BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
- Thread starter
- #41
Mkuu LazyDog nadhani watakaonaswa hapa ni kundi kubwa zaidi wakiwemo hao unemployed graduates. Cha kushangaza kuna vyanzo vya mapato chungu nzima ambavyo viko wazi na vingeingizia hii Serikali mabilioni ya pesa kila mwaka lakini TRA imevifumbia macho na huku Serikali ikiendelea kuimba wimbo wake maarufu "Serikali haina pesa. Vyanzo hivyo ni kama property tax, rental income kwale ambao wanakodisha nyumba zao kwa wapangaji wanaoishi au kuzitumia kama ofisi.
Kuna Wabunge 323 ambao kila mbunge kwa mwaka anapata shilingi 132 million (11,000,000 kwa mwezi) kama mshahara tu ambazo ni sawa na shilingi 42.6 billioni kwa mwaka kwa Wabunge wote 323, kila baada ya miaka mitano kila mbunge anapata "kiinua mgongo" cha shilingi 75 million ambacho ni sawa na shilingi 24.2 billion kila baada ya miaka mitano. Rais mshahara wake ni karibu shilingi 400 million kwa mwaka na Waziri Mkuu ni karibu shilingi 350 million kwa mwaka. Tuseme hawa waheshimiwa wangekuwa wanatozwa kodi ya 30% kila mwaka basi TRA ingevuna mapato mengi sana na kupunguza huu ukwasi mkubwa unaoikabili Serikali kila mwaka. Hapa hatujui kiinua mgongo cha Rais na Waziri Mkuu kila wanapomaliza awamu ya miaka mitano, labda Waziri Mkuu anapokea kiinua mgongo hicho kama mbunge. Kwa hiyo mapato ya Wabunge kila baada ya miaka mitano ya shilingi 66.8 billioni haya yote hayatozwi kodi. Hii ni haki kweli!? Kwa kazi ipi wanayoifanya? Kama hizi pesa wanazolipwa Wabunge zingetozwa kodi kwa miaka mitano Serikali ingekusanya shilingi 20 bilioni au sawa na shilingi billion 4 kila mwaka, pesa nyingi sana hizi kwa kufanyia mambo chungu nzima ya maendeleo.
Je, huyu Commissioner General wa TRA ana ubavu wa kufuatilia vyanzo vyote hivi vya mapato ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya kodi? Tunaijua nchi yetu mara tu atakapoanza kufuatilia vyanzo hivi vya mapato atapigwa vita na mara moja kufukuzwa kazi na si ajabu ndio asipate tena kazi ndani ya Tanzania.

Wakishavurugana na wafanyabiashara kwenye EFDs, watahamia kwa unemployed graduates, ama nimeelewa visivyo?
Kama sio wanafunzi waliokosa ajira, ni kundi gani limelengwa?