Hata mimi nadhani hivyo, lakini ndio ktk akili ya kufikirika!He Just Can't Mkuu
Hata mimi nadhani hivyo, lakini ndio ktk akili ya kufikirika!
Hivi kweli hakuna kabisa tumaini yaani He just can't -hawezi?
Je, viongozi wezee (waasisi) waliostaafu hawawezi pia! na kwa sababu gani hasa - FEAR?..
He Just Can't Mkuu
Wakuu zangu najaribu kutazama possibilities hapa kwa akili ya kufikirika!..
Mathlan Dr.Slaa akipata mgombea mwenza na mgomea Urais wa Zanzibar kuwa Salim A. Salim (ambaye aoondoke CCM) itakuwa vipi?
Nimefikiria hili kwa sababu siwezi kuficha - I still have faith in this guy kwamba ni mwana Mapinduzi na anaweza kuondoka CCM kujiunga na ukombozi huu kwa sababu he has nothing to loose!
Salim Ahmed Salim is not all he is trumped up to be. And I can go toe to toe on that with anybody who says otherwise.
He may be a little better than Mr. Zero bin Sumaye, but that does not mean much.
Hakika nawe umezungumza yaliyokuwa akilini mwangu kabla sijaiweka mada hii. Nimejaribu sana kufikiria mtu ambaye ataweza kumsaidia sana Dr.Slaa katika nafasi ambazo anapwaya uzoefu kiutawala na mtu huyo atokee visiwani au mwenye asili ya huko, ndipo jina la Salim linapokuja. Hakika sipendi kabisa mfumo uliopo wa kuchagua viongozi wa juu kwa kutazama wanatoka wapi ikiwa kweli tunatambua na kukubali Muungano tulokuwa nao. Huu n mfumo huu unaashiria zaidi uroho wa madaraka zaidi wa uwakilishi wa katiba kwani dhahiri inaoynyesha hatuna imani na katiba au tunaamini maslahi yatalindwa ikiwa na tuna mtu kiti cha juu. Dhana hii imehindikana toka mwanzo na hakika sii Jumbe, Mwinyi wala Shein wameweza kutetea au kuwakilisha upande mmoja wa Jamhuri zaidi ya wabunge wa pande hizi mbili.
Hata hivyo tupo ktk Taifa la Wagagagigikoko, watu wanaotazama vitu kwa rangi zake hivyo inatulazimu nasi kutazama ubora wa viongozi kwa vigezo vyao. Mimi siamini kabisa kwamba Salim hawezi kutoka CCM kwani kuna hotuba zilizopita amenipa moyo wa kufikiria yule Salim wa Umma party kaibuka tena. Na sidhani kama Salim ni mwoga na wala hana historia hiyo hasa ukimtazama enzi zake za UN alipowakalia kooni Marekani na UK kuhusiana na South Afrika. He had fought for Freedom and Justice all his youth na huu ndio wakati wake baada ya kutupiwa matope mwaka 2005. kama alivyosema Bulesi. Hakuwa na sababu ya kutoka wakati ule ule pasipo kuwashtua na wakaanza kumshughulikia mapema ila akiondoka leo inaweka akili zaidi...
Waswahili wanasema Unaweza mtoa mtu shamba lakini huwezi kuuondoa Ushamba kwa mtu huyo!
That kind of poaching Chadema wakiiweza ndo itasaidia. Asikudanganye mtu, chaguzi nyingi za Afrika watu huchagua watu, si vyama wala sera. Ukiwaambia watanzania kuwa sera zako ni center right, au ni left, n.k. hata hueleweki. Watu ambao wana records au wenye uwezo wa kujenga hoja zikasimama ndo wanaochagulika. Pengine Salim may not be appropriate kwa sababu ya kufanya kazi sana ndani ya machinery ya CCM. He is more like them, na anaweza asiwe sauti ya mabadiliko tunayotaka. Ni mtazamo tu...
Huyu Hamadi aliye kuwa msemaji wa kambi ya upinzani bungeni aweza faa na kufanya vyema, ni mzuri wa kujenga hoja, na hajaharibiwa na mfumo wa kifisadi!
Salim, yes is good, but kwa umri wake si rahisi kuingia katika mpambano kama huu!
Kwamba chaguzi nyingi za Afrika watu wanachagua mtu sio sera ni kweli lakini kumbuka kuwa chaguzi za Tanzania sio sawa na chaguzi za Afrika, Tanzania watu wanachagua kutokana na chama...
Mkuu I beg to differ. Tanzania kama nchi zingine za Afrika ina chagua mtu siyo chama. Sema CCM wanajua hilo na wana build personalities ndani ya chama ndiyo maana kuna muonekano kuwa watu wana chagua chama. Angalia uchaguzi wa 2005....watu walichagua chama au watu walimchagua Kikwete? It's all about personality building and propaganda mkuu nashauri uchunguze hilo.