T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 13,932
- 47,211
Mimi nilitaka kuthibitishiwa dharau aliyoonesha. Hayo mambo ya kuzima simu, kublock watu au kutowajibu huwa nafanya pia. Huwezi kuniletea undezi nikae unanisumbua eti ndo nionekane nakuheshimu. Ukileta deal nikalikataa mara ya kwanza, ukalirudisha tena, ukarudi tena, kwanini nisikublock au kukuzimia simu. Tabia za kimaskini sana kung'ang'ania kitu.Watoto was kiume huwa hawazimi simu, wao huwa wanajibu moja ndio au hapana
Sent using Jamii Forums mobile app
Kiwango chake Gadiel kimeshuka kwa kuwa Yuko benchi. Kiwango chake hakitapanda Tena...mark my words...yeye akae benchi ili awe anashangilia magoli wanayofunga Alina kagere, deo Kanda na wengineo...mchezaji mtanzania mwenye nyodo hawezi kupanda kiwango...abaki Simba msimu unaokuja ila ule unaofuatia itabidi aende kwa mkopo lipuli au ndanda na pia coastal timu rafiki wa Simba...pengine anaweza akapelekwa namungoHapa watu wanaongea kishabiki sana. Gadiel ni mtu mzima na ni yeye mwenyewe ndie anaejua kwa nini alitoka Yanga akaenda Simba kama ambavyo alitoka Azam akaenda Yanga. Anayejifanya kuwa anajua kuwa mchezaji fulani akienda timu fulani atawika sana au kiwango kitashuka huyo muongo kabisa. Zlatan alienda Barca kwa mbwembwe lakini mfumo ulimkataa akasepa zake na mpaka leo bado timu ma lulu na Lukaku akiwa Man U alikuwa utopolo kabisa lakini huko Inter anatupia balaa. Wakati mwingine unakuta mchezaji akihamia timu nyingine aidha kocha au mfumo mzima wa timu aliyahamia unamkataa. Kwa hiyo Gadiiel asihukumiwe kwa hilo bado umri unamruhusu atacheza tu timu yoyote hata nje ya ya nchi na vile vile uamuzi wake uheshimiwe.
Kwa mtizamo wangu Gadiel bado ni mchezaji mzuri ila ana tatizo ni dogo sana linalorekebishika. Kukaba anakaba vizuri sana lakini kwenye kushambulia ndio tatizo lipo. Hajui wakati gani apige krosi na hata akipiga hamlengi mshambuliaji wake, hajui wakati gani acheze "one" "two" na pia hajui wakati gani apige "V" pasi kwa washambuliaji. Hapa ndio Mohamed Hussein anapomuweka benchi. Gadiel huwa anasubiri mpaka adui amfikie ndio apige krosi matokeo yake krosi zake nyingi huwa zinaishi mbavuni kwa mabeki wa timu pinzani. Pia ana tabia ya kulazimisha sana kupiga chenga kupitia pembeni wakati hana uwezo kama wa mwenzake Zimbwe. Na kupiga chenga ni kipaji mtu anazaliwa nacho lakini kukaba, kupiga pasi na krosi vizuri ni mazoezi tu haihitaji kuwa na kipaji. Aliye karibu na Gadiel amuelekeze mambo hayo machache tu basi atarudi mchezoni na maisha yataendelea asisikilize maneno ya watu kuwa kiwango chake kimeisha atazidi kupotea.
Ndugu unachozungumza kina ukweli kwa asilimia kubwa kwa wachezaji wa kitanzania wakikaa benchi basi na wao wanakuwa kama wamekata tamaa hivi. Ila wapo wachache wanaojitambua na mara nyingi sana napenda kuwatolea mfano Juma Abdul na Muzamiru Yasin. Juma Abdul watu wengi walishajua kapotea wakati wa Zahera pale alipomuibua Boxer lakini kwa kuwa Juma Abdul alikuwa anajitambua alipambana na pale alipopewa nafasi alifanya "come back" ya hatari. Muzamiru naye ni kama alishapotea Simba na kila mpenda soka nchini alimshangaa pale alipoamua kuongeza mkataba huku akisema kuwa atapambania namba yake Simba. Kwa kweli ni ujasiri wa hali ya juu unaopatikana kwa mchezaji wa kitanzania. N a kweli na yeye akafanya "come back" ya hatari.Kiwango chake Gadiel kimeshuka kwa kuwa Yuko benchi. Kiwango chake hakitapanda Tena...mark my words...yeye akae benchi ili awe anashangilia magoli wanayofunga Alina kagere, deo Kanda na wengineo...mchezaji mtanzania mwenye nyodo hawezi kupanda kiwango...abaki Simba msimu unaokuja ila ule unaofuatia itabidi aende kwa mkopo lipuli au ndanda na pia coastal timu rafiki wa Simba...pengine anaweza akapelekwa namungo
Safi....ni uchambuzi mzuri kabisa...hongera ndugu...Ndugu unachozungumza kina ukweli kwa asilimia kubwa kwa wachezaji wa kitanzania wakikaa benchi basi na wao wanakuwa kama wamekata tamaa hivi. Ila wapo wachache wanaojitambua na mara nyingi sana napenda kuwatolea mfano Juma Abdul na Muzamiru Yasin. Juma Abdul watu wengi walishajua kapotea wakati wa Zahera pale alipomuibua Boxer lakini kwa kuwa Juma Abdul alikuwa anajitambua alipambana na pale alipopewa nafasi alifanya "come back" ya hatari. Muzamiru naye ni kama alishapotea Simba na kila mpenda soka nchini alimshangaa pale alipoamua kuongeza mkataba huku akisema kuwa atapambania namba yake Simba. Kwa kweli ni ujasiri wa hali ya juu unaopatikana kwa mchezaji wa kitanzania. N a kweli na yeye akafanya "come back" ya hatari.
Kwa wachezaji wa kitanzania kwao benchi maana yake ni kuwa uwezo umeshuka na yeye morali inashuka na kiwango chake kinaporomoka kabisa. Na hata pale anapopewa nafasi anashindwa kabisa kufanya vitu vya hatari kiasi kocha amshahau yule aliyekuwa anampiga benchi. Kwa mfano nawaangalia Kichuya na Luis walipewa nafasi kwenye mechi moja kama sikosei ilikuwa kati ya Simba na JKT lakini alichofanya Luis ni kumuonyesha kocha kuwa anakitu cha ziada cha kuisaidia timu ipate matokeo mazuri "team work" lakini mwenzake Kichuya yeye alitaka kuwaonyesha mashabiki kuwa mpira anauweza. Matokeo yake mpaka leo benchi linamhusu.
Nikihitimisha kwa upande wangu kuhusu Gadiel ni kuwa kila kitu kipo kwenye ubongo wake. Afanya mazoezi ya nguvu, arekebishe mapungufu yake kidogo sana kwenye kushambulia, namna ya kupiga krosi na asiwe analazimisha kupiga chenga kama Mohamed Husein kwani hana kipaji hicho na si lazima sana apige chenga. Baada ya hapo asubiri tu apewe hata dakika 15 uwanjani zinatosha kabisa kumshawishi kocha kuwa yeye naye ana msaada kwenye timu. Na kwa Gadiel kiukweli huwa anapata muda kiasi wa kucheza tofauti na wachezaji wengine ambao toka ligi ianze hawajawahi hata kukaa benchi. N a la muhimu kwa Gadiel na hata wachezaji wengine wanaokalia benchi wasitumie muda mwingi kuwaza watu wanowasema vibaya kuhusu viwamgo vyao badala yake wafanye mazoezi kwa bidii ili wawazibe midomo kama walivyofanya akina Juma Abdul, Saidi Makapu na Muzamiru Yasini.