What if kuna 'Conspiacy' dhidi ya Rais wetu na dhidi ya Uchumi wetu?

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,470
2,864
Nimepitia vyanzo mbalimbali ili kupata tafsiri rahisi ya conspirancy; inaelezwa kuwa ni njama au mpango wa siri unaofanywa na kikundi cha watu kufanya jambo lililo kinyume cha sheria au jambo lenye kuleta madhara.

Wasomi wengine wamekwenda mbali kwa kuja na tafsiri ya njama inaweza kuwa ukimya ambao ni makubaliano ya kukaa kimya (kupotezea) jambo ili liendelee kuwa siri. Siri inawafanya wachache wanafaidi huku wengi wakiwa wanabung’aa.

Naomba kutamka kuwa bila shaka au inawezekana kukawa na njama dhidi ya Rais na Watanzania ili tu tuendelee kuona wengi wakibaki katika umasikini kwa kutumia nadharia za wachumi wengi ambazo context yake haiku relevant kwetu Watanzanua. Bila shaka wakawepo wachumi wachache ambao hawakubaliani na economic models zinazoendelea kutekelezeka nchini. Kutokubaliana haina maana ni kupinga yanayofanyika, hapana. Yanayofanyika ni sawa yaendelee, ila iko haja na maengine yanayogusa watu yawe inclusive kama model ya Marshal iliyofanyika Ulaya, Ukiriki na Uturuki.

Bahati nzuri kwa wale wanaotoa economic model ambazo Serikali yetu inazitumia, zaweza kuwa zinakubalika na World Bank na IMF ila msingi wake ni kufanya mambo ambayo hayana mguso wa moja kwa moja wa kukwamua uchumi wa watu unaokukuza maendeleo ya watu ambao wao hasa ndiyo walipa kodi kupitia manunuzi ya bidhaa, huduma, kulipia tozo na malipo mbalimbali.

Nitoe mfano wa kazi kubwa za serikali nyingi hasa Afrika na latin America ambazo zimekuwa zikifanya miradi mikubwa ya miundombinu, umeme, afya, shule, maji… halafu “wanawapotezea” wakulima na wafanyakazi kwa lugha kuwa, ni jukumu lao kujiletea maendeleo; na kuwa serikali haiwezi kukuwekea mifumo ya kupata project financing kukuza kilimo, ufugaji au biashara inayoweza kusisimua ukuaji wa kiuchumi.

Ifahamike watu hao wanakosea na wanapotosha kwa kujua au kwa kutokujua kupitia nadharia za kiuchumi wanazotia. Mathalani, Ethiopia ni nchi ambao mifumo yake ya barabara, bandari, umeme na mashirika ya ndege yanafanya vyema kuliko hapa kwetu. GDP ya Ethiopia ni kubwa kuliko ya hapa kwetu. Japo hali ya maisha na mzunguko wa fedha kwa watu wa kawaida uko chini kuliko hapa kwetu na hali ilivyo hakuna dalili za hao watu wa chini kutoka. No wonder, mara kadhaa wanakimbia nchini kwao kujaribu maisha nje ya nchi yao. Hii sio afya hata kidogo kwenye jamii au Taifa.

Afrika Kusini nao wana miundombinu bora kabisa kama vile barabara, reli, mashirika ya ndege, migodi kutema hela wao wako njema sana kuliko Tanzania. Na GDP yao ni kubwa kuliko nchi kama Ureno iliyo dunia ya kwanza Ulaya. Japo, watu weusi wengi ni masikini kwelikweli na kwa hali inavyoendelea, kile kinachoitwa “kujiletea maendeleo” wao wenyewe haiku applicable. “Bondeni” wanawa-prove wrong Benki ya Dunia na IMF kwa model ya nini wachumi wanatuaminisha hapa kwetu pia.

Naomba ku-declare interest, toka Mwalimu Nyerere atoke, serikali zote hazijaja na mpango mkakati wa kukuza uchumi wa Watanzania wanahusika na KILIMO, UVUVI & MIFUGO. Uchumi ambao unazalisha malighafi na baadae bidhaa kwa tija na ubora kwa soko la ndani na nje ya Tanzania.

Kwa sababu, hesabu rahisi inanipa kubandika hapa, kama Watanzania 10 milioni tu, wakiwa na uwezo wa kutumia laki 5 kila mwezi katika matumizi yao ya huduma na bidhaa. Tafsiri rahisi ni kuwa kodi ambayo ingekuwa inakusanywa na serikali kwa manunuzi hayo ni takribani trilioni 10 kwa mwaka. Hawa watu wakiwa kwenye mifuko ya pensheni na bima ya afya iwe ni NHIF na zinginezo, mzunguko wa fedha katika mifumo rasmi ungekuwa mkubwa sana tu. Kwa bajeti ya Tril 32, ina maana matumizi ya kawaida ya wananchi kununua huduma na bidhaa yangekuwa yasha-offset theluthi (1/3) ya bajeti ya 2019/2020.

Ukienda Ulaya na Marekani ambao wao ndiyo wadau wakubwa wa World bank, serikali zao zinatoa ruzuku ya fedha kwa wakulima na wafugaji. Lengo ni kupata uhakika wa malighafi toka kwa wakulima ziende viwandani. Viwanda vina-process products kwa soko la ndani na nje. Viwanda vina wafanyakazi ambao wanalipwa mishahara na mishahara inakatwa kodi. Viwanda vinalipa corporate tax. Viwanda vinanunua huduma za umeme, maji, huduma za ubora “TBS za kwao”. Bila kilimo endelevu ambacho kiko Ulaya na South Africa pia , hakuna uhakika wa maziwa, nyama, ice cream, nguo za kuvaa iwe na raia au uniform wanafunzi na wanajeshi. Viatu na mikanda. Vyote hivi ni mazao ya kilimo.

Kwetu hapa, serikali inajivua jukumu la kuwa sehemu ya uzalishaji in the name of, serikali kazi yake si kumwezesha mkulima. Kilimo kinabaki kuwa cha kujikimu, na umasikini unapungua kwa kasi ndogo sana.

Kwanini South Africa wakulima wazungu ni matajiri na Zimbabwe pia kulikiwa na utajiri mkuwa kwa wakulima Wazungu. Kwanini bongo, wakulima wengi wamechoka na hawakopesheki kabisa. Kuna wakati baadhi ya wanasiasa uchwara wanazuga, wananchi wakipata hati za viwanja au mashamba yakisajiliwa wanaweza kukopesheka na mabenki. Wakati inafahamika sera ya mabenki hayakopeshi biashara zinazo-anza. Hawataki kutoa hela ili wachukue shamba au kiwanja kama dhamana,wao wanatoa hela based on cashflow ya biashara iliyopo.

Njama (conspiracy) iko wapi. Wasomi wetu wanaomshauri Rais kwenye sera za uchumi, “labda” hawana nia ya kuwatoa Watanzania. Na huenda furaha yao ni kuona mabarabara ya lami, viwanja vya ndege, SGR ili Rais atumie kama model ya nini kafanya kwa ajili ya Tanzania ila nyie Watanzania “komaeni kwa kupambana na hali zenu”.

Nataka kuwa wazi kuwa Rais anaweza kuwa misinformed na watu ambao aidha ni Watanzania wenzetu wana njama dhidi ya wananchi wa kawaida au wamelishwa yamini na “benki ya dunia” kumfunga mkuu wa kaya kamba kwa kumpa model ambayo haitajenga na kukuza uchumi wa Watanzania kwa haraka.

Naomba Rais wetu akumbushwe effects za Jim Crow laws zisitufanye tuishi maisha ya "separate but equal” na “we have eaqual opportunity kujenga Tanzania ya viwanda but we have no equal access” ya kuifanya njozi hiyo iwe realized.

Ombi langu kwa wasaidizi wa Rais, mpeni taarifa sahihi za namna ya kukuza uchumi wa wakulima na wafugaji wka kuwasaidia wapate training/consultancy, technology na machinery ili kukuza uzalishaji ya kuchakata mazao ya kilimo kwa soko la ndani na nje ya Tanzania.

Pengine tujiulize maswali ya msingi. Kwa soko la ndani ya Tanzania na Afrika Masharuki la Uniform za wanafunzi, wanajeshi zinatoka wapi? China au India. Kwanini tunapeleke hela nje wakati ingebaki hapa?

Soko la viatu na mikanda ya wanafunzi na wanajeshi inatoka wapi? Ngozi zipo kama raw, je machine za kutoa finished products ni rocket science ambao sisi hatuwezi kuwa nayo?

Manunuzi BVR za polisi, Uhamiaji, NIDA na TRA tumenunua (fedha zetu zimekuza private sector ya wazungu) na kupanua tax base ya nchi za wazungu

Dreamliner, Bombadier na Airbus (fedha zetu zimetoka nje kukuza private sector Canada na US), tumetengeneza ajira na tumepanuaa tax base ya wazungu.

Tunajenga reli na barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Procurement inafanyika nje kwa vyuma, wakandarasi wakubwa sio wakwetu. Fedha zetu zinakwenda nje kwa private sector ya Wachina na consultancy ya makampuni ya Wachina.

Tumenunua mitambo ya passport za kusafiri na visa toka Ireland. Mfumo huo wa kielectronic umepeleka hela za Watanzania kukuza ajira ya Private sector ya wazungu na kukuza ajira kwao.

Tunakwenda kujenga umeme wa stiglers Gauge… katika manunuzi, vifaa vingapi (nondo na vyuma) vinatengenezwa na viwanda vyetu. Bila shaka tukawa tuna-import

Kuna haja serikali kuwaa sehemu na kushiriki kujienga private sector ili kukuza uzalishaji wa bidhaa na huduma; hii itatoa ajira, itaongeza/itapanua tax base na kuleta neema Tanzania.

Tuna wajibu wa kizalendo wa kuwaomba wasaidizi wa Rais, wakati tunajenga SGR, barabara, viwanja vya ndege, tukinunua ndege; basi tunaomba serikali ifanya kazi na Watanzania kwa kuwasaidia hata kwa guarantee katika kuchakata pamba na kuwa na final product ya kitambaa. Tuwe na machinery za kuchakata korosho ili tuuze quality and standardized korosho inayokwenda kulika sokoni. Sio korosho ghafi. Ni wakati wa kuwa na liquid milk, powdery milk kwa ajili yetu na watoto wetu.

Haya yakifanyika, mkulima atatengeneza ajira humu ndani. Tax base itaongezeka. Hii ni competitive advantage ya kwetu. Kwa wenzetu wanauza technology na machinery, sie tukabe kwenye kufanya processing.

Ni vema kukaa chini na mzee wa magogoni kumpa ukweli wa haya pia. Ila tukiendelea na kile kilichotoka kwa wachumi ambao vitabu vyao walivyosoma na economc model zao zina hisani wa benki ya dunia, basi Rais wetu atajenga Reli, ataweka mifumo ya maji, umeme na barabara. Then, itakuja tokea siku Watanzania wengi watakuwa Watazamaji tu kama ilivyo South Africa.

Tusifikie huko pa South Africa na Zimbabwe ambako Rais Mugabe alikuja kufanya mageuzi akiwa kachelewa. I advise to make certain economic development is being inclusive by ensuring local Tanzania are part of the growth and development processes.

The rate of change of momentum is directly proportional to the force applied. The momentum change in economic development which is inclusive; Tanzanians being part in the value chain is inevitable.

Tofauti zetu zilenge kuijenga Tanzania na kuwajenga Watanzania kwa kuona wanakuwa. Isifikie tukarejea kule kwa zamani kwa vijana kuzamia meli na kukwea pipa kwenda kujaribu maisha bondeni au “mamtoni”. Tushirikiane tujenge mfumo endelevu na jumuishi hapa kwetu, asali na maziwa ya Canan yetu ni tamu na inawezekana tukafaidi kwa pamoja huku kukiwa na ongezeko kubwa la walipa kodi na makusanyo ya serikali kuongezeka.

Tafsiri ya sasa ya maendeleo kwa vipimo vya GDP ni conspirancy yenye kuleta madhara kwa Watanzania huko mbeleni. Ni vema kuing’amua na kufanya tofauti. Tukishirikiana, kuna right economic models za kufanyia kazi, zinazokidhi mahitaji ya kiuchumi kwa Watanzania. Huu ni uzalendo wa hali ya juu kwa kulipenda taifa kwa kuwafanya Watanzania wahusike na kujenga uchumi pia kwa teknolojia na mitambo kwa kukuza tija na ufanisi.
 
Huu ni utumbo ulioandika hapa eti njama. Jiwe alidhani ni raisi kuendesha nchi akidhani akiwa mkali mambo yataenda akasahau ukali haufui dafu kwa hela zilizo mfukoni kwa wanainchi. Huwezi kuwaambia wenye hela zao wapi waziwekeze au wapi wazitumia maadam huwafundishi kutafuta hela.

Yeye mwache aishi kwa hela za kodi ambazo hajui sisi wanainchi tunaumiaje ili yeye azitafune tyuu. Sasa sisi wanainchi ndiyo twampiga kisawasawa. Na kumpiga Jiwe ni kumpiga mfukoni kwenye uchumi ndo atashika adabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni utumbo ulioandika hapa eti njama. Jiwe alidhani ni raisi kuendesha nchi akidhani akiwa mkali mambo yataenda akasahau ukali haufui dafu kwa hela zilizo mfukoni kwa wanainchi. Huwezi kuwaambia wenye hela zao wapi waziwekeze au wapi wazitumia maadam huwafundishi kutafuta hela.

Yeye mwache aishi kwa hela za kodi ambazo hajui sisi wanainchi tunaumiaje ili yeye azitafune tyuu. Sasa sisi wanainchi ndiyo twampiga kisawasawa. Na kumpiga Jiwe ni kumpiga mfukoni kwenye uchumi ndo atashika adabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida niionayo mimi nisisi watanzania tunamchagua mmoja wa mtanzania mwenzetu kisha tunamkabizi akilizetu atusaidie kufikiri kwaniaba yetu hapahakuna cha profesa .dr. au injinea.wote tunaenda kulala. Yeye atufanyie kilakitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Conspiracy kwa Jiwe ni akili yake mwenyewe ,mawazo yake ya hovyo, maamuzi yake ya hovyo ,maagizo yake ya hovyo , uteuzi wake wa hovyo, matumizi yake ya pesa za Serikali ya hovyo, uongozi wa hovyo ,vipaumbele vya hovyo ,msitafute mchawi mchawi ni yeye mwenyewe.
 
Wanakwambia urasimishe ardhi ili ukopeshwe, hivi kweli uende na hati yako benki uwaambie 'nikopesheni nataka kuanzisha biashara ya juisi ya miwa' wakupe.

Sanasana utajikuta wewe ndio umejiingiza kwenye kulipa kodi ya ardhi.
 
Ngoja nikuangalizie muhindi wa kuchoma hapa, ule unywe na maji labda hasira zitapungua. Lakini alishasema hashauriki, kama anafanyiwa hujuma au ndo uhalisia anajua yeye aliyeikuru

Barafu la moto
 
Nasikia (sina uhakika)kuna wakati Rais wetu mmoja mstaafu alipokua nje ya nchi kwa ziara yake ya kikazi aliwahi kuulizwa ni kwa nini nchi yake ni maskini, alijibu ya kwamba hata yeye hajui ni kwa nini ni maskini!

Kwa mtanzania yeyote yule mwenye akili timamu atajiuliza tunapokosea ni wapi! Maana tuna kila aina ya utajiri ndani ya nchi yetu; kuanzia madini ya kila aina, mbuga za wanyama, mlima mrefu kuliko yote Africa, nguvu kazi, mito, mabwawa na maziwa makubwa, mabonde mengi yenye rutuba, ardhi ya kutosha, gesi asilia, chuma na makaa ya mawe,bahari ya Hindi, tumezungukwa na Land locked countries, nk!

Nadhani kuna kitu hakipo sawa, iwe kwa sisi watanzania na hata kwa viongozi wetu. Tukubali tu kukosolewa na pia kujirekebisha.
 
Shida niionayo mimi nisisi watanzania tunamchagua mmoja wa mtanzania mwenzetu kisha tunamkabizi akilizetu atusaidie kufikiri kwaniaba yetu hapahakuna cha profesa .dr. au injinea.wote tunaenda kulala. Yeye atufanyie kilakitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikatiba, Rais ni mtumishi wa wapiga kura. Iko haja tukafanya kila tuwezalo kwa kutumia known channels kumpa/kutoa development projects zanazo-supplement nini ni chema kukuza uchumi. Bila shaka ata-buy in.
Kuna mangapi ambayo wapinzani waliyasema kwa miaka mingi kwa sasa anayafanyia kazi?

Cha msingi ni kuwa na lugha ya staha na heshima ili kile tunachodhani kuna manufaa atuskize ili tuone utekelezaji ukifanyika.
 
Thread bora ya mwaka hii... Naipa 5*

Hii serikali haitaki private sector, serikali ni kama vile ilisha jitoa kufanya kazi na private sector.

Maamuzi mengine tunawalaumu washauri wa rais bure, hivi kuna mchumi aliye mshauri rais serikali inunue korosho kutoka kwa wananchi?

Serikali ilishindwa nini kukaa mezani na private sector kuangalia ni namna gani ya kuongeza dhamani ya ununuzi wa zao la korosho kutoka kwa wananchi.
 
Huu ni utumbo ulioandika hapa eti njama. Jiwe alidhani ni raisi kuendesha nchi akidhani akiwa mkali mambo yataenda akasahau ukali haufui dafu kwa hela zilizo mfukoni kwa wanainchi. Huwezi kuwaambia wenye hela zao wapi waziwekeze au wapi wazitumia maadam huwafundishi kutafuta hela.

Yeye mwache aishi kwa hela za kodi ambazo hajui sisi wanainchi tunaumiaje ili yeye azitafune tyuu. Sasa sisi wanainchi ndiyo twampiga kisawasawa. Na kumpiga Jiwe ni kumpiga mfukoni kwenye uchumi ndo atashika adabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tambua kwamba, ukali ni muhimu kwa mtu mzima kama ilivyo kwa mtoto.
Jifanye mpole, chekea chekea watu, uone venye watakufanya.
Balanced one, but, who are we, to know exactly balanced ukali, upoje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freddie Matuja wew ni kichwa sana na.mzalendo halisi.

Tuna ardhi lakini hatuwezi kufanya hayo uyasemayo kwasababu nguvu kazi yetu ambayo ni vijana haina elimu maarifa wala haina mitaji.

Hebu angalia. Wahitimu wengi nchi hii ni wahasibu, wachumi, watu wa store na watu kama hao. Huko ndiko tunakopeleka vijana wetu. Serikali ilikuwa ifanye makusudi ili wahitimj wetu wengi wawe wenye taaluma za kilimo na ufugaji pamoja na ufundi. Marekani haikufika kuwa taifa kubwa kwa kuwa na vyuo vingi vya kufundishia masomo ya biashara badala ya ufundi/ teknolojia

Hatuigi hilo ila tunaiga kuwa na uwanja wa mpira mkubwa kama wa kule uingereza
 
Thread bora ya mwaka hii... Naipa 5*

Hii serikali haitaki private sector, serikali ni kama vile ilisha jitoa kufanya kazi na private sector...

Maamuzi mengine tunawalaumu washauri wa rais bure, hivi kuna mchumi aliye mshauri rais serikali inunue korosho kutoka kwa wananchi?

Serikali ilishindwa nini kukaa mezani na private sector kuangalia ni namna gani ya kuongeza dhamani ya ununuzi wa zao la korosho kutoka kwa wananchi
Kimkakati Serikali kuzuia korosho ghafi isiuzwe nje ya nchi hapo niko upande wa serikali.
Kuwaondoka kangomba katika equation, pia niko upande wa serikali.''

Ilitakiwa Wizara ya Kilimo, Viwanda wa biashara na wizara ya fedha ifanya kazi na akina Manka, Masanja au Materu wawezeshwe kumiliki machinery na kupata consutancy ya ku-;process korosho na kutoa various products zenye viwango na ubora na packaging iwe yenye unakidhi global market... chungulia hapa chini
Organic Cashewnut Butter - 170g 5032722305892 | eBay

chocolate Cashewnut 160g | eBay

Tukifanya hivyo processor atarejesh mkopo, atapata foreign currency inayoingia kwetu hapa, hapa... TRA nayo itavuna kodi kubwa unlike mauzo yakiwa raw
 
Serikal ilikurupuka kwenye issue ya korosho. Tatizo limetokea halaf watu wakachukulia ni sehem ya kupatia fame. Matokea yake tunayajua..
Hatuna wafanyakaz makini.. huendakwa hata rais hawaamini wateule wake maana hata yeye anaona madudu yao huku chini.
Thread bora ya mwaka hii... Naipa 5*

Hii serikali haitaki private sector, serikali ni kama vile ilisha jitoa kufanya kazi na private sector...

Maamuzi mengine tunawalaumu washauri wa rais bure, hivi kuna mchumi aliye mshauri rais serikali inunue korosho kutoka kwa wananchi?

Serikali ilishindwa nini kukaa mezani na private sector kuangalia ni namna gani ya kuongeza dhamani ya ununuzi wa zao la korosho kutoka kwa wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom