Who's next Kisutu magistrate court?

Who's next Kisutu magistrate court?

Mh!! Mi nadhani hivi vichwa vifuatavyo vikitinga pale kisutu tunaweza kuona mwanga kuelekea ushindi katika hii vita ya Ufisadi....Mgonja, Chenge,Karamagi,Sumaye,Mkapa,Vincent Mrisho,Chenge,Rostam....

Mmeshaambiwa na DPP kuwapeleka wote hao mahakamani kwa wakati mmoja ni hatari kwa uchumi na usalama wa nchi.

Mramba na Yona wametolewa kafara. Waliobaki wataendelea kupeta tu!
 
Rostam na Bro Edo wanagusika tena saana tu.Na hawana ubavu kama wa Zuma.Zuma nguvu yake kubwa ni kuwa alikuwa mpiganaji hodari wa ANC, hao jamaa sijui walipigania nini zaidi ya ufisadi na kujilimbikizia mali.And they DONT have public support ,la wale waliowekwa katika positions na pochi zao-habari ndo....
 
Nasikia leo huyo manji hajaamka mpaka saa hizi-kalala tu
 
Nasikia leo huyo manji hajaamka mpaka saa hizi-kalala tu


Madawa yamemzidia!!!! Mahakamani Yona na Mramba!!! Mengi yatatibuka!!! Ya vitalu vya uwindaji, madini, n.k. Hivi mambo ya Import Support yalifanyika wakati gani?? wa mramba au Yona wakiwa Finance Minister???? The government is shaking!!!! Amani imeshatoweka, vimebaki umaskini uliokithiri kwa wengi na ubepari kwa wachache. Karl Max philosophies zimeshinda!!! Watalala weeeeee, mwishowe watalala kimoja!!! Msongo wa mawazo!!!
 
Abdalla Kigoda, aliyekuwa mshauri wa BWM kwa uchumi na uwekezaji, ina maana hukukatiwa 10 percent katika madudu yote ya ufisadi wa awamu ile? Kama Takukuru iko macho, naye watamsomboroa tuu.
 
Mkuu Mshiiri
Please rudisha kale ka picha kako ka mshiiri kweli...unajua thread inaweza kuwa inasua sababu hirizi umeiweka kabatini, ivae mkuu

OK kwa heshima na taadhima ka picha hako hapo au ni kengine Mwalimu Zawadi. Pls advise immediately. Wengi anyway wameniPM wakiomba nikarudishe kwani wanakapenda sana na nikaweka kiasi kuwa wakifika 200 wanaoomba karudi nitakarudisha. Sasa kwa maana hiyo wewe umejazia namba na sasa rasmi nakarudisha. Heshima kwa wote JF members.
 
For the correct who is next Kisutu Magistrate Court will receive 100,000TAS from Mshiiri. Offer ending 30-11-2008 at 0600am. i.e. One has to post the name(s) of who is next Kisutu next week as from now and deadline is 30-11-2008 at 0600am. The marking scheme will be by precedent on forum archieve. Naomba kuwakilisha.
 
Mkuu Mshiri,
Mi nashauri hizo laki moja ni heri umpatie Invisible kwa ajili ya kuendeleza na kusupport forum, kuliko kuweka kamali kwa atakayeleta habari wa kwanza.

Najua ni haki yako kuweza kuahidi donge nono kwa kitu chochote kile lakini nahofia athari yake kama tabia hii ikishika kasi tunaweza kupoteza mwelekeo wa mapambano haya ya kulipeleka taifa letu mbele.

Mifano michache tu ya athari zinazoweza kutokea:
-- Huyo mshindi wa hizo habari itabidi akupe details zake au muonane ana kwa ana ili aweze kupata zawadi yake, sasa hii inaweza kuhatarisha uwepo wake hapa maana identity yake tiyari itakuwa exposed (hatujui lengo lako).

-- Mtu mwingine anaweza kuwa anazo habari kamili lakini hataki kushiriki kwenye sindano lako kwa hiyo akaahirisha kuiweka hiyo habari hapa kwahiyo kuwanyima wana forum haki yao ya kupata habari.

-- Mwingine anaweza kuanzisha shindano kama hili lako ili awapate anaowatafuta, maana hapa kuna alias flan hivi zinajulikana zina information flan sasa fisadi au asiyewatakia mema anaweza kuweka shindano huku akijua kabisa flani ana uwezekano mkubwa wa kujibu kwahiyo kumpata.
 
Back
Top Bottom