Labda tuulize pia who is the star minister in this government? Maana wakati wa Nyerere walikuwepo akina Sokoine; wakati wa Mwinyi-akina Mrema; na kwa Mkapa walikuwepo akina Magufuli. Who is a star minister in this guy's government?
Nadhani tukubaliane na hiyo hoja yako,lakini ktk kipindi hiki itakuwa ngumu,kwa sababu awamu hii imejaa viongozi wengi ambao walikuja kwa mvuto na wote walipendelea sana kung'ara kama alivyo JK mwenyewe lakini wakasahau kuwa mng'aro wa JK ni KARAMA za mungu na si nguvu za kibinadamu.
Wakati wa Mwalimu alifanya kila awezalo ku shine yeye kama Mkuu ni Sokoine tu ndie aliyethubutu kujipambanua na kutawala mioyo ya waTZ,walikuwepo viongozi waliokuwa na mvuto lakini hawakupewa nafasi hiyo kwa makusudi au bahati mbaya na zaidi ni mfumo wa kimangimeza ulokuwepo ktk jamii yetu na watawala,Mwinyi yeye hakuwa na mng'aro mkubwa bali presidency ndiyo iliyomjenga hivyo alijikuta anarithi mfumo uliompatia mamlaka lakini alichelewa kung'amua kuwa asingeliweza kufanikisha malengo yake kwa taifa,mataifa na siasa kwa yeye kujaribu kuwa mrithi bora wa Mwalimu,alipoligundua hilo ndio changes za 1990 pale aliweza kutupatia sura yake rasmi ingawaje kwa kutojiamini sana maana bado alikuwa anajiona Mzanzibar zaidi kuliko TZ ambayo yeye ndiye rais wetu;kosa hilo lilimnyima mandate ya kurithisha mtu kiti hicho na Mwalimu akatupatia Ben,lakini 5yrs yake ya mwisho aliwawezesha wanasiasa wengi kujipambanua,JSM,Lyatonga,Kighoma,Lowasa,JK,Amina Salum Ally,nk.
Benj alipoingia alichofanya ni kutupatia PM asiye na nuru ktk jamii hivyo kwa njia hiyo walijitokeza wengine kama kina Magufuri na wengine wengina hata Sumaye alipoanza kujipambanua it was late but walong'ara waling'ara ,why not this time" Rais na PM ni watu ambao wanang'ara hata kama kuna kuzidiana kwa namna wanavyong'ara,ktk hali hiyo the only person ambaye angeliweza kujipambanua ni Waziri wa Mambo ya Nje lakini bahati mbaya ni kwamba bado hajapatia mtu wa karisma ya uhusiano wa kimataifa ambaye angeweza kutikisa mvuto wa PM au rais,aliyepo ni msomi mzuri wa diplomasia na mzoefu lakini hana mvuto unaofanana na kiti hicho,Migiro was going somewhere positively,akitaka kurejesha hali hiyo nafasi hiyo ampatie Dkt Mary Nagu,she is something better than aliyepo.
Naamini kwa dhati ya roho yangu kuwa Rais wetu ndiye ring Leader wengine wote hawa tuwaonao wanajitahidi kuisaka nyota hiyo ya Mng'aro.
Shukrani