When Things Goes Bad to Worse....

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,236
36,261
Yaani....

Nimekosa raha, tabasamu langu limepotea...

Nilitoka na niliapa kutokulia, ila jana machozi ya kwikwi yalinitoka.

Ni sehemu ya kufatilia namna ya kupata huduma, unauliza natakiwa nifanye nini nafanya vyote halafu naambiwa kesho asubuhi uje huduma yako iko tayari.

Unafika asubuhi unaambiwa subiri, nakuwa mtii nasubiri masaa kadhaa yanapita unaambiwa endelea kusubiri utapata nakuwa mpole nasubiri.

Inafika jioni unakuwa umechoka muda wa kazi umeisha unaona kabisa ulikuwa unadanywa kama danganya toto.....

Inaumaaaa, bora wangeniambia nenda tutakwambia lini uje... hapo siku nzima ushazungushwa panda floo ya 4 chumba na 12 ukifika unaambiwa nenda floo ya 8 kisha unarudishwa chini mapokezi kisha nenda floo ya 3 halafu unaambiwa ngoja usiondoke muda wa wowote huduma yako itakuwa tayari...

Matokeo yake jua linazama wale waliokupiga danadana tangu asubuhi wanabeba mikoba yao wanakwambia eeehh bado upo...!!!?

Hapo hasira imepanda, donge limenikaba kooni nachukua kikapu changu nielekee kituo cha daladala nirudi nyumbani...

Nikashindwa kujizuia, niliangua kilio kikubwa Cheney kwikwi na hasira na jazba hadi nikakaa chini.

Wakatokea walinzi wakaninyanyua bibi polee, jikaze ukilia haisaidii sanasana hapa utajaza watu wakurekodi na kukurusha mitandaoni.

Nikanyanyuka nikajifuta kamasi na mtandio wa dera huyoo nikaondoka polepole.

Najua muda si mrefu nitatabasamu tena na kurejesha furaha yangu, huduma nimeizira maana nikirudi tena ntaudhika tuu.

Al Jumapili Njema.
 
😘

There you go!

Haya rudisha tabasamu sasa.

You are.... my fire, the one I desire...

I run out of words....

And found myself running running running to you....😍🤗🤗.

Hugs and Kisses.

And,

Lacoste is breastfeeding today... since noon up to now.

Thank you and I laab yuuu too 😘
 
Pole kwa kuchomeshwa mahindi, Ni kawaida tuu katika huu Ulimwengu wa Nchi za mwisho

Yaani ......

Niko mvumilivu sana hata ukinoambia njoo baada ya miezi mitatu ntarudi ila kaa usindoke halafu hadi jioni hamna kitu na tena mtu anakushangaa....! Hujaondoka...?!

Inaumaa.
 
Mambo ya 'tiharaei' enzi hizo za mkwer.... hapo unapata container linapigwa storage....

Unatamani ungekuwa na mashine umkorosowe mtu...

Ndio urasimu wa waTZ huo Kasinde...pole!
 
Mambo ya 'tiharaei' enzi hizo za mkwer.... hapo unapata container linapigwa storage....

Unatamani ungekuwa na mashine umkorosowe mtu...

Ndio urasimu qa TZ huo Kasinde...pole!

Asantiii shuga.

Nimemuachia Mungu.
 
Naelewa maumivu haya. Pole sana miss Kasie.

Dunia inachosha sana Mungu atusaidie jamani. Mtu anafight kihalali lakini sasa si mchezo...

Na amani ya Mungu ipitayo fahamu zote..iwahifadhi akili na mioyo yenu katika Kristo. (May the peace of God that surpasses all human understanding guard your hearts and your mind in Christ.)

#goodweekpeople#
 
Naelewa maumivu haya. Pole sana miss Kasie.

Dunia inachosha sana Mungu atusaidie jamani. Mtu anafight kihalali lakini sasa si mchezo...

Na amani ya Mungu ipitayo fahamu zote..iwahifadhi akili na mioyo yenu katika Kristo. (May the peace of God that surpasses all human understanding guard your hearts and your mind in Christ.)

#goodweekpeople#

Blessings 🙏🙏😇😇.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom