voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,944
Ziara za Samia na Waziri Mkuu wake,Viongozi waandamizi wa CCM wote,wako kazini wakizunguka nchi nzima huku wakifanya mikutano ambayo,haina tofauti yoyote na ile ya Kampeni za uchaguzi mkuu.
Kama ni "T/shirt" zinagawiwa!
Kama ni "kofia" zonagawiwa!
Kama ni "vitenge na mitandio"inagawiwa!
Kama ni "wasanii" wanatumika ili kuvutia umati!
Kama ni kuomba kura zinaombwa kupitia wale wabunge wanaojifanya kutoa salamu.
Huku wakichombeza kwa kauli kama
"Hakika Hakuna Kama Mama...na ifikapo 2025,Mama ni wewe tu"
Na kisha kampeni inapigwa kwa Rais kutumia Muda wote wa hotuba zake,kusifu kazi za CCM,kwamba imeleta Mabilioni.....na Mengine bado yanakuja.....
Na baadae wanakaribishwa wapinzani sakatonge ambao tayari wameweka "MoU" na CCM ili kendeleza kampeni.
Kama ilivyofanyika huko Kigoma.
Hii kampeni ya
"Simika Samia" Tanzania bara,imeratibiwa kitaalamu kwa mgongo wa ziara ya Urais.
Lakini ukweli ni kwamba,Baada ya CCM kugundua kwamba Samia hana mizizi huku Tanzania bara.
Ndio ikaanza hii plan...kwa kuwapanga kwanza wakuu wa mikoa.wale ambao imeonekana ni watiifu zaidi kwa Samia.
Mfano rahisi ni huu:
Martini Shigella alikuwa Tanga,wakati wa uchaguzi wa 2020.mkoa wa Tanga ni mojawapo ya mikoa iliyoipatia CCM ushindi mkubwa katika chaguzi karibia zote huko nyuma 2015 na 2020.
Geita na Mwanza ni mikoa ambayo,bado CCM-Samia haina uhakika nayo,hasa baada ya kifo cha Magufuli(R.I.P).
Hivyo kwa muktada huo,ikaonekana Kwanza Engineer Robert Gabriel aliyekuwa Geita huku akionekana kutokuaminika kwa kuonekana kama mmoja wa Pro-Jpm...akaondolewa kwanza Geita,na kupelekwa Mwanza.
Kilichomtokea huko ikawa historia baada ya kuchomekewa "Askari jiji wamwaga Ndizi"
Na historia yake ikaishia hapo.
Sasa wamewaleta... Shigella-Geita.
Malima-Mwanza.
Na pia katika uchaguzi wa CCM uliopita,kwa mara ya kwanza tumeona watumishi wa serikali "Ma-DC" walioko kazini,wakigombea na kushinda ujumbe wa halmashauri na kamati kuu za CCM.
Mfano ni mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Murro.
Hawa Shigella na Malima wamewekwa ili kuutumia uzoefu walioupata wakiwa kule Tanga,na sasa wanatakiwa kuutumia huko kwenye vituo vipya.
Na matokeo yake yameanza kuonekana,maana juzi kilichoemdelea Geita ilikuwa ni "Simika Samia" na baadhi ya wahutubiaji walishindwa kutumia weledi....wakajikuta wakiropoka hadharani.mmoja alisikia akimtoa mama hofu kwamba " Mama usiwasikilize hao wanaosema sijui kuna Sukuma gang au sijui nini....hakuna lolote"
Huku zikitolewa zawadi kimkakati (Mbuzi na ng"ombe).
Na mwingine Makamba akiahidi kurudi kwa wajumbe wa kamati kuu ya taifa CCM,mkoa wa Geita."
miezi michache ijayo akiwa na ombi lake na yeye kwao"
Baadae ikachezwa hesabu,Samia akageuza mashambulizi kwenda Kigoma ambako tayari Zitto alikwisha andaliwa.,huku akimuachia PM Majaliwa akiingia Mwanza siku hiyohiyo kwa ziara ya siku moja,kwamba anakagua maendeleo ya miradi ya kimkakati.
My Take:
Sasa ni vema CCM ielewe kwamba haitendi haki kwa vyama vingine vya siasa nchini.
Pale ambapo wao wanazuiwa baadhi ya sehemu hata vikao vya ndani wanazuiwa na polisi.
Huku CCM wakizunguka watakavyo.
CCM na Serikali yake umefika wakati wa kuona AIBU kwa jambo hilo la msingi na kikatiba....liachiwe huru,ili kila chama kifanye siasa.
Ili wananchi wapate muda wa kuzichambua sera na madhaifu ya woote ikiwemo na CCM yenyewe.
Alamsiki.!
CC:
Pascal Mayalla