Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,607
Dola bilioni 16.9 zinahitajika ili kutatua janga la njaa linalozidi kushamiri duniani, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo, kiwango cha fedha ambacho dunia inatumia kila wiki kununua kahawa ya kunywa.
Kiwango hicho cha fedha kimetangazwa leo baada ya WFP kutoa Mwelekeo wake wa Mtazamo wa hali duniani kwa mwaka 2025, nyaraka ambayo inatokana na tathmimi ya hali ya mahitaji ya chakula na uhakika wa upatikanaji wa chakula duniani.
Kwa mujibu wa WFP, njaa inaendelea kuongezeka, ambapo watu milioni 343 katika nchi 74 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa ukosefu wa chakula, kiwango ambacho ni ongezeko la asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka jana.
Idadi hiyo inajumuisha watu milioni 1.9 walio katika hatihati ya kutumbukia kwenye baa la njaa, wakati huu ambapo kiwango kikubwa cha njaa kimeripotiwa huko Gaza, Sudan, Sudan Kusini, Haiti na Mali.
Cindy McCain, Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, ameelezea ukubwa wa tatizo akisema ,”Mahitaji ya kibinadamu duniani yanaongezeka, yakichochewa na mizozo, majanga ya mara kwa mara ya tabianchi, na hali ngumu ya kiuchumi. Na wakati huo huo kasi ya ufadhili haiendani na kasi ya mahitaji.”
Uhaba wa fedha mwaka 2024 ulilazimu WFP ipunguze shughuli zake, na kuacha nyuma wengi waliokuwa na uhitaji.
Kusini mwa jangwa la Sahara hali ni tete
Katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, zaidi ya watu milioni 170 wanakabiliwa na njaa, na kufanya eneo hilo kuwa mahali ambapo ufadhili wa WFP utaelekezwa zaidi mwaka 2025.
Mizozo nchini Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na ukanda wa Sahel, ikichanganywa na majanga ya tabianchi yanayochochewa na El Niño, vimefanya janga la njaa kuwa kubwa zaidi.
Operesheni za kibinadmau zimezidiwa uwezo kutokana na ongezeko la ukimbizi huku changamoto za kufikia huduma muhimu ikiibua matatizo zaidi.
Njaa kali Mashariki ya Kati
Eneo la Mashariki ya Kati linashuhudia ongezeko la kutisha la viwango vya ukosefu wa uhakika wa kupata chakula, huku Gaza, Syria na Yemen yakiwa ni maeneo yaliyoathiriwa vibaya zaidi.
Huko Gaza, asilimia 91 ya wakazi wake wana uhaba mkubwa wa chakula, na asilimia 16 wanaishi katika mazingira magumu zaidi.
Syria na Yemen zinakumbwa na changamoto kama hizo, mamilioni ya watu wakitegemea chakula cha msaada kutokana na mizozo inayoendelea.
Asia na Pasifiki nako madhara ya tabianchi
Barani Asia na Pasifiki, watu milioni 88 wanakabiliwa na njaa iliyosababishwa na majanga yahusianayo na tabianchi.
Kitendo cha eneo hilo kuwa kwenye mazingira hatari ya kukumbwa na majanga, pamoja na hali mbaya za kupitiliza za hewa, imevuruga mfumo wa chakula na mbinu za watu kujipatia kipato.
WFP imepanga kuimarisha mifumo ya ulinzi wa jamii na kupanga mapema hatua za kuchukua ili kupunguza madhara ya majanga hayo.
Msaada wa dharura unahitaji Amerika ya Kusini
Eneo la Amerika ya Kusini na Karibea yameathiriwa vibaya mno, kwani watu milioni 40 hawana uhakika wa kupata chakula, na milioni 14.2 wameainishwa kuwa wanahitaji msaada wa dharura.
Eneo ambalo WFP inajikita nalo zaidi kwenye ukanda huo ni kuimarisha mifumo ya uzalishaji chakula, kujenga mnepo dhidi ya tabianchi na kusaidia miradi ya ulinzi wa kijamii ili kuweka utulivu kwa jamii zilizo hatarini na kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.
Wito kwa dunia kuchukua hatua
Ufadhili wa dola bilioni 16.9 utawezesha WFP kulisha watu milioni 123 wenye njaa zaidi duniani mwaka 2025.
“WFP tumejitolea kufanikisha kuwa na dunia isiyo na njaa. Lakini ili kufikia hapo, tunahitaji kwa dharura msaada wa kifedha na kidiplomasia kutoka jamii ya kimataifa ili kubadili mwelekeo wa sasa wa ongezeko la mahitaji duniani na kusaidia walio hatarini zaidi kujenga mnepo dhidi ya ukosefu wa uhakika wa chakula,” amesisitiza Bi. McCain.
Mwaka 2025, WFP itaendelea kupatia kipaumbele na kuwa na mipango inayoendana na mahitaji mahsusi ya kila nchi, na kuoanisha uwezo na rasilimali zake ili hatimaye miradi au mipango yake iwe ya ubora wa hali ya juu.
UN News