Uchaguzi 2020 Why Bernard Membe is not a presidential material, at all!

Kiukweli CCM ya leo siyo ile CCM yenye pesa nje nje mzee kabana
mkuu inasemekana wanaccm asili wanaona wametengwa na wapinzani wanapendelewa hasa. siri ya kina Sofia simba kuteuliwa kwenye nyadhifa serikalini ni jitihada za Magu kujaribu kuzima hizo lawama za chinichini.
 
Hii ccm ya kuchezea box la kura kimachomacho limemuibua Membe. Wanaccm wengi sasa wanaona fika Magu na genge lake wameshindwa kufanya siasa za ushindani bali wamebaki kuburuza wananchi bila ridhaa yao. Kitendo cha Magu kuhakikisha mgombea wa ccm tena aliyemtoa upinzani na kuhakiksha anatangazwa mshindi kimewaacha wanaccm asilia na donge moyoni, hivyo wameamua wamtoe mapema.

Na hivi viashiria vya magu kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani kimemfanya jasusi Membe kutoka alipokuwa kwani wanajua kabisa wakikaa kimya jamaa atajiongezea muda maana haheshimu box la kura. Hivyo kuna kundi kubwa ndani ya ccm halikubaliani na mwenendo wa magu na wameapa 2020 kumpiga chini.
Hii ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano...
 
Kwanza:Kama kuna mtu anatamani kuiepusha Tanzania kwa sasa na mwanzo mbaya wa VISASI anapashwa aje na ajenda ya katiba mpya, tunaponzwa na kuamini katika nguvu ya mtu badala ya nguvu ya Taasisi husika.
Pili: naichungulia Tanzania inayoanza kuwaza matumizi ya nguvu badala ya matumizi ya hoja
Tatu:Yanayotokea sasa yananikumbusha enzi za chama kimoja ambapo njama za mapinduzi ya serikari zilijitokeza Mara name, Tangu 1992 hakujawahi kuwa na njama hizo kalini nahisi hali hii imeanza kurudi katika mawazo wa watu
Mwisho: KATIBA NI SURUHISHO, naamini sasa hata akija malaika inawza kuwa ngumu kutawala kwa katiba hii
 
Hapana sio kweli. Hii nchi ni ya wazalendo! Wasio wazalendo hawataki hii nchi ilendelee ku-exist. Ndiyo maana wanapinga kila kitu.

Clews;
1. Bombardier walizipinga mpaka kutumia mbinu ya kutafuta makampuni ya kutushtaki. Sasa wanapanda.

2. Dreamliner waliipinga sasa wanapanda.

3. SGR waliipinga, nadhani wataipanda.

4. Golf over waliipinga, lakini sasa wanazitumia.

5. Sheria mpya za kudhibiti uporaji wa madini yetu waliipinga na kuligomea Bunge.

6. Ukuta wa Mererani wa kulinda madini yetu ya Tanzanite yasiibiwe nao waliupinga na bado wanaupinga.

Do they really belong to Tanzania? Of course not!

Ningependa uasili wa Zitto Kabwe na Tundu Lissu uchunguzwe!
Wachunguzwe kwa kuwaza tofauti ma wewe?!
 
Benard Membe hawezi kusimama na John Magufuli hata kwa dakika 20. Kazi ya Magufuli inaonkena lakini ya Membe ni kusimulia/kujinadi zaidi, kila Mtu anaamini katika ishara na Vitendo sio rahisi kuwaaminisha Watanzania kwamba Membe anamzidi Magufuli sio rahisi!
 
Niaminishe hata kidogo mkuu, kuwa Membe ana nguvu kuliko alizokuwa naxo Lowassa ndani ya ccm, make huku kanda ya ziwa hata hatumjui, kma tulivyomjua Lowassa.
Nguvu ya Membe kufika 2020 itategemea sana matendo ya jiwe.Jiwe linaweza either kujimaliza or kujijenga pale tu litakapoanza kuwekeza katika ustawi wa jamii kifedha na si katika vitu kama lifanyavyo sasa!Any way muda ni mwalimu mzuri
 
Membe wanamtaka ili arudishe ufisadi Tanzania.

Lissu na Malim Seif wanawataka ili kuja kuvunja muungano na umoja wetu. Tanzania iwe Tanganyika dependent state na Zanzibar irejeshwe tena kwa Sultan wa Oman.
Ndio nyimbo za CCM hizi sio enzi za Marehemu KOMBA.
 
Watu wanashangaza sana! Kuwa Membe hafai kuwa Rais wa Tanzania!! Sasa huyu wa sasa ana uwezo gani wa kuongoza? Nini kimebadilika hasa ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wake? Na vipi yeye aliandaliwa na nani wakati nasikia hata kuwahi kushika nafasi ya chini ndani ya Chama hakuwahi pia, zaidi ya kuwa Mbunge wa Chama hicho!!

Maendeleo ya watu au maisha ya Watanzania wengi hasa wa chini yameimarika kwa kiwango gani? Hakuna la zaidi tu bora CCM ibadili mfumo wake wa kihafidhina wa mihula miwili, imtose Dr Magufuli miaka 5 inamtosha tu.
Hapana mkuu hapo nakupinga. Kwa kusema hivyo humtendei haki Rais wetu.

Nakubali maisha ya watu hayajabadilika sana zaidi ya kuwa watumishi wa serikali wananidhamu na kidogo hawajioni kama wao ni miungu wadogo na ofisi sio zao tena. Watu walio bahatika kuajiliwa kwenye ofisi, makampuni na mashirika ya umma walikuwa wanatumia ovyo sana nafasi na madaraka yao kwa kuwa nyanyasa watanzania wenzao.

Mfano; Nakumbuka siku za nyuma sana, dada yangu aliyekuwa anafanya kazi NPF wakati ule, alilia wiki nzima baada ya yeye kwa amri ya boss wake kumdhulumu baba wa watu mzee pension yake. Huyo mzee wakati ule, kulingana na maelezo ya dada yangu, ilikuwa apate shilingi elfu 21, kwa wakati ule ni hela nyingi sana, badala yake alipata shilingi elfu 13 tu.

Sasa kwa bahati mbaya au mzuri huyo dada yangu alimkuta huyo mzee kwenye ngazi za mlango wa kuingilia hiyo ofisi, wakati anarudi kutoka lunch mchana, machozi yakimtoka kwa kudhulumiwa hela zake ambazo mwenyewe alikwisha zipangia bajeti, labda ya kununua nyumba nakadhalika.

Dada yangu alikuwa mhasibu (book keeping). Alipo mwuuliza shida ni nini? Ndiyo akapata hiyo story. Ilimuuma sana.

Kwa hiyo mkuu kama wewe hukupata manyanyaso kama hayo kwenye serikali za awamu za nyuma basi inawezekana mwenzetu utakuwa aidha ndiyo mmojawao wa watendaji wa manyanyaso hayo au kwa uwezo na fursa uliyo kuwa nayo wakati huo, haikukubidi kuwa confronted na watumishi wa umma. Hiyo ilikuwa karibu kila sekta.


Na yeye aliwahi kusema kuwa kazi yake ni ngumu anajuta, CCM impumzishe tu Dr Magufuli.
Kwa hili hata mimi naona Rais hakustahili kusema hivyo. Kama yeye mwenyewe aliamua kuchukua form za kugombea urais hanabudi kulalamika. Kama kazi zina mhelemea basi ajiuzuru, lakini sio kuwakatisha tamaa viongozi wa kesho. Kama Pop anaweza kujiuzuru kwanini ishindikane kwa Rais?

Kwa kukupa matumaini tu mkuu, mimi binafsi nina uhakika Magufuli hakuwa chaguo la kwanza la Rais Kikwete na makada wa CCM, ila baada ya wao kuona Lowassa ameingia upinzani kwa kishindo, hapo nafikiri plan yao iliwatoka. Wakaona hatari iliyo kuwa mbele yao kama yeye angeshinda uchaguzi. Angelipiza kisasi, maana alikuwa na Bifu nao. Wangemkoma!

Katika kupiga mahesabu yao wakaona hawana budi kumteua mgombea ambaye kidogo wananchi wengi wanaimani yaye, ambaye ni Magufuli tu ili ku-neutralize hasira ambazo wananchi walizo kuwa nazo dhidi ya viongozi wa CCM.
 
Back
Top Bottom