Wezi wabuni mbinu mpya jijini Dsm

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
*TAADHARI*

Kuna mtindo mpya wa wizi umevamia jiji la Dar.

Katika sherehe ya harusi ikiwa inaendelea majambazi uja na kuongea na MC wa harusi kuwa kuna gari namba fulani fulani nje ya ukumbi limezuia gari, hivyo MC utangaza na muhusika anapokuwa anatoka nje majambazi hao ujua hakika unakuja na funguo za gari hiyo hivyo unapofika kwenye gari wao huwa wapo na bastora na kukukamata na kukulazimisha kuendesha gari pamoja nao mpaka mbalimbali na eneo hilo kisha uondoka na gari.

Ni vizuri kuwa mwangalifu juu ya hili, Zingatia mambo haya:

1. Usitoke muda huo huo naposikia kuhitajika nje kusogeza gari.

2. Usitoke pekee yako, toka hata na watu wawili au zaidi.

3. Usielekee moja kwa moja kwenye gari lako, kwanza tazama kwa mbali kama kweli gari lako limezuia gari la mtu na hakikisha mtu yupo katika gari hilo na angalia kama kuna watu wengine eneo la gari lako.
Tafadhari Copy na Ku-paste ujumbe huu kusaidia watu, Kama hauna gari shilikisha wengine hili.
 
Ahsante mkuu maana ka gari kangu hata mkopo sijamaliza, naenda nako kwenye sherehe alafu narudi kwa mguu na kipigo juu maana mimi ni mbishi hawawezi kuniacha salama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom