Baada ya vita vya pili vya dunia, miji ya Wajerumani ilibaki kama hii picha hapa chini, walishushwa hadi sifuri, wameteseka sana na kuamka upya, hawana hamu ya vita tena, hawataki kuskia hicho kitu, leo hii Ujerumani ndio second largest exporter in the world, hivyo anategemea sana majirani zake kiuchumi, hawezi akazingua.
Ili ufanikishe vita, lazima upate uungwaji mikono na raia wako, wajerumani walitenganisha jeshi na siasa, yaani baada ya ya kuona kitu walifanyiwa na NAZI.
Kwa kifupi mataifa yote ambayo yamewahi kulemazwa na full scale war na kuamka, huwa hayana hamu tena ya kurudi huko, ni kama leo uwaambie Watanzania wakusanyike tena dhidi ya Uganda kama ilivyokua kwenye vita dhidi ya Idi Amin, ikikumbukwa mpaka leo hawajanyanyuka kabisa kutokana na hasara waliyopata wakati ule, Pi ukumbuke leo hii Tanzania na Uganda wanategemeana pakubwa kibashara, ndivyo ilivyo kwa Uingereza na Ujerumani, kizazi cha leo kinategemeana sana, ni vigumu kuwapiganisha.