When Mwendo kasi meets mwendaPole

Zingine ni hujuma. Haiwezekani hadi leo tusielewe tu. Ni kama tulivyoua mashirika ya usafirishaji ili tununue malori yetu
 
Wakati najifunza udereva, mwalimu wangu alinifundisha kuwa dereva mzuri Ni yule anayeweza kuepusha ajali hata kwa kufidia makosa ya watumiaji wengine wa barabara, kitu hiki hawanacho kabisa baadhi ya madereva wa mwendokasi, hasa maeneo yenye taa, yeye taa ya kijani ikiwaka hata Kama wanaokatiza wapo kwenye jam analileta Tu Kama picha inavyojieleza
 
Zingine ni hujuma. Haiwezekani hadi leo tusielewe tu. Ni kama tulivyoua mashirika ya usafirishaji ili tununue malori yetu
Anayehujumu nani sasa?, angalia picha basi la mkoa linamalizia kuvuka Na mwendokasi analeta gari yake mpaka zigusane!, amesbindwaje kufunga breki Ili kuepusha ajali?
 
Hiyo sio adhabu huyo kapumzishwa, alitakiwa miezi mitatu segerea na viboko saba kuingia saba kutoka akawaonyeshe kijiweni
Hahaha adhabu ya namna hii ingepitishwa watu wangekuwa na adabu
 
Sioni point, je kama kachanganya wazazi?
 
Mkuu hahaha inakera mpaka inapitiliza......halafu choka mbaya
 
Haya mabasi yamekatiwa insurance ya aina gani? Kufikia mwisho wa mwaka barabara za mwendo kasi zitapangiwa matumizi mengine.
 
Sioni point, je kama kachanganya wazazi?

Wewe ukimuangalia huyo ni Muirani? Na wewe ndiyo wale wale mnaokana kwenu wakati Dunia nzima inawajua kama sisi ni watu weusi sasa sijui unakana ili iwe nini? Hata kama kachanganya wazazi ndiyo ajiite Muirani wkt amezaliwa na kukulia TZ? Huyo akienda Irani unafikiri watamkubali na kumuita Mshirazi?
 
Haya mabasi yamekatiwa insurance ya aina gani? Kufikia mwisho wa mwaka barabara za mwendo kasi zitapangiwa matumizi mengine.
Ninachokiona ni Mabasi yale ya Tata au Eicher kuingia barabarani ili ku replace hayo maboksi, japo hayo MA Eicher nayo Mmmmghhh
 
Kwani hizo taa za brt hazijawa synchronized na za kawaida? Ikiwaka kijan kwa brt kwa kawaida iwake nyekundu and vice versa??
 
Kwani hizo taa za brt hazijawa synchronized na za kawaida? Ikiwaka kijan kwa brt kwa kawaida iwake nyekundu and vice versa??
Mkuu anadhani madereva wetu wanaheshimu hizi alama za usalama Barabarani? Hapa ni vurugu tu
 
Mwendo kasi wanagonga makusudi.... Treni hazina breki za ghafla ila sio hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…