Nilitokea kumpenda dada mmoja wakati nipo mlimani nasoma. Dada huyu alitokea mwanza alikuwa na dada yake mkubwa akiishi mtaani kwetu, walikuwa wamezaliwa baba mmoja ila mama zao mbali mbali ila wazazi wa huyu msichana wote walishafariki,alikuwa amemaliza secondary. Sister wake mkubwa akawa anamfanya Kama msichana wake wa kazi lakini nikamshauri aendelee kusoma atakubali ila akawa Hana uwezo wote wa kujilipia shule kwahiyo akawa anafanya kazi temporary huku anasoma na Mimi nilimsaidia baadae akaja kupata kazi tra na Mimi nikawa nimemaliza masomo yangu ila nikawa sijapata ajira kwahiyo nikawa namsaidia baba yangu kazi za ofisini kwake, huyu dada akaja kunibadilikia kabisa na kunifanya Mimi nionekane sio level yake kabisa uhusiano wetu ukafa ila niliumia sana, akawa hata akipita karibu na ofisini kwa mdingi na marafiki zake hanisalimii kabisaa! Nikawa najihisi vibaya sana, baadae nikapata scholarship ya kuja kusoma Japan nae akaenda kusoma holland, nilipomaliza masomo yangu nikapata kazi sasa amerudi bongo Hana kazi kwani tra alifukuzwa sababu hasa sijui ila kuna cheti chake kimoja alifoji na kutumia cha Mdogo wangu japokuwa uhusiano wetu ulikufa nikiwa bado nipo bongo sikuona sababu ya kumharibia maisha yake, kinachonishangaza ametafuta namba yangu ya simu na kunitumia texts kwamba amepata kazi kwenye ofisi ya ku print vitabu japokuwa sio taaluma yake ameamua afanye huku akitafuta kazi nyingine ila anaomba nimsaidie pesa za kujikimu baadae atanirudishia! Najiuliza angekuwa na maisha mazuri angenitafuta? Why now? Na inaonyesha amesahau yote alionifanyia! Na pia Ana dada zake wawili wa baba mmoja,mama mmoja wanaishi uk kwann wasimsaidie ndugu Yao? She seems to be in serious problem. Voice messages ni nyingi na texts, naombeni ushauri wakuu.