leo Urusi imesema madai ya Umoja wa Ulaya hayana msingi na kwamba nchi hiyo haitokaa kimya juu ya kitendo hicho kisicho cha kirafiki. Umoja wa ulaya uliwawekea marufuku ya kusafiri na kuzuia mali za maafisa kadhaa wa Urusi, wakati nchi hiyo ilipowakamata mabaharia 24 na manuari za kijeshi za Ukraine kwenye mlango bahari wa Kerch mwezi Novemba mwaka jana.