Where did Israelites came from?

hapo nilipo-bold-kama Mungu alikuwa ameshawapa nchi yao-huoni kuwa hao wapelestina ndo wanatakiwa kuondoka hapo-si kwao
 
Israeli ni taifa lililoanzishwa miaka kama yapata 4000 hivi iliyopita, wakati Abrhamu alipohamia nchi iliyotambulika hapo nyuma kama Kanaani. Historia yao kuanzia abraham hadi leo haikunyooka, kwani siku zote wamesumbuliwa na kuteswa sana na Mataifa makubwa ulimwenguni. Na kilichosababisa wawe shabaha ya walimwengu ni kutokana na unyeti wa sehemu nchi ilipo.
Israeli iko katikati ya bara la Ulaya, bara la Africa, bara Asia na bahari ya mediteranian(bahari ya kati). Kutokana na historia yake Israeli imekuwa kama bawaba inayoshikilia mlango wa amani ya ulimwengu kwa upande mmoja na vita ya ulimwengu kwa upande wa pili. Ukweli hauwezi kupingika kwamba wamekuwepo wayahudi na waarabu ambao wote kwa pamoja ni raia wa taifa la Israeli. Lakini sababu za kimaslahi zinaonekana kuligawa taifa hili katika mafungu mawili, yaani palestina na Israeli. Israeli kama taifa moja limekuwepo toka enzi zote hizo na lina bendera yake(bendera ya Daudi) inayosadikika kuwa ya kale kuliko zote tulizo nazo sasa. Na mji wake mkuu umekuwa Yerusalemu tangu mwanzo, mji uliyokuwa umejengwa na mfalme wao Daudi. Haukuwahi kugawanywa kuwa mji mkuu wa nchi mbili tofauti kama ambavyo baazi ya wakuu wa dunia wanataka iwe, akiwemo B. Obama.
Israeli imekuwepo hapo ilipo sasa miaka yote na hata kama walipelekwa utumwani kwa kulazimishwa, mara zote haikuwa ni wote waliokwenda. Na pia itakaa hapo ilipo siku zote, na hatakaa atokee yeyote katika dunia yetu tunayoishi awaondoshe hapo.
Tahadhari ni kwamba, kwa wale wanaofikiri Mungu hatawali kote ni lazima watambue kwamba anatawala Mbinguni na duniani pia. Hivyo kitabu cha biblia siyo kitabu cha falsafa kama mtizamo wa baazi ya watu. Bali pia historia tena iliyo huru na ya kweli kabisa. Na ikiwa ya kwamba hatuta takakusadiki, basi hatuta thibitika kamwe.
.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…