Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,200
Kwanza nimpongeze kakangu Dr. Mkumbo kwa jinsi alivojaribu kufafanua juu ya alivyo zito. Mi nafikiri tusiwe na conclusive statements juu ya Zitto kisa tu eti anafikiri tofauti na sisi, hatutaenda haki kwa Ndg yetu Zitto hata kidogo. Zitto ni mwanasiasa mchanga wengi wanaomfahamu toka yuko sekondari na Chuo pale mlimani ni mtu makini anayependa kusimamia anachokiamini, na mda mwingine huwa yuko tayari hata kusimama peke yake kutetea anachokiamini na hii ndio sifa kubwa ya viongozi wengi duniani ilimradi tu anachokisimamia na kukiamini kiwe na maslahi kwa waliowengi. Tumeona hivyo kwa Mwal. kipindi cha uongozi wake kuna kipindi aliotofautiana na wenzake ndani ya chama akawambia CCM sio mama yake kwa kuwa alijua anachosimamia, vivyo hivyo mapema miaka ya mwanzoni kuna hata waliotaka kumpindua kwa kufikiri tofauti na yeye. Na kwa CDM mimi nafikiri ili chama hiki imara kiwe imara we need a diverse of views and sometimes our ideas may differ as far as we think differently. Zitto asihukumiwe kwa lolote kwa sasa, personaly bado namuona Zitto kama kiongozi shujaa, makini, visionary, mzalendo, na wa mfano kwa vijana wengi na ambae atakisaidia sana chama huko mbele. Mfano mzuri ni katika kutetea rasilimali za nchi kutonufaisha wachache. Tutafute taarifa sahihi kumhukumu kiongozi huyu sio uvumi unaletwa na wasioitakia mema CDM tutakuja kujuta baadae.
Na kwako zitto huu ni wakati wa changamoto ndio wakati wa kusimama imara katika kuwatumikia watanzania, tunakuamini chapa kazi.
Kuna jamaa yangu yupo Interpol Nchini Rwanda kanieleza kuwa kuna linaloendelea baina ya Zitto Anayetaka urais na Paul Kagame na alishapata kushuhudia zitto akitinga pale Ikulu ya Rwanda mapema mwaka huu.what is behind the scene?
Achieved at: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38079-kauli-hizi-za-zitto-zinatupa-picha-gani-print.htmlZitto Zuberi Kabwe
- Nimekuwa Mbunge miaka 4 sasa. Kweli siwezi kuwa na pesa za kununua VX mbili tatu nk? Mwaka 2007 nilinunua gari ya kifahari kabisa (pamoja na msaada wa marafiki wa nje) aina ya Hummer, nayo nilihongwa na nani? Nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Afrika Mashariki kwa miezi 6 nalipwa kila siku 200,000 shs. Pia nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Madini ya Bomani kwa miezi 4 na nusu na kulipwa 350,000 kila siku. Kweli ndugu zangu nishindwe kununua VX ya 60m, tena second hand pale AfriCarriers? Mbona mnanitukana ndugu yenu? Nimesomea kiasi cha kutosha Biashara ya Kimataifa na kufanya kazi za 'consultancy' Wizara ya fedha na wizara ya Biashara na Viwanda kuandaa mkakati wa nchi katika mazungumzo ya Economic Partnership Agreements dhidi ya EU. Nimekuwa nikilipwa vizuri tu. Nimefanya kazi kwa Mwaka mmoja na Rais Kohler kuhusu mpango wa Ujerumani kuhusu Afrika. Nimefanya consultancy na EU kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Biashara ya Kimataifa....... Kweli jamani, hata kama mtu ana ajenda ya siri, siwezi kupata fedha za kununua gari ninayoipenda? Hivi sasa nina gari 5 - Prado 2 (zote sasa nimezigawa kwa Wagombea Ubunge watarajiwa wa CHADEMA mwakani, Nissan Patrol 1 ambayo inatumika Jimboni kwangu, Prado 2 moja anayotembelea Jacquiline, my partner na VX ambayo ninaitumia mimi kwa ziara ndefu za Chama. Gari zote nimeziorodhesha katika fomu za maadili na zile za kuzitoa nitazitoa baada ya kubadili umiliki.
Source: HABARI MOTOMOTO: ZITTO KABWE 'AANIKA' UTAJIRI WAKEZitto Zuberi Kabwe
Akizungumzia Utitiri wa magari ya kifahari anayodaiwa kuwa nayo anasema "Watu wanaishi maisha ya kufikirika sana, hayo magari wanayodai ninayo sina, iko hivi; mimi nina gari moja dogo aina ya Toyota Vista na nina Land Rover, Free Lander ambalo nimelichukua kwa mkopo, bei yake ni Dola 30,000, sijamaliza kulipa. Hayo mengine yanayosemwa ninayo ni ujinga tu wa watu.
Baada ya kuwa mbunge, nakumbuka April 2007 niliingiza nchini gari aina ya Hammer na nadhani nilikuwa mtu wa pili kuingiza gari hilo hapa nchini. Kaka yangu Salum anayefanya biashara ya magari ndiyo aliyeniletea na hili sikuliendesha zaidi ya wiki mbili, likanishinda. Lilikuwa la kifahari mno, nikamwambia alichukue aliuze na hela yangu anirudishie.
Nakumbuka nilikwenda nalo Dodoma nikiwa naendesha na nilikwenda na Dk. Slaa na siku moja mwenyekiti wangu Mbowe baada tu ya kuletewa tukiwa Protea Hotel iliyo karibu na Kanisa la mtakatifu Petro, alijaribu kuliendesha akaniambia ni gari zuri sana. Hili nililikataa. Mwaka 2008 nilinunua Toyota Land cruiser V8. Hili nililitumia hadi kwenye kampeni mwaka 2010 na baada ya hapo nililiuza.
Salum alipoona sina gari kwa sababu nadhani ya kujua mimi ni mbunge akaniletea tena Range Rover Vogue Sport nililitumia kidogo likanishinda kwa sababu ni la kifahari sana, sikuweza kuligharamia. Nina akaunti mbili tu moja benki ya NMB na nyingine benki ya CRDB na zote hazina fedha zaidi ya shs Mil. 15 kila moja."- Zitto Kabwe
Mwanzoni nilipoona mada hii na majibu ya baadhi ya watu hapo awali sikuona umuhimu sana wa kujibu kwani ni mada ya zamani sana, mwaka 2007. Nilisema kwa mara ya kwanza kuwa sitagombea ubunge mwaka 2010 mwezi September mwaka 2006 na kuripotiwa na gazeti la SundayNews. Nilirejea tena kauli hiyo mwezi March mwaka 2007 nikiwa Wilayani Maswa mkoani Shinyanga na kuleta mjadala mkali sana wakati huo.
Mwezi March mwaka 2008 nilihojiwa na gazeti la The EastAfrican na kusisitiza kuwa nia yangu ni kutumikia kipindi kimoja tu cha Ubunge na kupumzika kwa miaka mitano kabla sijarudi tena Bungeni...... soma hapa ...allAfrica.com: Tanzania: Zitto Kabwe - The Country's One-Man Backbench (Page 1 of 2)
Mara zote nilisema kuwa sababu kubwa ya kuamua kuwa Mbunge wa kipindi kimoja ni kurudi kusoma zaidi na kupata fursa ya kufanya kazi maana toka nimemaliza shule nimefanya kazi mwaka mmoja tu (Shirika la Friedrich Ebert Foundation) na hivyo kujiona kuwa ninakosa 'some skills' za uongozi ili kutumia kipaji changu 'to the fullest' na kutumikia nchi yangu. Hata siku moja sijawahi kutia shika nia yangu ya kutumikia Taifa. Lakini siku zote nimekataa kuwa carrier politician. Ninapenda nikimaliza kazi zangu za kisiasa niweze kuwa na uwezo wa kufundisha katika vyuo vikuu taaluma yangu nitakayobobea. Baada ya kuwa Mbunge kwa takribani miezi 9 tu (na hasa baada ya kikao cha bajeti cha mwaka 2006/2007) niliona dhahiri kuwa kwa Bunge letu hili, mabadiliko ni nadra sana. Hivyo nikasema mapema kabisa kuwa nitakuwa Mbunge wa 'term' moja. Nilisema mapema ili watu wa Kigoma Kaskazini wenye mawazo ya kutaka kugombea wajue 'incumbent' hatagombea. Nilifanya kwa nia njema kabisa. Ninadhani nina uhuru wa kuamua kutogombea kama nilivyoamua kugombea bila kusukumwa na mtu. Mimi sikuombwa kugombea ubunge. Niliamua mwenyewe…..
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.
We kupeng'e kalale hujui lugha ndo maana comments zako kwenye mada za kiingereza ni too generalNaona Zitto anatafuta mbinu ya Julias Marema maana amepoteza supporters wengi kwenye chama chake
Je hii mbinu yake ya kutaka kureview hii mikataba itamsadia?