Pia ni kwakuwa wana MUNGU wa kweli..teh teh teh..natania tu jamani!
Sio utani mtu wangu, like it or not, kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu unasaidia sana tu. Mimi nimesoma shule ya kikatoliki (sio seminari) na kusali ilikuwa ni lazima kiasi kwamba you grow to enjoy it. Na whether you agree or not, ni one of the factors zinazoset shule hizi apart.
I would also like to disagree a bit with a comment made earlier. Wanafunzi wanaoenda shule hizi za kikatoliki au seminari sio special in any way. I believe mwanafunzi yeyote anaweza akafanya vizuri akilelewa na akafuata sheira katika mazingira ya shule hizi. Ndio maana wapo wanaoshindwa na wanaacha shule na wale wanaobaki na kufuata sheria na mienendo inayokuwa encouraged na shule hizi wanafaulu vizuri.
Kama shule zetu za serikali zingekuwa na madarasa yenye wanafunzi wasiozidi arobaini tuseme, wana maktaba zenye vitabu vyote vinavyotakiwa, wana maabara zenye vifaa vya kutosha, wana walimu wanaojali mwanafunzi asipofanya homework kwa mfano na ambao wanalipwa vizuri kiasi kwamba wanapenda fani zao na wako tayari kujitolea muda wao kufundisha wanafunzi hata iwe usiku au wikiendi. Shule hizi zingekuwa na ratiba ya kusoma inayoeleweka isiyokuwa interrupted na mambo kama ukosefu wa chakula uliosababisha shule zifungwe au sijui matatizo gani, ratiba isiyoruhusu muda wa idleness, kila kitu kiko systematic. Mi nafikiri shule hizi zingefaulu way more than zinavyofanya sasa hivi.
Lakini, we all know, condition ya shule za serikali tena hasa za kata ni the total opposite of what I have just described. This is a problem that will take a while to fix especially considering that ni shule hizi za serkali zinazoaccomodate maelfu ya wanafunzi throughout our country. Ila kama serikali yetu ikiwa na nia ya ukweli ya kuendeleza quality ya elimu yetu then our future could be brighter!
By the way, a point of correction, sijui kwa nini watu wana hii idea kwamba shule za kikatoliki zina chakula kizuri. Trust me when I say, they don't. Shule yetu tumelishwa ugali wa dona kwa maharage yaliyochemshwa mondays through fridays. Nyama ilikuwa mara mbili kwa mwezi, na wali maharage unapikwa huku maharage yanachanganywa na cabbage humo humo, chai ya maziwa tulikuwa tunapata mara moja kwa wiki tena maziwa ya unga. Kaka yangu kasoma seminari na siku wakila kitimoto (ambao wanafuga wao wenyewe seminarini) unaona nyama na nyanya zikielea kwenye maji hadi unaweza kubadilisha mawazo ya kula...and the list goes on. Au labda waliokuwa wanacomment, mlikuwa mnalinganisha chakula hiki na cha wapi?