What can be done to prevent our economy from collapsing? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What can be done to prevent our economy from collapsing?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 27, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Some few months ago (In April to be precise) I wrote this thread: https://www.jamiiforums.com/hoja-nzito/125963-on-the-brink-what-is-troubling-tanzanian-economy.html

  In it I asked these questions:

  Na watu wengi walitoa majibu ya kina na mengine ya kudokeza. Leo hii hali ya uchumi inazidi kuwa tete hasa kama factors nyingine zote zikichukuliwa. Kwa mfano hatujui kama lile jengo la serikali lililonunliwa limenunuliwa kwa mkopo au cash na hilo la kutoa kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Tanzani kuna athari gani katika uchumi wetu (as far as I know haikununuliwa kwa mkopo - I stand to be corrected).

  Sasa katika hali inayoendelea sasa hivi kweli kuna namna yoyote ya kuokoa uchumi au ndio kama wenzentu wanavyosema finally the "the chickens are coming home to roost".

  Je ndio wakati wa CCM na serikali yake kujikuta wanalazimishwa kulipa gharama ya sera na utendaji wao? Je ndio wakati ambapo Tanzania hatimaye itajikuta inalazimishwa kulipa gharama ya kuruhusu mfumo wa utawala wa kifisadi? Je, nani ataitwa kuikoa Tanzania endapo uchumi utaanza kuwa vurugu hasa bidhaa za kila siku (vitunguu, nyanya, mikate n.k) zitakapoonekana kuwa ni za juu kuliko uwezo wa watu wetu wengi?
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  I don't think sera zilizopo za uchumi zinasimamiwa inavyotakiwa na serikali. Rushwa inaogopesha! hakuna tena siri jinsi watu wanavyodai na kupokea rushwa. Huo uchumi tutausukuma vipi kama kila kitu kinasukumwa na nini mtu anayesimamia ataneemeka kwanza? TRA, kama kulivyo sehemu nyingine kuna matatizo makubwa ya rushwa.
  Unless we change they way we lead ourselves,we would collapse! This world has no mercy for people who dont want to apply their mind!
   
 3. S

  Shiefl Senior Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aksante sana bwana Mwanakijiji.

  Nchi ina kansa ya uongozi. Na ukishakuwa na huyu mdudu kansa mambo mengi huwa yanaparanganyika kabisa. Watanzania kama ni wazuri wa historia watakumbuka yaliyotukutuka enzi za Mwinyi walijawa na hela mifukoni mpaka kwenye soksi lakini serikali haina hela. Tukaambiwa ni athari za uchumi huria chini ya ruksa kila kitu.

  Akaja Mkapa akabana hela...sera za katika mfumo wa uthibiti wa hela zilikuwa mzuri sana.

  Lakini sasa kwa huyu jamaa kuna maswali mengi ya kujiuliza. Pamoja na kudodora kwa uchumi wa dunia ambayo yeye na watu wa uchumi walitamba sana miaka ile ya mwanzo kuwa uchumi wa Tanzania hautegemii chumi za magharibu lakini wakati hawajatuomba radhi watanzania kuwa walichemka. Wakajitengenezea Economic Recovery Package. Wakagawa kwa wanaowajua wao. Mpaka leo mtoto wa Mkulima anaandikiwa barua na akina Zitto hajibu anang'ang'ania kuuza ardhi ya kwao kwa wamarekani.

  Hivi sasa watanzania watakumbuka noti mpya zinazoonekana kwangu kama feki zimezagaa mitaani japo kuna malalamiko kila mahali kuwa zile ni substandard lakini si Prof wa BOT wala serikali wanaonekana wakifanya lolote katika hili. Kuna uvumi kuwa hizi noti zilivyotua bongo wajanja walizonyakua na kuziingiza kitapeli kwenye mfumo.

  Sasa wewe jiulize nini kitatokea kama siyo kujaa kwenye system?

  Rushwa: Hasa hizi kubwa inazoshirikisha mizengwe kama ya mikataba inajaza unnecessary money in the system. What next...

  Kazi kweli na watz wanaohitaji elimu ya uraia wachache wetu tuna kazi kweli
   
 4. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuruhusu fedha chafu (tena nyingine kupitia BoT) kuingia kwenye mfumo wa uchumi, nadiriki kusema kuwa by December 2011 tutakuwa tunakaribia ku-collapse kabisa ki-Uchumi...

  Hali ya uchumi ni mbaya sana - But very unfortunately - and sad indeed - The President Of the Republic Of Tanzania is very much unaware!!!
   
 5. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  wanasema raisi alisomea uchumi je? Kwanin uchumi unashuka?

  Mipango mizuri isiyotekelezeka.

  Kashfa za ufisadi ni mingi kuliko mipango ya kuikombo tsh.
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  In a few years to come tutaanza kwenda sokoni na kapu la noti kununua mkate kama Zimbabwe.
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Mimi walipo issue new currency notes in January while maintaining the old ones nilijuwa tayari mambo yeshaenda mrama ........na zaidi ya kununua hiyo nyumba kwa $24m na hisi Dowans wamelipwa kimyakimya
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,531
  Likes Received: 5,680
  Trophy Points: 280
  Moja tatizo la nishati lishughulikiwe kidharura haraka sana na gharama za nishati zishuke by 20%,pia central bank isimamie uchumi moja kwa moja kwa kipindi chote hadi inflation itapofikia 5.7% na kabla hawajajitoa wawe wame set policy zitazoendesha uchumi salama bila inflation kuzidi 6% na hizo policy ziwe very close monitored kuzi update.pia kuanzia sasa kwa namna ya pekee kabisa swala la Money laundering liangaliwe kwa umakini tena haraka sana na hapa NBAA,TRA washirikishwe kusimamia utekelezaji wake.pia tutunge sheria ya kuzuia matumizi holela ya dola,kwasasa ni too much,dola huku mtaani ina take over kwa kasi ya ajabu! Kuna mengi lakini kwa kuanzia hapo si pabaya!
   
 9. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sijawahi kuona wala kusikia nchi moja inatumia noti aina mbili. Kibaya zaidi hizo zinazoitwa 'mpya' ndo zina kiwango cha chini kabisa. Fedha haramu zitadhibitiwa vipi?
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  The only solution is removing ruling party from the power
   
 11. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,531
  Likes Received: 5,680
  Trophy Points: 280
  Mkuu kutoa pesa kwenye mzunguko ni zoezi dogo ambalo BOT wanaweza kuiplement kwa muda mfupi tu.
   
 12. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  Kikwete aache visasi na chuki za kiasiasa,ukweli ni kwamba Mkullo na Ndulu wameshindwa ku-deliver and they should be ejected.Dr. Kigoda apewe wizara ya fedha na pia kikwete angeweza kumsogeza ata Prof. Mbilinyi hawa wangemsaidia sana kuliko kung'ang'ania watu waliofeli ku-deliver.
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,531
  Likes Received: 5,680
  Trophy Points: 280
  Tulipofikia hata tuweke chama gani lazima tupate maumivu ili uchumi uweze kuwa stable tena afadhali kipindi cha Ben inflation haikuwa mbaya.
   
 14. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  I wonder if we really have to fear about collapsing of the economy which is actually not existing.
  We would rather fear the collapse of those "parenting countries" like the USA and the Western.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hata mimi nahisi hili. Uchumi wetu unahitaji kusahihishwa au kujisahihisha kwani ulivyo sasa ni unsustainable. Swali litakuwa ni maumivu kiasi gani yatatokea ili tutoke hapa.
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Mbona thread kama hizi akina GB, MS, FF, Karange ...... huwa hawachangii!!!
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Hivi huu tunaouita uchumi wetu bado upo kweli au ulisha collapse siku nyingi? Labda swali lingebalika na kuwa how can we resuscitate our collapsed economy? Viashiria kuwa uchumi umekufa na unahitaji kufufuliwa ni:-

  (i) Uzalishaji viwandani kupungua kwa sababu ya ukosefu wa umeme;
  (ii) Mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na gharama za maisha;
  (iii) Kupungua kwa makusanyo ya kodi za serikali;
  (iv) Serikali sisiyoweza kulipa gharama za uendeshaji wake na kutegemea misaada/mikopo;
  (v) Mgao endelevu wa umeme unaoathiri siyo tu shughuli za viwandani bali hata biashara ndogodogo;

  Wachumi wanisaidie ni viashiria gani vingine zaidi ya hivyo hapo juu vinavyotuambia kuwa uchumi wetu umekufa.
   
 18. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nilisoma hii quote asubuhi ya leo na I wish rais wetu asiyejua ni kwa nini uchumi unaanguka na hajui umasikini unatokana na nini angeiona na kutafakari.
  Na wananchi wanalijua hili lakini kila wakijaribu kuwaondoa hawa jamaa, NEC inabadili mbinu na kuweka watu wao na saa nyingine nguvu kubwa mno inatumika kuwadhdurumu!
  Ngoja tuone kama mwelekeo wa maandamano ya jumamosi unaweza 'to animate' mwanzo wa mapambano mapya!
  View attachment 40057
   
 19. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Uchumi hoi ni matokeo ya serikali hii goigoi.
  Kubadili serikali linaweza kuwa suluhisho.
  Huu ni mtazamo wangu, ninahisi wengi tupo pamoja.
   
 20. m

  mharakati JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  hizi siasa za kimakundi, chuki binafsi na visasi ndiyo zimeanza hata huyu bwana mkubwa atayekuja nae ataweka loyalists wake bila kujali uwezo wa uongozi, uzoefu wao, uzalendo, ari na tija kwa taifa. tunajikuta kama nchi tunanyimwa viongozi wachapa kazi kwa sababu ya upumbuvu wa kisiasa..angalia baraza la mawaziri limekaa kijinga jinga tu
   
Loading...