Whitedent msibweteke

Ngoheranga

Member
Oct 13, 2012
28
35
Kwa miaka mingi sasa watanzania wengi wamekuwa wakitumia zaidi dawa za meno za Whitedent kuliko dawa zingine zozote, naamini hii ilitokana na Whitedent kuja na bidhaa nzuri na zenye bei nafuu ukilinganisha ilivyokuwa kwa dawa zingine kama vile Colgate, Sensodyne n.k.

Mimi, kama ilivyo kwa wengi wetu, miaka ya nyuma kidogo nilikuwa natumia zaidi Colgate wakati huo. Kama sikosei moja ya makampuni ya IPP ilifikia hatua ya kutengeneza dawa hizo hapa hapa Dsm, sina hakika kama bado wanaendelea kuzizalisha. Ujio wa Whitedent uliochagizwa zaidi na unafuu wa bei uliipaisha katika soko bidhaa zake na kama sikosei ukaifanya iongoze katika soko la dawa za meno hapa nchini.

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona mapungufu katika bidhaa za Whitedent kitu kilichopelekea andiko hili. Ipo kasoro ninayoiona mara kwa mara katika "tyubu" za dawa hizi za meno. Unapominya ili uweke dawa kwenye mswaki mara nyingine, dawa huanza hutokea kwenye 'shingo' ya tyubu kabla haijafika kwenye mdomo rasmi wa kutokea na hasa dawa inapobaki kama robo hivi ya ujazo wake. Sidhani kama hilo linanitokea mimi tu.

Inawezekana ikaonekana sio kitu kikubwa, lakini kibiashara, hata kama sasa hivi mmelishika soko la dawa hizo, sio sahihi. Ina maana wenye kiwanda hilo hamjaliona? Au mnatutengenezea bidhaa ambazo wenyewe hamzitumii? Mbona zamani hali haikuwa hivyo. Rekebisheni hiyo hali ili tuendelee kupenda vya kwetu na tujivunie bidhaa bora kutoka Tanzania.
Whitedent, msibweteke.
 
Naunga mkono hoja, hasa hiyo ya dawa kutokea shingoni. Warekebishe. Tube huwa inakatika shingoni. Mbona zamani ilikuwa haiwi hivyo?
 
Back
Top Bottom