What is wrong with our currency?

What is wrong with our currency?

Kwa uelewa wangu thamani ya fedha ya nchi hutegemea zaidi 'global demand na supply'. Lakini pia sera za nchi ambazo hutolewa na benki kuu husaidia kuweka thamani ya currency.

Somalia wakati wa vita na machafuko pesa yao ilishuka thamani mpaka zaidi ya SOS 35,000 kwa 1 USD.

Baada ya amani ya Somalia kuimarika na uwekezaji kuanza kufanyika, thamani imepanda sana.

Pia uhitaji wa currency (demand) ambayo hupelekea thamani ya currency Somalia inachangiwa kwa kiasi kikubwa na pesa wanazotuma wasomali waliopo nchi mbali mbali duniani (somali diasporans) ambao kwa mwaka inakadiriwa hutuma cash ya zaidi ya USD 2bn. Kwa uchumi wa Somalia(GDP) kiasi hiki ni kikubwa sana kufikia hata 23% ya GDP kwahivyo lazima kifanye thamani ya currency iwe kubwa.

Kwahiyo tofauti na Tanzania, fedha za kigeni sio nyingi na hivyo dwmand ya TZS ipo chini.

Inakadiriwa wasomali zaidi ya 1mn wapo nchi mbali mbali ulaya na Amerika ambao hutuma remittance nchini mwao ambazo zinategemewa na zaidi ya nusu ya wanasomalia kuendeaha maisha yao.
Screenshot_20210203-132221_Chrome.jpg
 
Wataalamu wa masuala ya uchumi mtujuze tafadhali...

Nini kinaendelea kwenye hili la kushangaza?

USD 1 = SOMALI SHILLINGS 530/-
USD 1 = TANZANIAN SHILLINGS 2300.

Nini kimetokea hapa?
Chukulia kwa mfano; Uganda wananunua bidhaa zao kwa bei nzuri kuliko sisi, kwa sababu hela yao ni ndogo kuliko yetu. Pesa kidogo ya uganda inanunua mkate ambao unanunuliwa na pesa kubwa ya Tanzania. Ukilinganisha kwa kutumia dola, unakuta mganda ametumia dola kidogo kununua mkate, wakati mtanzania ametumia dola nyingi kiasi kumzidi mganda, kwa kununua mkate ule ule. Vile vile wakenya hela yao ni kubwa kuliko yetu, nao vile vile ukiwalinganisha na sisi in terms of dollars, wana maisha magumu kuliko sisi. Niliwahi kusafiri kwenda nje ya nchi wakati fulani kabla nchi hiyo haijaanza kutumia Euro, niliishi maisha kama niko Paradiso. Nikaja tena nikajichnaganya sasa nikarudi tena wakati tayari wameshaanza kutumia Euro, nilichoka. Hela yao ilikuwa ndogo kuliko Euro, na kile ambacho kipindi hawajnaaza kutumia Euro tulikuwa tunakinunua tuseme 50 ya hela yao, nilikuta kitu hicho hicho kimebadilika na kinanunulia Euro 50. Nilichoka
 
Back
Top Bottom