Yaani huyo binti nilimuoa akiwa na mtoto mdogo wa mwaka mmoja na kama miezi mitatu hivi japo awali hakuwa ameniambia kuwa ana mtoto kwan alikua anahisi labda na mimi ningelimkimbia kama ilivyokua kwa huyo mwanaume wake wa awali ambaye alimkimbia baada ya kumpa mimba akiwa bado ni mwanafunzi sasa mimi nilikutana naye akiwa form four tukatengeneza urafiki ambapo nilikua nikimsaidia mambo mengi ya masomo ukizingatia hakuwahi kusoma form three kwakua alikua kwenye mambo ya uzazi kwa siri na ndipo ilipofika hatua ya kuingia form four akaingia darasani kujiunga na wenzake kitu ambacho nilikuja kugundua baadae kwani mwanzoni hakua muwazi japo nilimbana sana kisa cha yeye kuwa shallow sana kwenye topic za form three akawa ananiambia sikua naelewa kwa hiyo nikimfundisha mm ndo anaelewa kumbe hakusoma kabisa. Basi kwa namna hiyo ndipo mapenzi yalianzia na hatimaye kumchumbia mara baada ya matokeo ya form four kutoka na ndipo nilipokuja kugundua kuwa ana mtoto na nilistushwa sana lkn ikabidi niamue tu kumlea mtoto wake pindi nitakapomuoa na ndivyo ilivyokua nililea mtoto wake ambaye alikua na matatizo ya kiafya ikiwemo kuumwa utapiamlo hali iliyopelekea mtoto kushindwa kusimama mapema na nililishughulikia hilo mpk akaweza kutembea kabisa na ndipo nilipoamua kumpeleka mke wangu masomoni ambapo alinitaka nimpeleke chuo cha ualimu na nilifanikiwa kupata chuo na kumsomesha mpk alipomaliza huku nyuma wakt yeye yuko chuo mimi nilikua na zoezi la kumlea mtoto wake mpk pale alipohitimu masomo yake na hatimaye kujipatia ajira ambayo ndo anayo mpk saaa na hii ajira aliipata baada ya kunipatia mtoto wa kiume. Lakini tatizo lilikuja pale alipoanza kupokea mshahara wake ambapo alianza kunigeuzia kibao kwa kunionesha kiburi cha wazi wazi,ikawa kila siku ni magomvi yasiyo na mwisho mpk nikawa naiona nyumba yangu ni chungu kukalika na kila mkigombana lazima adai talaka yake, hana stara ktk kunijibu ilifikia hatua hata ukijaribu kumkumbusha wema niliomtendea basi atanijibu kirahisi tu eti "umenisaidia kwa sababu unaniona nanoga mbona hao wengine wa kabla yangu hukuwasomesha basi wala kuwahudumia kama ulivyonihudumia mie basi ndo ujue mi nanoga kuliko wale" daah yaani nikikumbuka adha nilizokumbana nazo katika kutengeneza maisha yake ikiwemo gharama za ada, pocket money na usumbufu nilioupata katika kumlea mtoto wake kipindi yeye hayupo halafu leo asione thamani yangu mbaya zaidi ameanzisha mahusiano ya kimapenzi na baadhi ya maafisa pale halmashauri ambao wanashiriki kunifanyia firigisu firigisu kwenye ajira yangu maana nimepona mara mbili kuhamishwa kituo cha kazi ili nipelekwe porini huko ili wao waendelee kula bata kwa Uhuru wao lkn kwa ubishi wangu wakshindwa kulifanikisha hilo na sasa wamehamia mahakamani ambapo wanajitahidi kumuhonga hakim na kumsukuma aendeshe kesi ya madai aliyoifungua huyo mtalaka wangu vile atakavyo mke ikiwemo kuuza nyumba ambayo niliijenga mimi mwenyewe pindi yeye mke akiwa ndo mwaka wa mwisho chuoni na ukizingatia tuna mtoto ukiuliza mahakamni kwa nn tuuze nyumba wakti tuna mtoto kwa nini mimi nisimlipe kiasi fulani huyu mdai kama fidia(ambacho nilipendekeza) ili nyumba iwe mali ya mtoto? Eti hakimu asema huyo mtoto atatafuta yeye mwenyewe akikua yaani inafika kipindi unatamani umzabe makofi hakim kwa namna anavyopindisha sheria na mpk sasa bado kesi hii inaendelea lkn ni katika mazingira magum sana kwangu. Kwa hiyo siwezi kummiss mtu kama huyo aisee