Mfugaji Alitembelewa Na Mwandishi Wa Habari Kwakua Hawapendi Waandishi Akaamua Kumpa Majibu Ya Kumchosha.
Mwandishi: Unawalisha Chakula Gani?
Mfugaji: Ng'ombe Yupi Mweupe Au Mwekundu?
Mwandishi: Mweupe.
Mfugaji: Namlisha Nyasi Na Viguta Vya Mahindi.
Mwandishi: Na Mwekundu.
Mfugaji: Vile Vile Namlisha Nyasi Na Viguta Vya Mahindi.
Mwandishi: Ahaa Sawa Sehemu Ya Kulala Ni Wapi?
Mfugaji: Yupi Mweupe Au Mwekundu?
Mwandishi: Mweupeee!
Mfugaji: Mweupe Bomani Kulee.
Mwandishi: Na Mwekundu?
Mfugaji: Vile Vile Ninamlaza Na Mwenzie.
Mwandishi: Hii Sehemu Yote Majumba Mengi Na Wakienda Kulisha Unafanyaje?
Mfugaji: Yupi Mweupe Au Mwekundu?
Mwandishi: Wooote (Kwa Hasira)
Mfugaji: Mweupe Ninamfunga Kamba Na Kumzungusha Malishoni Na Kumrudisha.
Mwandishi: Na Mwekundu?
Mfugaji: Ninamfunga Kamba Na Kumzungusha Kama Mwenzie.
Mwandish: Kwanini Kila Mara Nikikuuliza Huduma Za Ng'ombe Unaniuliza Mweupe Au Mwekundu Halafu Kazi Zao Wote Sawa?
Mfugaji: Kwasababu Mweupe Ni Wangu.
Mwandishi: Na Mwekundu?
Mfugaji: Ni Wangu Vile Vile.






