What really happened in Simba Sc Vs Stella Abidjan in 1993?

Bolizozo happened
 
Ni bora Azim angeacha Simba ishinde halafu asiwanunulie hizo Kia.
Kuliko alichokifanya.
Kama ni ukweli basi hao akina Masatu, Mwameja na Masha wanatakiwa wahojiwe na Takukuru kwa kulihujumu Taifa.
Mimi ningekuwa wao ningechukua pesa na ningecheza kwa uwezo wangu wote ili kukinda heshima ya Taifa na Michezo kwa ujumla.
 
Timu ya ALGERIA inaitwa Al Arach
 
Kuna interview alihojiwa George Masatu na Clouds Sport Extra aliongea vitu vya msingi sana.
1- anasema kabla ya mechi siku ya ijumaa walishinda kwa wataalamu kuombea dua tu
2- usiku wake walikuwa awakulala kila muda wanaambiwa wapelekwe kwa wataalamu tu.
Sasa kwa maandalizo hayo kweli ushindi unaweza kupatikana, kama tungepata cd ya interview hiyi ndio tungeelewa kilichoisababishia Simba kufungwa.
NB. Iliundwa kamati ya kitaifa kuratibu sherehe za ubingwa wa Simba kabla ata mechi kuchezwa, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walikuwa ni wapenzi wa Yanga sasa unategemea nini?
 
KOCHA MSAIDIZI NI ETTIEN ESHETE MU ETHIOPIA SIYO AFFIF
 
HII GAME ILINIFANYA NIWE KAMA JPM ALIVOFANYA SIKU ILE JUMAMOSI....NINABAKI KUWA MNYAMA ILA SIYO MPENDA UNAZI KATIK UBOVU WA TIMU....

NDIO MAANA SIMBA WAKIKOSEA NINANYOOSHA MANENO TENA MAKALI NA KAMA FAIR GAME NINAIKUBALI KEJELI AMA USHINDI KWA FURAHA.

SIMBA 1993 FAINALI TULIKUWA NA GIFTED PLAYERS ILA SIYO PROFESSIONAL PLAYERS....WALIFIKIA PALE KWA SABABU WACHEZAJI WETU WALIKUWA NA VIPAJI NA MORALI YA MASHINDANO ...

FAINALI TULIKWAMA KWA SABABU MORALI ILISHUKA SANA KWA WACHEZAJI WETU...WALIINGIA UWANJANI WAKIWA DOWN KINYUME KABISA NA GAME YA KWANZA ABIDJAN

AIDHA AZIM DEWJI NA UONGOZI WALI DISTRACT MORALI YA WACHEZAJI AMA HUJUMA TOKA NJE KUPITIA KAMATI YA USHINDI YA SSC.

SABABU YA PILI NI BENCHI LA UFUNDI LETU LILIBEBWA NA HAMASA YA WACHEZAJI ZAIDI KULIKO TACTICS ZA WAALIMU
 
simba hawakuwa na gifted players bali mwanzoni walikutana na timu mbovu kutoka msumbiji na angola kabla ya kukutana na kisiki kutoka ivory coast stella na bolizozo akawaua mchana kweupe. Kikosi hicho unachokiita cha gifted players muda mfupi baadae kiliipigwa goli 2 bila na yanga iliyokuwa na wachezaji wa kawaida akiwemo mchezaji chipukizi James Tungaraza aliyemtoboa mwameja tundu 2 hata akabatizwa jina la bolizozo wa tz
 
Azim Dewji aliuza mechi ili asiwalipe wachezaji zile KIA alizowaahidi

Uongo nilikuwepo hapo uwanjani na Azim alilia kichizi nusu azimie ( ama wataka kusema yalikuwa machozi ya mamba). Mimi pia nilishiriki kuimba " Uzalendo umenishinda ..." Sababu ya mdomo wa wanasimba siku hizo. Mpaka msafara wa kombe litakapopita ulitangazwa kabla ya mechi na Kanali Swedi ( ama jina kama hilo), nafikiri by then alikuwa kiongozi wa FAT ama BMT, Ama kweli "usianze kutandika kitanda kabla mwali hajafika hata kama umeshatoa mahali", kweli waliumbuka.

Mimi nililipiwa kiingilio na mnazi mmoja wa simba (by then bado mwanafunzi) na maneno ya kejeli kibao eti "twende ukaone leo TUNAOA 😎", kufika uwanja WAKAOLEWA wao, jamaa alipotea mtaani wiki tatu.😀😀😀😀 Nasikia alikuwa anaingia kwake usiku wa manane na kuondoa alfajiri kabla jogoo hajawika, watu walikosa AMANI sana siku hizo. 😛😛
 
Hakuna ukweli bana mbumbumbu wanamsingizia Dewj
 
Mwameja alizoea kutobolewa hata Idd Moshi alimtoboa mara mbili na hata Kalimangonga Ongala hakumuacha salama.
 
Conspiracy theories. Simba was simply well beaten.
 
Hivi unamfahamu Bolizozo we jamaa kweli ?
 
Stella wanasema baada ya mechi ya kwanza walikaa na makocha tofauti nakuisoma simba, wakati makocha wetu walikuwa wakiwapa wachezaji mazoezi magumu bila kuangalia mapungufu ya mechi ya kwanza pia kuna wachezaji hawakuchezeshwa mechi ya kwanza ili waje wacheze mechi ya pili wakisahahu kuwa mechi zote zilikuwa muhimu
Kiukweli benchi letu lilikuwa na mapungufu ni uwezo binafsi wa wachezaji ndio ulioifikisha simba fainali walioangalia mechi ya simba Angola watakwambia
 
Ki ukweli mechi ile simba walizidiwa ki uwezo, ki uchawi kizengwe na ki mkakati. Stella abijan waliigawanya timu ya mara2, kundi la wachezaji wa kwanza kilikuwa ni kikosi b lkilitua dar wiki1 kabla ya mchezo, simba wakawa wanakiloga usiku na mchana, kundi la2 yaani kikosi cha kwanza kiliweka kambi nairobi na kilivuka border na kufika dar j5 na kilifichwa ubalozin adi ijumaa jioni ndiyo wakafanya mazoezi mepesi uwanya wa Tanganyika packers, kwenye hicho kikosi kulikuwa na wachezaji3 wa kukodiwa viungo2 na beki1ambao waliwadhibit wachezaji wa simba vilivyo, siku3 baada ya mechi simba waliwakatia rufaa ambayo caf iliitupa kwa vigezo kadhaa na mtonyo huu simba walipewa na mwandishi wa habari wa stella abijan.......... ni story ndefu kidogo, binafsi nilibahati kutoka
 
Ilipangwa hadi route ya kupitisha Kombe "lao".
 
Tukapigwa Goli la kwanza Uwanja Ukawa kimyaaaaa Mara likaingia la pili Mchomo uliopigwa umbali wa mita 18 hapo ndipo Kelele za Mashabiki wa Yanga '...Uzalendo umetushinda...' Ndio zikaanza

i
Wewe Hatukusema UZALEENDO UMETUSHINDA....... Tuliimba, Tumekosa uzalendo tumekosa uzalendo
Binafsi nilifurahi sana, Mechi ambayo sitaisahau ni Ile ya Simba Na Atletico sports Aviacao ya Angola

Ilikuwa na wachezaji kama Kanka Wemba, Abilio Amanali, Gito, Bravo, Lolo, libenge, Yanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…