Who is the Father of Modern Physics? Galileo au Einstein

Who is the Father of Modern Physics? Galileo au Einstein

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,564
Reaction score
7,324
Kuna mjadala unaendelea kuhusu nani ni Baba wa Fizikia ya Sasa au ya Leo "Father of Modern Physics"

Wengine wanasema Baba (Muasisi) wa Physics ya leo ni Galileo kutokana na kuitoa Dunia kwenye Imani za kale na kujenga misingi bora ya sayansi ususani kwa njia za Kitafiti, majaribio na kimahesabu. Ulikuwa ukileta ubishi yeye anakuaminisha si kwa maneno tu bali kwa vitendo vya kitafiti, mnaongia uwanjani mnaoneshana nani yuko sahihi na si porojo tu.

Huyu mwamba aliyekuwa mkali wa majaribio ya kitafiti alizaliwa mwaka 1564 na kufariki 1642, alizaliwa kipindi ambacho watu wengi waliamini nadharia ya geocentrism ya Aristotle na Ptolemy, ikisema Dunia ndicho kituo cha ulimwengu na kila kitu angani kinazunguka dunia. Nadharia hii ilikuwa imedhamiriwa na Kanisa Katoliki na ilikuwa sehemu ya mafundisho ya kidini.

Mfano zamani watu waliamini dunia ni tambarare, jamaa akaja na nadharia na akafanya kwa vitendo kujibu maswali mengi ya kisayansi na Fizikia. Na aliweza kuwakosoa kisayansi watu kama kina Aristotle, sio Aristote chawa wa Diamond. Aristotle mwanasayansi. Alibadili Imani juu ya mambo ya sayari, akatengeneza darubini na kwa mara ya kwanza akaweza kuigundua miezi inayozunguka sayari ya Jupiter.

Mwanzo wanazuoni, wachawi, watu wa imani ya asili na watu wa dini waliamini Jua na mwezi na kila kitu angani vinazunguka Dunia. Mwamba akaja na tafiti zenye maelezo kuwa Dunia na sayari nyingine ndio zinazunguka jua na pia sayari hizo zinazungukwa na Miezi.

Jamaa pia alifanya majaribio ya kurusha ndege angani, hizo ndege unazotambanazo inapiga nazo picha kuwa unasafiri. Galileo aliumuza ndonga. Alifanya vitu vingi vilivyoitoa Dunia kwenye Giza.

Miaka hiyo Sayansi na imani ya dini zilikuwa zikichanganyikana; tafiti za kisayansi mara nyingi zilitafsiriwa kwa mujibu wa Biblia au mafundisho ya kidini. Ushirikina, imani za asili, na falsafa za kale zilikuwa zimeenea, na wachunguzi wa sayansi walikuwa na hatari ya kuharibu “imani” ya watu.

Sayansi haikuwa kama tunavyoiita leo. Ilijulikana kama natural philosophy, ambapo uelewa wa dunia unachanganyika na imani, tafsiri ya falsafa na dini. Galileo alikua katika kipindi ambapo ufahamu wa kimfumo wa uchunguzi wa majaribio na hesabu haukuwa maarufu; alijenga misingi ya sayansi ya kisasa.

Galileo hakubuni darubini kwanza, lakini aliboresha lenses na kuongeza zooming capacity. Alitumia darubini yake kufanya uchunguzi wa anga, jambo ambalo lilipeleka sayansi ya astronomy (Sayansi ya anga) kwenye level mpya. Aligundua miezi minne mikubwa ya Jupiter (inayoitwa Galilean Moons): Io, Europa, Ganymede, Callisto.

Hii ilithibitisha kwamba si kila kitu angani kinazunguka Dunia. Pia Aligundua kuwa uso wa Mwezi si laini kama watu wengi walivyoamini miaka ile, bali una milima, mabonde na mapango. Alikadharika alionyesha kuwa Jua lina madoa (sunspots), ikionyesha kuwa si lenye rangi kamili moja.

Pia aliweza kujaribu kurusha vitu kutoka juu, akionyesha kuwa vitu vya uzito tofauti vinashuka kwa kasi sawa, kinyume na Aristotle. Hivyo alianzisha msingi wa kinematics, laws of motion and Mechanics.

Sheria hizi za motions/mechanics ndizo zikasababisha uboreshaji wa ugunduzi wa ndege, magari na vyombo vyote vyenye mwendo, ambapo Isaac Newton alikuja na kupita njia hizo.

Pia alithibitisha kuwa dunia na sayari nyingine zinazunguka jua, akihakikisha na kudhibitisha nadharia ya Nicolaus Copernicus, ambaye alikuwa mwanasayansi wa awali aliyesema Dunia inazunguka jua kabla hata ya ujio wa Galileo.
Screenshot_20251012_090928_ChatGPT.jpg

Lakini miaka mingi badae alikuja mwamba mmoja anayeitwa Albert Einstein aliyezaliwa mwaka 1879 na kufariki 1955 miaka 5 kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Yeye alikuwa mkali wa kutengeneza nadharia bila kufanya majaribio. Alikuwa mkali wa maandishi zaidi, anakupa nadharia za kimahesabu wewe ukienda kufanya majaribio unakutana na majibu yaleyale. Mwamba alikuja na nadharia za Relativity na kuboresha nadharia za Quantum physics ambayo hapo mwanzo wanasayansi kama kina Max Planck walikuwa wameshaumiza ndonga.

Quantum physics ndio ilimpa tuzo ya Nobel. Quantum physics kwenye Photoelectric effects aliwezesha ugunduzi wa Solar Panels, Digital Cameras, Electronic sensors, Lasers nk.

Pia alikuja na Relativity Theories ambayo iliwezesha ugunduzi zaidi wa Physics ya angani (Sayansi ya nyota, Black holes, Cosmology), pia ugunduzi wa Mionzi na vifaa vya mionzi kama MRI machine za mahospitalini, Nishati ya Nyuklia, na teknolojia ya nyuklia.

Vilevile alirahisisha ugunduzi wa Semiconductivity na electronics ambao ndio msingi wa computer na simu za leo, pia utengenezaji na ugunduzi wa GPS satellites umetokana na ujuzi wake.
Screenshot_20251012_090935_ChatGPT.jpg

Galileo alikuwa mkali wa kufanya vitendo, Einstein alikuwa mkali wa nadharia (maandishi), kalamu sana.

Je kwa maelezo haya na unayoyajua wewe nani anastahili kuitwa "Father of Modern Physics"
 
Usitumie neno waligundua au Father of physics ikiwa kazi zao hawajagundua from zero ,hao hawakugundua bali waliendeleza kwenye kile walichojifunz

Galileo hakuwa muanzilishi wa hizo inventions alijifunza kutoka kwa waislamu kwenda Ulaya

Kabla Galileo hajazaliwa Waislamu (Muslim golden age) waliandika vitabu kuhusu optics, astronomy, motion, mathematics, na experimental methods.

vilitafsiriwa kwa Kilatini vikasambaa kweny vyuo vya Ulaya hadi cha University of Padua ambako Galileo mwenyewe alisoma na kufundisha

Mifano ya vitabu ambavyo Galileo alivisoma ,Ibn al-Haytham (Alhazen) aliandika Kitabu cha Optic (Kitab al-Manazir) Kilitafsiriwa kwenda Kilatini baadae Galileo alikitumia kama msingi wa theory of light and vision.

Pia Al-Birunialiandika Vitabu vya mechanics na astronomy vinaelezea mzunguko wa dunia

Hata Einstein nadharia zake alijifunza kutoka kwa wanasyansi na ma philosopher wa Kiislamu ambao wamechangia pakubwa sayansi ya leo

lengo sio kuwadowngrade Galileo au Einstein lengo ni kurekebisha kihistoria ambayo mara nyingi inapotosha kwa kuonyesha kana kwamba maendeleo yote ya kisayansi na kifalsafa yalianza Ulaya .
 
Newton na galileo wanamchango mkubwa kwenye physics hasa classical physics ila kwa upande wa modern physics huwezi kuacha kumtaja physics hasa kwa mchango wake mkubwa kwenye Quantum mechanics na theory zake za specila na general relativity
 
Usitumie neno waligundua au Father of physics ikiwa kazi zao hawajagundua from zero ,hao hawakugundua bali waliendeleza kwenye kile walichojifunz

Galileo hakuwa muanzilishi wa hizo inventions alijifunza kutoka kwa waislamu kwenda Ulaya

Kabla Galileo hajazaliwa Waislamu (Muslim golden age) waliandika vitabu kuhusu optics, astronomy, motion, mathematics, na experimental methods.

vilitafsiriwa kwa Kilatini vikasambaa kweny vyuo vya Ulaya hadi cha University of Padua ambako Galileo mwenyewe alisoma na kufundisha

Mifano ya vitabu ambavyo Galileo alivisoma ,Ibn al-Haytham (Alhazen) aliandika Kitabu cha Optic (Kitab al-Manazir) Kilitafsiriwa kwenda Kilatini baadae Galileo alikitumia kama msingi wa theory of light and vision.

Pia Al-Birunialiandika Vitabu vya mechanics na astronomy vinaelezea mzunguko wa dunia

Hata Einstein nadharia zake alijifunza kutoka kwa wanasyansi na ma philosopher wa Kiislamu ambao wamechangia pakubwa sayansi ya leo

lengo sio kuwadowngrade Galileo au Einstein lengo ni kurekebisha kihistoria ambayo mara nyingi inapotosha kwa kuonyesha kana kwamba maendeleo yote ya kisayansi na kifalsafa yalianza Ulaya .
Chukua tende hapo Kwa mpemba nitalipa
 
Back
Top Bottom