Jestina
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 4,828
- 1,716
Ndugu yangu, si busara sana kuleta ndoa yako jf badala ya mbele za Mungu au kwa mchungaji wako.
Huyu mama unaemuongelea ninamfahamu sana muda,mimi ni mama mwenzie. Mara ya kwanza kumfahamu miaka iliyopita,alikuwa mwenye afya kweli na mng'ao wa matumaini kama mtu ila nilimshangaa nilivomuona juzi juzi hapo,nilimuuliza ni nini?una matatizo gani? unawaza nini. Tofauti na ulivosema hapa kuhusu God fearness,mimi nilikutana nae kanisa la kiroho misa ya pili kwenye maombi napo alikuwa ametoka ibada ya kwanza akaunga huku maombini. na siku hiyo alisema amelala analia hivo akija kwenye maombi ataondoka mwepesi. Unamwambia na kumfanyia vitu vizito sana na vingine unamlazimisha akubali.
Mambo ya kampani na kuchati na kuona wanawake wengine ndio wa maana acha! Msichana ambae uliflirt nae,ukampa zawadi unadiriki tena na kuanzisha nae biashara afu unalazimisha mwenzio akubali. je ni haki?
Kama uliwahi kuambiwa uoe kabila fulani ukaoa wa kabila lingine,ikatokea hajakubalika kihivyo na ameshaliona hilo hata akienda huko ukweni,je atakuwa huru kwenda huko? mfano " aliambiwa eti unasikiliza nini "acha kufanya masikio kama paka mara ya kwanza tu kwenda? ni neno la kawaida kumwambia mkweo?
kumwamrisha mwenzio afanye matakwa ya wifi au ndugu wakati mkeo huwezi kumfanyia hilo kiujumla ni sawa? Nyumba ni yenu na amri na maamuzi yatoke kwenu.
Mavazi mara nyingi ni yeye anastruggle akupendezee. Ni kujinyima tu. si kweli wewe ndio unashughulika. anakuonesha wewe kama kioo chake kama vile wewe unavyomuonesha akupe opinion yake ukivaa.
Kumwambia utazaa nje upelekee wazazi watoto eti umetumwa na unataka kuwaridhisha , je ni sawa? Huo uperfectionist !!
Unamwambiaje mwenzio mtoto mdogo akakae kwa bibi badala ya mama yake?
Ubalance. inakuwaje unamkataza kwenda kwenye misiba ya upande wa mke?
Hayo ni machache ,mengi nimeyastahi na kuhifadhi toka kwa mama huyo. Ila mengi yako hapo uliyoeleza umejipotray kama mtakatifu usie na mawaa.
Nimeyahifadhi sababu Jf si mahali pake.
Mmmnh mtakuwa waarabu mnajuana kwa vilemba,,mtoa mada sie wanawake ni watu wa hisia,ukicheza na hisia zetu basi ume-tuwin,tunapenda kuonewa huruma na kuonyesha tunajaliwa....embu kuanzia sasa step out of the line,jishushe..na uanze kumsifia mkeo km amependeza,mpe hela akasuke nywele hata km unajua hana shida hio, mtoe out ,mpitie kazini, mrushie vocha...msaidie kazi za nyumbani mkuu ukifanya hayo lazima utawin back her affections
Mkuu kingine ni kutafuta mzizi wa matatizo yako na kuukata, seems unaplay " blaming mind game"....kwamba matatizo yote mlio nayo km kukosa hela,kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa yameletwa na mkeo!....sio kweli, nakushauri ujishushe to her level na myaongee...usimfanye akafeel wewe ni superior yeye ni binadamu km wewe anafaa kusikilizwa na kujaliwa...
As for kuumwa nendeni hospitali for check up and treatment, inawezekana ni underlying bigger problem kama msongo wa mawazo ambao unaweza kuathiri ufanisi ktk kazi zenu na mahusiano yenu ya kindoa!
Mwisho mkuu kusiwe na nyumba ndogo unaizengea na wifi akajua!hamna jambo la kunyong'onyeza na kukoseshaa amani km hilo....kunyang'anywa tonge mdomoni...ndio maana hata tendo la ndoa linalega lega,simply ana hofu usije kumuambukiza!.... nakushauri kuanzia sasa biashara na mipango mingine ya maendeleo,usifanye na wanawake wengine,fanya nae ili kuondoa 'hofu' may be theres'something behind rather than bussiness!!