Mizizi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,275
- 391
Selous wandugu ndio ghali kuliko kote huko! Kwanza hakuna guest house, hotel zote ni mwendo wa dola, na lazima ulipe kwa package! Petroli buku3 kwa lita, usafiri wa public ni gari Moja tu, ukitaka kwenda makao makuu ya mkoa, incase una shida ya ki utawala unahitaji utembee mwendo wa masaa kadhaa hadi ufike moro, then ndio utafute mwendo mwingine hadi Kibaha! Or uzunguke hadi kibiti, then mkuranga, then dar, ndio ufike kibaha! Cement sh elf 27 mfuko mmoja! Mvua ikinyesha ndio mnakula samaki tu, hakuna barabara itakayo pitika kuleta bidhaa huku! Mnaongelea ughali wa pesa tu, huku kwetu hakuna dala dala, kutembea kilomita 30 kwa miguu kumfuata mshkaji wako kumdai buku ni kitu cha kawaida saana hapa! Tunashangaa huko mnapiga kelele madaktari kugoma siku 2, huku hatujawahi kukaa na dr hata kwa wiki 1, wakipangiwa wanakuja na kugeuka siku hiyo hiyo! Huku kutemebea mwisho saa 1 jioni, zaidi ya hapo simba, tembo kifaru, wote halali yako! Huku tuna mito lakini kuogelea kula maisha beach tunakusikia tu kwani Ngwena(Mamba)(ukija huku usiite mamba ni mwiko) wametanda pembe zote! Jamani haya ni maisha rahisi? Au nyinyi ughali mnauangalia kwa kulipa pesa tu?