WHO inawasikiliza sana mabeberu!

WHO inawasikiliza sana mabeberu!

Hivi jamani tuwe wakweli, Nchi ya Kenya walikuwa na Lock down au Curfew?. Kwa sababu Kenya waliweka muda wa kutotoka kuanzia saa moja jioni mpaka Saa kumi na mbili asubuhi(07:00pm-06:00am) , lakini mchana wote watu wanazagaa mitaani wakiwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
 
Hata Magu alisema chapeni kazi huku mkichukuwa tahadhari. So ni kitu kile kile tu. Lockdown bado haikuwasaidia kwa sababu maambukizi bado yalikuwa makubwa tu.

Halafu usifananishe Uingereza na Tz kuhusu mambo ya lockdown. Uchumi haufanani. Kwa alivyofanya Magufuli ni sahihi kutokana na status ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inamaana na Boris Johnson walitangaza siku tatu za maombi na kuwataka raia wake wajivukize nyungu?
 
Wakuu habari!

Moja kwa moja kwenye mada. Wakati nchi mbalimbali zikiendelea na mapambano ya hili gonjwa la covid-19, hapa kwetu Tanzania pia tunaendelea na mapambano. Juzi kati wakati Rais Magufuli anamuapisha waziri wa katiba na sheria Mh. Mwigulu Nchemba, Rais alisema mambo mengi na ndipo tulipokutana na story za mbuzi, mapapai, kware na mafenesi na kupelekea kufanyika kwa uchunguzi wa maabara ya taifa.

Kuna jambo Mh. Rais aliliongea japo watu hawakulichukulia serious sana. Hili la kuwa hivi virusi inawezekana tukaishi navyo kama ilivyo kwa virusi vingine. Alizungumzia pia uwepo wa magonjwa mbalimbali ya mlipuko ambayo yalikuwa tishio kipindi cha nyuma na kusema kuwa watu waliyazoea na kuishi nayo mpaka sasa hivi. Akatutoa hofu kuwa inawezekana hili gonjwa tukaishi nalo kama yalivyo magonjwa mengine.

Juzi kati niliona kwenye vyombo vya habari vikimnukuu waziri wa Uingereza Boris Johnson akisema maneno yaleyale aliyosema Rais Magufuli. Kuwa huu ugonjwa hauna dalili ya kuisha mapema cha msingi tuendelee kuchukuwa tahadhari na mambo mengine yaendelee. Kidogo watu wakaanza kushtuka kuwa Rais Magufuli aliongea ukweli.

Leo pia naona nukuu ya WHO kwenye media mbalimbali za habari kuhusu suala lilelile alilosema Magufuli na Boris Johnson. Ninachojiuliza hawa WHO walikuwa wanasubiri mabeberu kwanza waseme na wao waseme au? Inaonekana baada ya Boris Johnson kusema hivyo nao wakaenda kufanya kautafiti ka siku mbili na kuja kutuambia maneno yale yale yaliyosemwa kitambo na Rais Magufuli.

Tukubali tukatae hawa watu (mabeberu) wana nguvu sana na ndio maana watakachosema wao ndio kinasikilizwa na kufanyiwa uchunguzi. Sisi tuendelee na maombi na kujikinga Mungu anatuonesha nguvu zake za kuwaonesha mabeberu kuwa hatotutupa kwa vile tunamtegemea yeye.



Sent using Jamii Forums mobile app


Hao mabeberu ndiyo wanoiweka mjini hiyo WHO.So lazima waisikilize sana la sivyo hawataenda choo
 
Back
Top Bottom