What TRA wants from you in 5 yrs

Kwanini hutaki jimbo Michelle? Bado msimamo wako ni ule ule kwamba hutaki jimbo hata 2015?

She is too smart to be a Tanzanian politician!! Unaweza kumfananisha Michelle na wakina Sophia Simba!! Michelle kaa huko huko uliko na jenga nchi kupitia JF!!!
 
Hakuna kitu kinachoniuma kama kulipa kodi...yaani kutoka ndani ya moyo huwa napata uchungu sana ninapoona manunuzi yangu yamehusisha na kodi....kwani katika maisha sijawahi kuona faida ya kodi ninayolipa katika nchi yangu....kwani kwa miaka yote niliyolipa kodi sijawahi kupata huduma yoyote ya kijamii inayonifanya nijivunie ulipaji wangu wa kodi...zaidi ya kunipa majonzi na machungu kwa kuwa kuna wapuuzi wachache wanaokula majasho yetu kiulaini kwa kukaa tu kwenye ofisi zenye viyoyozi na kuzungusha miguu kama vilema....huku wakipanga wakale au wafanye wapi shopping kwa vijisenti vyetu tulivyokamuliwa walala hoi....
Nitajivunia vipi kulipa kodi ili hali huduma za afya nalipia kwa kiwango cha kukatisha tamaa....??
Nitajivunia vipi kulipa kodi wakati hata hao tiliowapa mamlaka ya kulinda usalama wetu huku tukiwalipa kwa kodi zetu ,ndio hao hao wanaotutoa uhai wetu....huku wakitukamua rushwa kupata stahili zetu...??
Nitajivunia vipi kulipa kodi ikiwa mimi mlipa kodi ninashindia mlo mmoja alafu viongozi wangu wanatumia mamilioni ya fedha kununua mboga tu.....??
 
Shida kubwa ipo kwenye lavish spending. Kulipa kodi sio ishu sana ila tunakereka na matumizi yasiyo endelevu ya kodi zetu. Tukiwaambia wanunue magari ya be rahisi hawataki. Tukiwaambia wanunua fenicha za Keko hawataki, wanataka za China.

Wanafanya hivyo ili kutuhadaa waweke 10% zao, wewe hujasikia bei ya mapazia ya ikulu???? Hata hivyo tatizo langu kubwa mbali na hayo manunuzi ya anasa kutoka nje, lipo kwa hawa wawakilishi wetu; Kwa nini sisi tunaowakilishwa tunalipa kodi halafu wao wasilipe? Yaan mlala hoi mwenye kipato kidogo anabanwa halafu wabunge wenye vipato vikubwa wanasamehewa!
 
Tatizo kubwa la Tanzania sio vyanzo vya mapato, bali ni pamoja na utaratibu mbovu wa matumizi ya makusanyo yanayofanyika.
Pili, Serikali inapoteza pesa nyingi kutokana na wafanyabiashara wakubwa kutokulipa kodi stahiki. Yaani shehena yameli moja ya sukari ikisamehewa kodi inaikosesha serikali pesa nyingi mno!

Tatu - Magari yanayotolewa mifano - yanamilikiwa na wafanya biashara wa kati na wale wakubwa. Hivyo, tunazunguka pale pale - tatizo ni la wafanya biashara wakubwa.
 
Ni kweli kabisa Michelle wakati mwingine mipango yako mikubwa uliyokuwa nayo jimboni inakwamishwa tu kwa sababu jimbo limechukuliwa na upinzani wanakufanyia hivi miaka yote kisha wao ndio wa kwanza kukunanga huyu kafanya nini jimboni kwake katika miaka mitano/kumi iliyopita. Wakati huo huo majimboni kwao asilimia kubwa hakuna la maana lililofanyika kwa miaka mitano/kumi iliyopita. Nchi yetu bado ina safari ngumu na ndefu sana hadi kufikia maendeleo ya kweli hizi siasa za kukomoana zinaigharimu na zitaendelea kuigharimu sana nchi yetu.

Wakati mwingine huangalii tu uwezo wako binafsi BAK,unaangalia na ule wa yale ambayo unaweza kuyafanya kwa mamlaka unayoitaka na unayoweza kuwa nayo na unaangalia uliodhani wangefanya yasiyowezekana wamefanya nini kwa miaka mitano-kumi waliyopewa wajibu unaotaka kuwa nao....inakatisha tamaa sio kwangu tu hata wengine wengi.
 
Last edited by a moderator:
Je, TRA ni ya ngapi kwenye corruption index?

Wananchi tunawajibu wa kuchagua wawakilishi wanaonweza kubana serikali kwa lavish spendings.
 
Natamani tupate viongozi watakaomsaidia bade kufikia ndoto hii, ila kwa uongozi uliopo mmhhh......yaani wasinunue Mavx? Wasisafiri? Wapunguze perdiems and allowances?... Kwahiyo hata akusanye vipi, as long as kapu lina matundu, pesa haitakaa......
 
Ni kweli kabisa everlenk misamaha ya kodi kwa mwaka imefikia 1.8 Trillioni na wanaofaidika ni Mawaziri na Wabunge na pia awawajibishe wapokea rushwa ndani ya TRA ambao sasa wamekuwa ni wengi mno. Yule mama kapokea rushwsa ya 80 million lakini cha kushangaza hadi hii leo bado yuko kazini! Huyu mwizi na mpokea rushwa ilibidi afukuzwe kazi miezi mingi iliyopita.

Ni kweli BAK na wengine wamediriki kutangaza hadharani kabisa kwamba hawatatoa kodi kabisa na hawajachukuliwa hatua,leo hii wameenda kinondoni kuwafungia maduka wafanyabiashara ambao hawana machine za kietronik za TRA,hii maana yake nini sasa? Wanatulazimisha tuwe na mashine wengine hawapo hata katika category ya kuwa na hizo mashine..na bado mfumo wenyewe bado ni matatizo matupu.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakati huo huo Rais ambaye mshahara wake kwa mwaka ni karibu shilingi 400 million halipi kodi, Waziri Mkuu ambaye mshahara wake kwa mwaka ni karibu shilingi 350 halipi kodi na Wabunge ambao mishahara yao kwa mwaka ni shilingi 132 million na shilingi 75 million kiinua mgongo kila baada ya miaka mitano Wabunge zaidi ya 300 hawalipi kodi!!! Halafu Serikali hii inakuwa mstari wa mbele kupaza sauti kwamba haina pesa!!! Wakati vyanzo vya mapato kama vya hawa waheshimiwa havitozwi kodi....Only in Tanzania!

Mhhhh, hilo la Serikali kubana matumizi, labda mwakani hivi......

Vasco_da_Gama_(Livro_de_Lisuarte_de_Abreu).jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakati huo huo Rais ambaye mshahara wake kwa mwaka ni karibu shilingi 400 million halipi kodi, Waziri Mkuu ambaye mshahara wake kwa mwaka ni karibu shilingi 350 halipi kodi na Wabunge ambao mishahara yao kwa mwaka ni shilingi 132 million na shilingi 75 million kiinua mgongo kila baada ya miaka mitano Wabunge zaidi ya 300 hawalipi kodi!!! Halafu Serikali hii inakuwa mstari wa mbele kupaza sauti kwamba haina pesa!!! Wakati vyanzo vya mapato kama vya hawa waheshimiwa havitozwi kodi....Only in Tanzania!

Aggggggggrrr!!!! Inatia hasira sana ukifikiria hiyo mishahara yao, na kwanini wasitoe kodi wana tofauti gani na sisi na wao si watumishi wa uma kama sisi? Kwa mtanzania wa kawaida ukichukua vyote alivyonavyo na yeye mwenyewe bado hafikishi hivyo 400m labda umuongezee miaka mingine isiyopungua 5 ili afikishe hiyo hela.

Unakuta mtu ni mtumishi wa uma anaondoka na take home ya 350,000 katika mshahara wake ambao amekatwa kodi, kutokana na hali ngumu ya maisha kaamua kujibana kaanzisha kaduka kake hapo napo kodi anatoa, kila siku anavyoenda dukani kufanya manunuzi yake ya kawaida lazima alipie Kodi, ana kagari ka mkopo mafuta anayoweka included na kodi, bili ya maji included na kodi, umeme nao kodi, akiumwa akienda hospital bei za matibabu included na kodi, nyumba anayokaa lazima alipie kodi ya majengo,tuko hapa JF na bando zetu za 8MB ni kodi, kila kitu ni kodi kodi kodi!!! Agrrrrrr!! Yenyewe haya maviongozi yanapata hizi huduma za kijamii bure na salary la kufa mtu na bado yanatuibia,hovyooo kabisa!!!!!

Jamani tusiunge mkono katiba lao tuhakikishe katika Katiba Sheria ya kodi iwabane na wao na kipengele cha uwabikaji wa moja kwa moja kwa watumishi wasio waadilifu kinakuwepo.
 
Mimi sikatai kulipa hiyo kodi ila wakitaka maendeleo ya kweli waanzie huko juu kurekebishana, misamaha hiyo ya kodi wanayoitoa ni rasimali tosha kuliko kuwabana wauza nyanya kko, fedha za Escrow na mabilion ya uswis yakirudi yataongeza pato la taifa kwa asilimia Fulani,

Hili la misamaha bila kuwa na kiongozi mwenye nia ya dhati kabisa kuiondoa hatutaweza kujitegemea.
 
Mkuu BAK Heshima kwako; Hakuna ujinga wa dunia ninaoushuhudia kama kweye hii mamlaka ya mapato Tanzania..... juzi tu kwenye kampuni niliokuwa nafanya kazi wametoka kutoa rushwa ya milioni kumi..yani kodi ni milioni 50, imechezeshwa hadi kumi..... uliza utitiri wa ukokotoaji usio na standard yani kila mtu na lwake kutegemea ni nani anakushika mkono....after all why should i pay tax? to finance roads in Dar es Salam and especially masaki while we dont even dream of tarmac road toward our village? To finance leaders tea trips while i struggle to get Dala dala fare? their V8s? their Concubines?Their treament in USA whlie my sister is delivering a baby on the floor? School fees of their kids in abroad while my uncles are studying on the floor? money to their accounts in HSBC? are you kidding me?
 
Mkuu unaijua ile kampuni ya Clearance and Forwarding ya mwana wa mkulu... Unakupitishia Kontena lako pale Port kwa Million 30 pekee haijalishi ulitakiwa kulipa hata Billion kama kodi. Tena unaambiwa we tangulia tu huko Nanjilinji mzigo utakuja..

Kukusanya kodi ni jambo moja, ila ufanisi wa ukusanyaji wa hiyo kodi ni jambo lingine.. Kuna wazee wameganda na vyeo vyao pale TRA HQ tangia miaka ya 2000, 2001 mpaka leo na elimu ya kutosha wanayo ila hakuna promotion wala nini, watu kama hao kwanini wasipige tu?? Sababu hata system yenyewe haiwajali.. Matokeo yake ndio hao akina Bade wanatolewa walikotoka wanawekwa wanapewa ukuu hapa wengine wakiwa wamesugua tangia TRA imeanzishwa mpaka sasa wapo hapo wanaishia kwenye Ukamishna tu. Simaanishi Bade hana uwezo ila hao waliomweka hapo hawatakaa walipe kodi stahiki kwenye biashara zao mpaka atakapotoka.. This is our rotten system, kuna mkuu hapo juu kasema nguvu tuzielekeze kuwatoa tu hawa mabwana, we cant fight two battles at a time.
 
Siasa Tz ni chafu sana kuliko tunavyofikiri. CCM wamefika hatua ya kushinikiza private investors kuwanyima baadhi ya vijiji mapato ambayo ni haki yao wala sio misaada. Mwekezaji anakuwa na sera zake za benefit sharing na wananchi,sera amabayo imetumika kwa muda, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuisha vijiji vyote vilivyochagua upinzani havitakiwi kupata hizo funds. Haya ni maelekezo kutoka kwa wakuu wa wilaya wakishirikiana na madiwani wa CCM. Hili nimeshuhudia mwenyewe sijahadithiwa.

Fedha zenyewe sio nyingi lakini kuna watu wanajipanga na kuplot jinsi ya kuwaadhibu wananchi kwa sababu wamechagua upizani.

Ni kweli kabisa Michelle wakati mwingine mipango yako mikubwa uliyokuwa nayo jimboni inakwamishwa tu kwa sababu jimbo limechukuliwa na upinzani wanakufanyia hivi miaka yote kisha wao ndio wa kwanza kukunanga huyu kafanya nini jimboni kwake katika miaka mitano/kumi iliyopita. Wakati huo huo majimboni kwao asilimia kubwa hakuna la maana lililofanyika kwa miaka mitano/kumi iliyopita. Nchi yetu bado ina safari ngumu na ndefu sana hadi kufikia maendeleo ya kweli hizi siasa za kukomoana zinaigharimu na zitaendelea kuigharimu sana nchi yetu.
 
Last edited by a moderator:
Aachane na siasa, let him collect the tax, how the government spends it is not what we know he is concerned about.
...and he is not even mandated to look at government spending.
Akusanye kodi, sisi tutajua kama maCCM yanakula zote au vipi.
 
Siasa Tz ni chafu sana kuliko tunavyofikiri. CCM wamefika hatua ya kushinikiza private investors kuwanyima baadhi ya vijiji mapato ambayo ni haki yao wala sio misaada. Mwekezaji anakuwa na sera zake za benefit sharing na wananchi,sera amabayo imetumika kwa muda, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuisha vijiji vyote vilivyochagua upinzani havitakiwi kupata hizo funds. Haya ni maelekezo kutoka kwa wakuu wa wilaya wakishirikiana na madiwani wa CCM. Hili nimeshuhudia mwenyewe sijahadithiwa.

Fedha zenyewe sio nyingi lakini kuna watu wanajipanga na kuplot jinsi ya kuwaadhibu wananchi kwa sababu wamechagua upizani.
Vyama vyote...almost vyote vya kupigania UHURU ni useless hivi leo, na tukiendelea kuvilea tutaumia mbaya.
 
The "little" that TRA is collecting now is not being used or allocated effectively. The problem we are facing is not how little TRA is collecting but how effectively that tax is being used. If you are collecting TAX only to pay salaries for government officials and to fund state ceremonies what kind of authority will keep on charging more, increasing tax rates and creating more names for tax for the expense of poor citizens,who are below poverty line?
The problem with TRA is, every TRA official thinks the only reason why TRA was established is to "collect" tax. After collection, it can be used anyhow.that's why the only thing you will hear is " we have collected this much "........for them progress/development is collect more tax than previous years.

Nyerere aliwahi kusema," nchi corrupt huwakimbiza maskini ili walipe kodi na kuwaacha matajiri"
 
BAK said:
TRA is banking on electronic fiscal devices to rope more of the country’s 46 million people into the tax bracket. National identity cards will also help the taxman reach a much wider population for tax collection purposes.

Wakishavurugana na wafanyabiashara kwenye EFDs, watahamia kwa unemployed graduates, ama nimeelewa visivyo?
Kama sio wanafunzi waliokosa ajira, ni kundi gani limelengwa?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom