MTU mmoja alifariki na kwenda
jehanamu.
Kufika huko akakuta kuna jehanamu
tofautitofauti kwa kila
nchi. Akaamua kuzunguka zunguka ili
aweze kuipata jehanamu yenye maumivu kidogo zaidi .
Akaenda jehanamu ya Ujerumani .
Akamwuliza mtu aliyemkuta
mlangoni.
“Wanakufanyaje ukiingia humu?”
Akajibiwa: “Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha umeme kwa
saa moja , kisha wanakulaza kwenye
kitanda cha misumari
kwa saa moja nyingine . Kisha anakuja
shetani wa Kijerumani
anakucharaza bakora kutwa nzima . ” Mtu huyo hakuipenda jehanamu hiyo.
Akaamua kujaribu
jehanamu za Marekani, Uingereza na
nyinginezo nyingi lakini
akagundua kuwa zote zina adhabu sawa
na jehanamu ya Ujerumani .
Kisha akaifikia jehanamu ya Tanzania.
Akastaajabu kuona kuna foleni ndefu ya
watu wakisubiri
kuingia humo. Kwa mshangao
usiosemekana akauliza ; “Jamani kwani humu wanawafanyaje ?”
Akajibiwa; “Kwanza wanakuweka kwenye
kiti cha umeme kwa
saa moja , kisha wanakulaza kwenye
kitanda cha misumari
kwa saa moja nyingine . Kisha anakuja shetani wa Kitanzania
anakucharaza bakora kutwa nzima . ”
Akazidi kustaajabu . Akauliza, “Lakini
mbona kinachofanyika
humu ni sawa kabisa na kwenye
jehanamu nyingine , kwa nini hapa kuna foleni kubwa sana watu wote
wanakimbilia huku ?”
Jamaa mmoja akamshika mkono .
Akamvutia pembeni .
Akamnong ’ oneza ; “Watu wanakimbilia
huku kwa kuwa jehanamu ya Tanzania haina umeme wa
uhakika ,
unakatikakatika kila dakika kwa hiyo kiti
cha umeme hakifanyi
kazi . Halafu pia misumari ilishalipiwa
lakini wala haijaletwa na mzabuni kwa hiyo kitanda cha humu
ni raha tu kukilalia.
Na jambo lingine ni kuwa shetani wa
Kitanzania alipokuwa
duniani alikuwa mtumishi wa umma . Kwa
hiyo ameshazoea kufika ofisini na kusaini kitabu cha
mahudhurio kisha
kuondoka zake kwenda kufanya shughuli
zake binafsi