a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,388
- 1,319
Thanks JingalaFalsafa. Ingawaje katika uhalisia wake "demokrasia inastahiki kulindwa [kwa njia za kidemokrasia] popote pale ulimwenguni," tatizo la Afrika (in most of it) hakuna demokrasia bali viongozi wanatumia mgongo wa demokrasia kujenga na kulinda himaya zao ambazo ni mbaya zaidi kuliko udikteta.
Demokrasia ndiyo impayo haki bilionea kuweka watumishi nyumbani kwake. Ndiyo impayo haki mtu kununua prado, vx ama benzi hali jirani yake hana pakulala, hana mavazi, hana chakula, amekosa madawa, nk...fikiria jirani huyu mnyonge akiamua kuchukua panga kwenda kuiba japo mikate miwili store kwa jirani yake tajiri, pana mlinzi na bunduki, kitakachotokea tunakijua. "Right to own and protect private properties" itamlinda kwa mauaji aliyofanya, MANTIKI JE? Japo mwizi alisukumwa kuiba kwa njaa yake ili asife, demokrasia haijali hilo. Hiyo ndio Demokrasia,kushangaa bunduki ndani yake, ni sawa na kufuga manyigu ukataraji kulina asali.
TUKUBALI TU, DEMOKRASIA SIO NJIA SAHIHI YA KULETA AMANI, UTULIVU, na MAENDELEO kwa nchi zetu za kiafrika. Pamoja sana!
Mungu wetu anaita!