Why! CCM iko Kampeni,Wapinzani wamefungwa Midomo!

Ziara za Samia na Waziri Mkuu wake,Viongozi waandamizi wa CCM wote,wako kazini wakizunguka nchi nzima huku wakifanya mikutano ambayo,haina tofauti yoyote na ile ya Kampeni za uchaguzi mkuu.

Kama ni "T/shirt" zinagawiwa!
Kama ni "kofia" zonagawiwa!
Kama ni "vitenge na mitandio"inagawiwa!
Kama ni "wasanii" wanatumika ili kuvutia umati!

Kama ni kuomba kura zinaombwa kupitia wale wabunge wanaojifanya kutoa salamu.
Huku wakichombeza kwa kauli kama

"Hakika Hakuna Kama Mama...na ifikapo 2025,Mama ni wewe tu"

Na kisha kampeni inapigwa kwa Rais kutumia Muda wote wa hotuba zake,kusifu kazi za CCM,kwamba imeleta Mabilioni.....na Mengine bado yanakuja.....
Na baadae wanakaribishwa wapinzani sakatonge ambao tayari wameweka "MoU" na CCM ili kendeleza kampeni.
Kama ilivyofanyika huko Kigoma.

Hii kampeni ya
"Simika Samia" Tanzania bara,imeratibiwa kitaalamu kwa mgongo wa ziara ya Urais.

Lakini ukweli ni kwamba,Baada ya CCM kugundua kwamba Samia hana mizizi huku Tanzania bara.
Ndio ikaanza hii plan...kwa kuwapanga kwanza wakuu wa mikoa.wale ambao imeonekana ni watiifu zaidi kwa Samia.
Mfano rahisi ni huu:
Martini Shigella alikuwa Tanga,wakati wa uchaguzi wa 2020.mkoa wa Tanga ni mojawapo ya mikoa iliyoipatia CCM ushindi mkubwa katika chaguzi karibia zote huko nyuma 2015 na 2020.

Geita na Mwanza ni mikoa ambayo,bado CCM-Samia haina uhakika nayo,hasa baada ya kifo cha Magufuli(R.I.P).
Hivyo kwa muktada huo,ikaonekana Kwanza Engineer Robert Gabriel aliyekuwa Geita huku akionekana kutokuaminika kwa kuonekana kama mmoja wa Pro-Jpm...akaondolewa kwanza Geita,na kupelekwa Mwanza.
Kilichomtokea huko ikawa historia baada ya kuchomekewa "Askari jiji wamwaga Ndizi"
Na historia yake ikaishia hapo.

Sasa wamewaleta... Shigella-Geita.
Malima-Mwanza.

Na pia katika uchaguzi wa CCM uliopita,kwa mara ya kwanza tumeona watumishi wa serikali "Ma-DC" walioko kazini,wakigombea na kushinda ujumbe wa halmashauri na kamati kuu za CCM.
Mfano ni mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Murro.

Hawa Shigella na Malima wamewekwa ili kuutumia uzoefu walioupata wakiwa kule Tanga,na sasa wanatakiwa kuutumia huko kwenye vituo vipya.

Na matokeo yake yameanza kuonekana,maana juzi kilichoemdelea Geita ilikuwa ni "Simika Samia" na baadhi ya wahutubiaji walishindwa kutumia weledi....wakajikuta wakiropoka hadharani.mmoja alisikia akimtoa mama hofu kwamba " Mama usiwasikilize hao wanaosema sijui kuna Sukuma gang au sijui nini....hakuna lolote"
Huku zikitolewa zawadi kimkakati (Mbuzi na ng"ombe).

Na mwingine Makamba akiahidi kurudi kwa wajumbe wa kamati kuu ya taifa CCM,mkoa wa Geita."
miezi michache ijayo akiwa na ombi lake na yeye kwao"

Baadae ikachezwa hesabu,Samia akageuza mashambulizi kwenda Kigoma ambako tayari Zitto alikwisha andaliwa.,huku akimuachia PM Majaliwa akiingia Mwanza siku hiyohiyo kwa ziara ya siku moja,kwamba anakagua maendeleo ya miradi ya kimkakati.

My Take:
Sasa ni vema CCM ielewe kwamba haitendi haki kwa vyama vingine vya siasa nchini.
Pale ambapo wao wanazuiwa baadhi ya sehemu hata vikao vya ndani wanazuiwa na polisi.
Huku CCM wakizunguka watakavyo.

CCM na Serikali yake umefika wakati wa kuona AIBU kwa jambo hilo la msingi na kikatiba....liachiwe huru,ili kila chama kifanye siasa.
Ili wananchi wapate muda wa kuzichambua sera na madhaifu ya woote ikiwemo na CCM yenyewe.

Alamsiki.!
CC:
Pascal Mayalla
This is Tanzania chief
 
Hata Kenya walikuwa wanapiga Risasi kabisaaa....

Ebu niambie kinachoendelea huko kwa sasa,soma hii kama unao uwezo wa kusoma hiyo lugha!

Kenya's new president, William Ruto, said he had dissolved a police unit accused of extrajudicial killings, in a move hailed by human rights groups. The Special Service Unit (SSU), which was created more than two decades ago, has been in the spotlight as cases of disappearances and murders in the East African country soared in recent years. "We have disbanded the unit that was killing Kenyans arbitrarily," Ruto said on Sunday. "Security deteriorated and the police changed to killing Kenyans instead of protecting them," he added, referring to the tenure of the previous administration in which he was deputy president. Read more: Kenya disbands 'killer' police unit
Inatarajia hao krimu ya Chadema ni adui wa CCM? Karibu dining table uone!
 
Uko sahihi mkuu,lakini sasa tatizo ni kwamba Dunia onabadilika kwa kasi ya 5G na CCM ilipaswa kutumia weledi katika kufanya siasa zake,badala ya kuendelea na huu ambao nauita uzamani wa kisiasa.

Baba wa Taifa aliwahi kusema mwaka 1995 kule Dodoma wakati akihutubia kamati kuu ya CCM,iliyompitisha rasmi Mkapa kugombea urais na mimamnukuu...

"Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyaona au wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM," alisema Nyerere.....
Mwisho wa kunukuu.

Kwa hiyo,siasa ya sasa hivi inataka akili na sio mabavu kama zamani.
Sawa watu wanataka mabadiliko! Lakini, kwani wewe unaona CCM imelala? Si ndiyo unaona wanafanya kampeni (na kusema kwenye mikutano yao hiki tumefanya, kile tumefanya, kama mnataka hiki nacho tutafanya)? Usifikiri hawana macho na masikio kunusa watu wanataka nini. Mwaka 2015 watu walilia sana ufisadi, mikataba ya kinyonyaji, na unaona huko ndiko kulisababisha CCM waje na Magufuli wakijua fika wakija na mtu mwingine "watu watayatafuta mabadiliko nje ya CCM".

Miaka mitano ya Magufuli ilitumika kuwaaminisha watu kwamba CCM ina uwezo wa kuleta mabadiliko. Lakini lengo ni lile lile, aidha kwa kuwaaminisha watu kwamba CCM ndiyo chama pekee cha kuaminiwa na pia kwa kutumia nguvu ya dola kubaki madarakani bila kujali imani ya wananchi yote hayo mi naona ni usanii, CCM haina nia ya kutaka kutoka madarakani. Binafsi, baada ya miaka takribani 30 ya vyama vya siasa nchini, na kuona jinsi vyama vya siasa nchini vinavyoanzishwa na kufanya kazi, sidhani pia kama tunapaswa kuendelea kuentertain usanii wa kile kinachoitwa demokrasia nchini. Ni usanii, pure and simple. Ndio maana watu hulka ya Magufuli hawana uvumilivu hata kidogo kuhusu hizi demokrasia. Mfano kidogo: ukiangalia figisu zilizomwondoa Zitto chadema, ukamwona na Zitto alivyoanzisha chama chake akajiita yeye ni "kiongozi wa chama" yaani hapingwi, hashindanishwi, ni wa kudumu, unapata picha kabisa kwamba at the core vyama vya upinzania ni ubinafsi mtupu.

Now linganisha na CCM, pamoja na mapungufu yao yote, jinsi walivyojikita na kufanya kazi kama taasisi, wanavyochaguana kuanzia mashinani, vijana wa aina zote, kutoka pale Tanzania wanavyojitolea na kuanza kulelewa kwenye mizizi ya siasa za CCM, sometimes tuache unafiki, nchi hii ni nchi ya chama kimoja tu.
 
Wewe hukuwa mataga awamu iliyopita??!
Tatizo ni kwamba hili la siasa linagusa maisha ya kila siku ya kila mtanzania,na CCM inawaona watanzania kama wasiojitambua wala kuyaona hayo yanayoendelea.
 
Ziara za Samia na Waziri Mkuu wake,Viongozi waandamizi wa CCM wote,wako kazini wakizunguka nchi nzima huku wakifanya mikutano ambayo,haina tofauti yoyote na ile ya Kampeni za uchaguzi mkuu.

Kama ni "T/shirt" zinagawiwa!
Kama ni "kofia" zonagawiwa!
Kama ni "vitenge na mitandio"inagawiwa!
Kama ni "wasanii" wanatumika ili kuvutia umati!

Kama ni kuomba kura zinaombwa kupitia wale wabunge wanaojifanya kutoa salamu.
Huku wakichombeza kwa kauli kama

"Hakika Hakuna Kama Mama...na ifikapo 2025,Mama ni wewe tu"

Na kisha kampeni inapigwa kwa Rais kutumia Muda wote wa hotuba zake,kusifu kazi za CCM,kwamba imeleta Mabilioni.....na Mengine bado yanakuja.....
Na baadae wanakaribishwa wapinzani sakatonge ambao tayari wameweka "MoU" na CCM ili kendeleza kampeni.
Kama ilivyofanyika huko Kigoma.

Hii kampeni ya
"Simika Samia" Tanzania bara,imeratibiwa kitaalamu kwa mgongo wa ziara ya Urais.

Lakini ukweli ni kwamba,Baada ya CCM kugundua kwamba Samia hana mizizi huku Tanzania bara.
Ndio ikaanza hii plan...kwa kuwapanga kwanza wakuu wa mikoa.wale ambao imeonekana ni watiifu zaidi kwa Samia.
Mfano rahisi ni huu:
Martini Shigella alikuwa Tanga,wakati wa uchaguzi wa 2020.mkoa wa Tanga ni mojawapo ya mikoa iliyoipatia CCM ushindi mkubwa katika chaguzi karibia zote huko nyuma 2015 na 2020.

Geita na Mwanza ni mikoa ambayo,bado CCM-Samia haina uhakika nayo,hasa baada ya kifo cha Magufuli(R.I.P).
Hivyo kwa muktada huo,ikaonekana Kwanza Engineer Robert Gabriel aliyekuwa Geita huku akionekana kutokuaminika kwa kuonekana kama mmoja wa Pro-Jpm...akaondolewa kwanza Geita,na kupelekwa Mwanza.
Kilichomtokea huko ikawa historia baada ya kuchomekewa "Askari jiji wamwaga Ndizi"
Na historia yake ikaishia hapo.

Sasa wamewaleta... Shigella-Geita.
Malima-Mwanza.

Na pia katika uchaguzi wa CCM uliopita,kwa mara ya kwanza tumeona watumishi wa serikali "Ma-DC" walioko kazini,wakigombea na kushinda ujumbe wa halmashauri na kamati kuu za CCM.
Mfano ni mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Murro.

Hawa Shigella na Malima wamewekwa ili kuutumia uzoefu walioupata wakiwa kule Tanga,na sasa wanatakiwa kuutumia huko kwenye vituo vipya.

Na matokeo yake yameanza kuonekana,maana juzi kilichoemdelea Geita ilikuwa ni "Simika Samia" na baadhi ya wahutubiaji walishindwa kutumia weledi....wakajikuta wakiropoka hadharani.mmoja alisikia akimtoa mama hofu kwamba " Mama usiwasikilize hao wanaosema sijui kuna Sukuma gang au sijui nini....hakuna lolote"
Huku zikitolewa zawadi kimkakati (Mbuzi na ng"ombe).

Na mwingine Makamba akiahidi kurudi kwa wajumbe wa kamati kuu ya taifa CCM,mkoa wa Geita."
miezi michache ijayo akiwa na ombi lake na yeye kwao"

Baadae ikachezwa hesabu,Samia akageuza mashambulizi kwenda Kigoma ambako tayari Zitto alikwisha andaliwa.,huku akimuachia PM Majaliwa akiingia Mwanza siku hiyohiyo kwa ziara ya siku moja,kwamba anakagua maendeleo ya miradi ya kimkakati.

My Take:
Sasa ni vema CCM ielewe kwamba haitendi haki kwa vyama vingine vya siasa nchini.
Pale ambapo wao wanazuiwa baadhi ya sehemu hata vikao vya ndani wanazuiwa na polisi.
Huku CCM wakizunguka watakavyo.

CCM na Serikali yake umefika wakati wa kuona AIBU kwa jambo hilo la msingi na kikatiba....liachiwe huru,ili kila chama kifanye siasa.
Ili wananchi wapate muda wa kuzichambua sera na madhaifu ya woote ikiwemo na CCM yenyewe.

Alamsiki.!
CC:
Pascal Mayalla
Kwani upinzani bado uko Tanzania ? Hauko serious.
 
Uko sahihi mkuu,lakini sasa tatizo ni kwamba Dunia onabadilika kwa kasi ya 5G na CCM ilipaswa kutumia weledi katika kufanya siasa zake,badala ya kuendelea na huu ambao nauita uzamani wa kisiasa.

Baba wa Taifa aliwahi kusema mwaka 1995 kule Dodoma wakati akihutubia kamati kuu ya CCM,iliyompitisha rasmi Mkapa kugombea urais na mimamnukuu...

"Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyaona au wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM," alisema Nyerere.....
Mwisho wa kunukuu.

Kwa hiyo,siasa ya sasa hivi inataka akili na sio mabavu kama zamani.
Hiyo akili mnayo ? Usijitekenye
 
Kitakachowapiga butwaa CCM safari hii ni jinsi hizo nyayo zao zitakavyofutika kwa spidi ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Heri wawaruhusu wenye mawazo tofauti mapema lakini wanavyoendelea kuwazuia ndivyo kiu ya kusikiliza mawazo mbadala inavyozidi kukua.

Kwa akili zao ndogo ngoja waendelee kusakata rumba peke yao uwanjani wakidhani wanawakomesha wenzao....

Watakaposhtuka watakuta wamechuja kama nguo za mtumba kutoka China!
CCM haichuji kamwe CHADEMA ndio imechuja na iko mahututi mochware ya kisiasa.
 
Sawa watu wanataka mabadiliko! Lakini, kwani wewe unaona CCM imelala? Si ndiyo unaona wanafanya kampeni (na kusema kwenye mikutano yao hiki tumefanya, kile tumefanya, kama mnataka hiki nacho tutafanya)? Usifikiri hawana macho na masikio kunusa watu wanataka nini. Mwaka 2015 watu walilia sana ufisadi, mikataba ya kinyonyaji, na unaona huko ndiko kulisababisha CCM waje na Magufuli wakijua fika wakija na mtu mwingine "watu watayatafuta mabadiliko nje ya CCM".

Miaka mitano ya Magufuli ilitumika kuwaaminisha watu kwamba CCM ina uwezo wa kuleta mabadiliko. Lakini lengo ni lile lile, aidha kwa kuwaaminisha watu kwamba CCM ndiyo chama pekee cha kuaminiwa na pia kwa kutumia nguvu ya dola kubaki madarakani bila kujali imani ya wananchi yote hayo mi naona ni usanii, CCM haina nia ya kutaka kutoka madarakani. Binafsi, baada ya miaka takribani 30 ya vyama vya siasa nchini, na kuona jinsi vyama vya siasa nchini vinavyoanzishwa na kufanya kazi, sidhani pia kama tunapaswa kuendelea kuentertain usanii wa kile kinachoitwa demokrasia nchini. Ni usanii, pure and simple. Ndio maana watu hulka ya Magufuli hawana uvumilivu hata kidogo kuhusu hizi demokrasia. Mfano kidogo: ukiangalia figisu zilizomwondoa Zitto chadema, ukamwona na Zitto alivyoanzisha chama chake akajiita yeye ni "kiongozi wa chama" yaani hapingwi, hashindanishwi, ni wa kudumu, unapata picha kabisa kwamba at the core vyama vya upinzania ni ubinafsi mtupu.

Now linganisha na CCM, pamoja na mapungufu yao yote, jinsi walivyojikita na kufanya kazi kama taasisi, wanavyochaguana kuanzia mashinani, vijana wa aina zote, kutoka pale Tanzania wanavyojitolea na kuanza kulelewa kwenye mizizi ya siasa za CCM, sometimes tuache unafiki, nchi hii ni nchi ya chama kimoja tu.
True100%
 
Mkuu zimmerman !

Hoja au topic yako iko vizuri sana,pia nikupongeze kwa jinsi unavyotumia muda wako vizuri kwa kusoma topic za wenzako kwa umakini na hatimae kuja na uchamgiaji wenye tija.
Uko pia sahihi kuhusu CCM kufanya mambo yake kimfumo tofauti na vyama vingine vya kisiasa nchini.

Tatizo langu kubwa kwa CCM ni pale isiporuhusu siasa kufanywa kwa uhuru na vyama vyote vya siasa.

Kwa s ababu,kuvizuia kufanya siasa za majukwaani,kunavipa nguvu kwa wananchi,kuliko ambavyo vingeachwa na kufanya siasa zao, hatimae wananchi wakachagua ni yupi mwenye sera mahsusi za kumletea maendeleo chanya.(nadhani soon wangegundua kwamba wameishiwa).

Vyama vingine pia vingeachwa viendelee majukwaani na huku CCM pia ikifanya kote kote .
Namaanisha majukwaani pamoja na serikalini kwa kuwatumikia wananchi,huku kikitimiza ahadi zake za ilani yao ya uchaguzi.

Pia CCM ingenufaika kwa vyama vingine kufanya siasa,kwani ndio njia pekee ambayo wangekuja ni wapi wanaboronga na wapi wanafsnya vizuri kutokana na ukosoaji wa wapinzani wao kisiasa.

Jambo lingine baya linalofanywa na CCM ni pale linapokuwa na "Political Cartel" ndani ya chama cha CCM.

Kwamba badala ya CCM kufuata matakwa ya wanachama walio wengi,wao wanalazim8sha walio wengi wafuate amri za kundi dogo la mabwanyenye ndani ya CCM.

Ahsante.
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Na labda niliweke wazi kabisa kwamba CCM wao wanaamini nchi ni ya chama kimoja...bhaasi. Uwepo wa vyama vingi ni kuwazuga wale wanaoitwa "wafadhili". Sasa ni vigumu sana kufanya kazi ya siasa za vyama vingi katika nchi ambayo kifalsafa siyo ya vyama vingi. Na hapo ndipo ninapotofautiana sana na wazungu wanaolazimisha model yao iwe model ya kila sehemu. Kulazimisha huko ndiko kunakofanya CCM wafanye siasa za ulaghai, kiuhalisia hawataki ushindani, lakini kwenye makaratasi wanatakaka kuiambia dunia (na watanzania) kwamba kuna ushindani. Sasa mtu kama wewe mwenye uelewa mtambuka hupaswi kuishi kwa kulaghaiwa.

Na katika dunia hii iliyojaa unafiki naona wanaoumia zaidi kwa sasa kwa siasa za aina hii ni wanachama wa kawaida wa vyama vya siasa za upinzani (au watu neutral wanaopenda siasa za hoja za ushindani). Lakini viongozi wakuu wa vyama vya upinzani washausoma na kuujua huu mchezo, na wamesharidhika na wanachotaka ni kutaka kufaidika na "nafasi" walizonazo kwenye siasa za nchi hii. So mtu kama Magufuli anapokuja na kuvuruga system maslahi hiyo, dah! wanamuona na mtu hatari sana. Mtu mwingine kama Samia anayeonekana kutaka kurudi kwenye ile system ya kula na kipofu ila usimshike mkono lazima wamwone ni afadhali sana. Hapa tunachosubiria ni kuanza rasmi kwa siasa za majukwaani kwa wapinzani, na naweza kusema kinachochelewesha labda ni hofu ya mama ya kutotaka kuonekana ni anti-Magufuli kwa pro-Magufulians (ambao wapo, ni wengi na wana nguvu pia).
 
zimmerman

"wakuu wa vyama vya upinzani washausoma na kuujua huu mchezo, na wamesharidhika na wanachotaka ni kutaka kufaidika na "nafasi" walizonazo kwenye siasa za nchi hii. So mtu kama Magufuli anapokuja na kuvuruga system maslahi hiyo, dah! wanamuona na mtu hatari sana. Mtu mwingine kama Samia anayeonekana kutaka kurudi kwenye ile system ya kula na kipofu ila usimshike mkono lazima wamwone ni afadhali sana. Hapa tunachosubiria ni kuanza rasmi kwa siasa za majukwaani kwa wapinzani, na naweza kusema kinachochelewesha labda ni hofu ya mama ya kutotaka kuonekana ni anti-Magufuli kwa pro-Magufulians (ambao wapo, ni wengi na wana nguvu pia)."

Ni kwa mantiki hiyo ya kuhofia vyama vya upinzani pamoja na Pro-Maguguli.

Ambayo imepelekea CCM kuingia kazini kimkakati ili kumsimika kwanza Samia huku Bara,ili muda si mrefu zoezi hilo litakapo kamilika.

Ndio sasa waruhusu siasa za majukwaani kuanza.
Maana tayari watakuwa wameishajiaminisha.
Kumaliza kazi ya kuwa brain wash wananchi wa kawaida kote nchini.

Hivyo ninakubaliana na wewe,kwamba Samia sio mpenda Demokrasia kama anavyojinadi.
Bali anafanya maigizo hayo,ili apate uungwaji mkono toka kwa wahisani na wafadhili wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom