What are random interesting facts about yourself?

Hauwezi kushuhudia maana hautanipeleka penye hao wadudu.
Kinyume chake beba diapers kwa ajili yangu kama haupendi aibu Mla Bata.

pole sana, hutaki kujifunza kukabiliana na hiyo phobia?
 
nimecheka hadi nimelala chini
Cheka tu wakati this is serious problem.
Btw lilikua daraja la relini ambalo ukipita unapaona chini Kwakweli nilishindwa kuvuka. Au kuna madaraja ambayo pembeni hua wameweka njia ya kupita watembea kwa miguu yaani hua sipiti hiyo sehemu.

Sipandagi miti kabisa labda matawi yawe yanafika hadi chini!
 
Pole my dear
kwa mazingira hayo hata mimi nisingeweza kuvuka
 

hongera sana Hannah
 

umepewa kibali na Mungu, hongera sana chief…….mimi pia kidogo.
 
Sina mda/ sijawai kaa nikammis ndugu au mazazi. Ata kama nikimtafta namtafta tu ili asije sema nimemtenga. Sijui kwann tu nipo hiv

Huwa nakubaliwa sana na Watoto yan ata kama simjui anaweza nichangamkia kama vile tunajuana mda mrefu na mm nikiona hvyo uwa nawachangamkia zaid ili wasijihis vibaya.

Watu wengi wanajua mm huwa sili sana kumbe mimi huwa napenda nikae nakula kila mda ila sio chakula cha kula kushiba.
 
tuko sawa kwene hilo la kwanza sema mi nna kingine Cha ziada sipendi kuongoza kwa kifupi sipendi kutumiwa Kama mfano ata Kama kitu nnakijua kiasi gani.... Mara nyingi najifelisha kwa makusudi
 
Sipendi na sitakuja kula miwa na mihogo...
Napenda kulia na kusoma nasoma kila kitu...
Cha ajabu wanaonijua wananibishia nikiwaambia vitu ninavyovipenda.
 
Nikitoka out na mpenz wangu sipendi kuona mwanamke mwingne kapendeza kumzidi mrembo wangu....

Hii ipo automatically kwangu... Nikivutiwa na aina flan ya mavazi or watch or style flan ya nywele, huwa najitahid mrembo wangu asikose hio kitu kabisa.

It's a crazy fact about myself
 
Naogopa maji ya Mto, bahari,... Yani ata Yale Madaraja yanayopita juu ya maji huwa sitazami chini napata kizungu zungu cha ajabu. Kuvuka tu Mto utanionea huruma. Sijajuaga kwanini hii Hali ninayo. Hii Hali kiasi kwamba imenipelekea nisiweze kufika sehemu inayoitwa bichi tangu nizaliwe.

Naogopa kuku jamani ata vifaranga siwez kuvishika, mende, panya.

Napenda kununua kitu chochote kile ambacho nimekipenda ata kama ni cha gharama, siwazii.

Sipendi kuonewa wala kuona mtu aonewa nitapambana.

Napenda zawadi, kununua na kuwapelekea watu ninaowapenda. Ata akiwa ni mwanaume wangu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…