sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 649
Ngazi zilizo wima zinateremka kuelekea chini na katika giza totoro, hewa ni nzito, ina kama moshi hivi na kuna joto katika eneo hili ambalo punde itakuwa Sudan Kusini iliyoo huru.
Kuna pingu zinaninginia kwenye mhimili wa chuma kwenye dari nyeusi. Kumbukumbu ya ukatili na mateso yaliyowahi kutokea hapa.
Kwa Sudan Kusini, ambyo tayari inajitahidi kumaliza ghasia, eneo hili linatoa onyo kali kwamba siku za usoni hazitakiwi kuwa kama zilizopita.
"Ni Taifa litakalokuwa jumuishi?" aliuliza Jok Madut Jok, Profesa wa taaluma na historia katika Chuo Kikuu cha Loyola Marymount, California, alipozungumza katika mhadhara wa karibuni.
"Au litakuwa halina msimamo kama nchi nyingine zimetumbukia-kwamba unapata uhuru , halafu unaendelea kufanya yale yale uliyoyapinga?" alisema Bw Jok, ambaye pia ni afisa mwandamizi katika
Wizara ya Utamaduni.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC Peter Martell, kuna maeneo machache katika mji mkuu wa Sudani Kusini Juba ambayo yanaibua hofu kama jengo lijulikanalo kama "White House".
Wakati wa vita ya Sudan 1983-2005 lilipata umaarufu kama eneo kuu la Kusini la kutesea na kunyongea la serikali ya Khartoum, kwa wale iliyoamini kuwa ni vikosi vya waasi.
Kuta zenye grisi na masizi pamoja na maganda ya risasi yenye kutu yalitapakaa sakafuni.
Balbu yenye mwanga hafifu ikitoa mwanga mdogo kwenye kona za giza kwenye chumba hicho.
"Nina wasiwasi kama waandishi wengine wamewahi kufika hapa," afisa usalama wa serikali alisema kwa kunongona.
"Kama waliwahi, basi hawakutoka wakiwa hai," mwenzake aliitikia.
Inakadiriwa kuwa watu 1.5 milioni walikufa katika vita, mgogoro uliotokana na imani, ukabila, udini, maliasili na mafuta.
Waasi wa Sudan Kusini walipigana dhidi ya kile walichokiita kutengwa na kujilundikia madaraka kwa serikali iliyojaa wasomi ya Kaskazini.
'Kuongezeka kwa ukatili'
Sasa wapiganaji hao wamekuwa jeshi rasmi la Kusini, ambayo itakuwa Taifa lililojitenga Julai 9, likiigawa katika mataifa mawili nchi yenye eneo kubwa kuliko yote Afrika.
Lakini jengo kama White House halibebi kumbukumbu mbaya za Sudan iliyopita iliyokuwa imejaa damu.
Watu wanasema wanatoa ujumbe wa siku zijazo. Kwamba utawala uliotumia mateso dhidi ya watu wake wenyewe katika Sudan iliyokuwa moja ni lazima iwe historia na kwa namna yoyote isibebwe katika Sudan Kusini mpya iliyojitenga.
"Eneo hilo lilikuwa ni jinamizi kwetu-ukisikia mtu amepelekwa huko, utakuwa tayari umeshaagana nao, hawakuwa wanarudi," alisema mwanafunzi wa chuo Mabil William.
Ingefaa paitwe 'Red House' kwa sababu ya damu na sio White House alisema askari wa SPLA.
Baba yake hakuonekana tena baada ya kukamatwa vitani, inaaminika kuwa alikufa huko White House
"Tulipopiga kura kwa ajili ya kujitenga, kusema kwa heri kwa Khartoum, maeneo kama hayo tunayapungia mkono wa kwa heri."
Lakini wakati matumaini ya mabadiliko ni makubwa, changamoto ni nyingi.
Chama cha Kusini cha Sudan People's Liberation Army (SPLA) hakijawa na rekodi kamili.
Kuhama kutoka chama cha waasi na kuingia kuwa jeshi la kawaida kumezusha tuhuma za mauaji na ubakaji, kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu
"Taarifa za uporaji, unyanyasaji kwa raia na hata mauaji vimesababisha kuwa na wasiwasi mkubwa" sehemu ya taarifa ya pamoja ya makundi ya Kimataifa na ya Sudan kuhusu haki za binadamu ilisema.
Taarifa hiyo ilionya juu ya "kuongezeka kwa ukatili wa serikali" Kusini, huku pesa na mamlaka vikilundikwa Juba, na usalama ukichukua sehemu kubwa ya bajeti.
Chama cha SPLA kimekuwa kikipambana na takribani vikundi vya wapiganaji vipatavyo saba kwa mwaka. UN inasema pande zote mbili zilikuwa zikilenga raia.
Zaidi ya watu 1,800 wameuawa mwaka huu Sudan Kusini na wengine 264,000 kwa mujibu wa makisio ya UN.
Serikali ya Kusini imerejea kusisitiza kuwa inafanya kazi kwa manufaa ya siku za usoni, na inasema wakati makosa tayari yameshafanyika, mabadiliko kutoka vita vya msituni hadi serikali si kitu rahisi.
"Sudan Kusini itaheshimu haki za watu wote wanaoishi katika milki yake wawe wa kutoka mchanganyiko wa makabila , utamaduni, lugha dini na asili " ilisema taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa sasa kabla ya kutangazwa uhuru ikiahidi kuzingatia tamko la Haki za msingi za Binadamu.