Wezi wa EPA wavuka kitanzi cha mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi wa EPA wavuka kitanzi cha mahakama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Nov 1, 2008.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2008
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wezi wa EPA wavuka kitanzi cha Mahakama

  2008-11-01 12:44:17
  Na Waandishi wetu


  Idadi kubwa ya mafisadi waliopora fedha kutoka Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), iliyokuwa chini ya Benki Kuu (BoT), hawatashitakiwa.

  Hatua hiyo inatokana na idadi kubwa ya mafisadi hao, kukidhi agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa bungeni Agosti 21, mwaka huu, kuwataka warejeshe fedha walizipora ifikapo jana, vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

  Akilihutubia Taifa kupitia televisheni na redio, Rais Kikwete, alisema hadi kufikia juzi mchana, Sh. 69,326,437,650 kati ya 90,359,078,804 ambazo mafisadi walipaswa kurejesha, zilikuwa tayari zimerejeshwa.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, kiasi hicho cha fedha zilizorejeshwa, ni sawa na asilimia 76.7 ya fedha zilizoporwa kwa makampuni 13 ambayo uchunguzi wake ulikuwa umekamilika. Jumla ya Sh. bilioni 133 ndizo zilizokuwa zimeibwa katika EPA.

  Hata hivyo, alisema kampuni tisa uchunguzi wake bado unaendelea, hivyo, Sh. bilioni 43 hazimo katika urejeshaji wa jana.

  Hivyo, kwa takwimu hizo, idadi kubwa ya mafisadi imekidhi kutekeleza agizo la Rais Kikwete, hali itakayosababisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya upotevu wa asilimia 20.3 ya fedha zilizoporwa katika EPA.

  Rais Kikwete, alisema taarifa kamili kuhusu kiasi halisi cha fedha zilizorejeshwa, itatolewa leo.

  Agosti, 21 mwaka huu, Rais Kikwete alilieleza Bunge kuhusu hatua zilizofikiwa na kuchukuliwa katika kulishughulikia suala hilo.

  Pia, Rais Kikwete, aliwataka mafisadi wa EPA, kupitia kampuni 13 zilizolipwa Sh 90,359,078,804, kuzirejesha ifikapo jana.

  Aidha, aliagiza uchunguzi kwa kampuni tisa zilizolipwa Sh. 42,656,107,417 uendelee.

  ``Nimekwishatoa maelekezo kamili kwa wale ambao hawakutimiza malipo, kamati ikabidhi majalada yao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka mara moja, kwa hatua zipasazo za kisheria,`` alisema, akizungumzia kiasi cha asilimia 20.3 ya fedha ambazo hazijarejeshwa.

  Alisema, Mkurugenzi wa Mashtaka ni idara huru ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, akiwa na mamlaka ya kuendesha mashtaka mahakamani, baada ya kupokea taarifa za upelelezi kutoka kwa Jeshi la Polisi na Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

  Kuhusu uchunguzi uliokuwa unaendelea kufanywa kuhusu kampuni tisa, Rais Kikwete alisema, bado anasubiri taarifa mpya kuhusu maendeleo yake.

  Alisema, taarifa aliyopewa wiki mbili zilizopita, inaonyesha kuwa, polisi bado hawajapata majibu kutoka kwa wenzao katika nchi walizoomba msaada.

  ``Hivyo, nakusudia kuwataka waendelee kufuatilia kwa wenzao ili hatua zipasazo ziweze kuchukuliwa,`` alisema.

  Rais Kikwete, aliipongeza Timu ya Mwanasheria Mkuu na kuwashukuru wananchi kwa uvumilivu na uelewa wao wakati wote serikali ilipokuwa inalishughulikia sakata la EPA.

  ``Tumefarijika sana kwa uelewa na ushirikiano wenu, nawaomba tuzidi kushirikiana katika mambo yote yanayohusu mustakabhali wa nchi yetu,`` alisema.

  Rais Kikwete, alisema utaratibu wa kuzigawa fedha hizo kwa ajili ya shughuli za kilimo na miundombinu umekamilika.

  Timu hiyo iliyoundwa Januari 9, mwaka huu, inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika.

  Wajumbe wengine wa timu hiyo, ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP, Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.

  Iliundwa na Rais Kikwete, pamoja na mambo mengine kuangalia taratibu za kisheria ili kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA.

  Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernst and Young, wizi ulibainika katika EPA kwa mwaka 2005/06 ulikuwa katika mafungu mawili.

  Fungu la kwanza, lilihusisha wizi wa sh. bilioni 90, ambazo mkaguzi huyo alipata ushahidi unaothibitisha kuwa fedha hizo ziliibwa waziwazi na kupendekeza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliohusika na wizi huo.

  Kwa upande mwingine, Rais Kikwete, hakuzungumzia suala la madai ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  ``Katika hotuba yangu ya leo, sikuweza kugusia suala la madai ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu serikali inaandaa tamko rasmi litakalowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi,`` alisema.

  Pia, Rais Kikwete, aliwataka wananchi kujiepusha na mambo yanayoweza kuwagawa na kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwao.

  Mauaji ya albino​
  : Awasihi wananchi kutoa ushirikiano

  Kuhusu suala la mauaji ya maalbino, Rais Kikwete aliwataka wananchi kushiriki na kushirikiana katika kuyakomesha.

  Alisema wananchi wanapaswa kuwataja kwa siri watu wanaohusika katika mauaji hayo, ili serikali ifuatilie kwa karibu nyendo zao.

  Suala la OIC
  : Ataka mjadala huo ukome

  Rais Kikwete, amewasihi Watanzania waache kuuendeleza wala kuudekeza mjadala wa suala la Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kulipeleka taifa mahali pabaya.

  ``Mjadala huo unaelekea kuchukua sura ya malumbano baina ya waumini wa dini zetu kuu na kupandikiza chuki baina ya serikali na wafuasi wa dini hizo. Ni mjadala unaosikitisha sana,`` alisema wakati akilihutubia taifa jana usiku kwa njia ya televisheni na redio.

  Rais Kikwete, alikumbusha kuwa, mwaka 1993, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitakiwa kujiondoa kutoka OIC, baada ya kujiunga kwa hoja kwamba (OIC) ni shirika la kimataifa, ambalo wanachama wake ni mataifa.

  Hivyo, alisema kama kungekuwepo na suala la kujiunga na chombo hicho, basi iliyostahili kufanya hivyo ni Serikali ya Muungano.

  ``Hayo ndiyo matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hivyo basi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilijiondoa kwenye OIC na kuiachia Serikali ya Muungano kushughulikia jambo hilo na kuamua ipasavyo,`` alisema.

  Alisema, tangu wakati huo, Zanzibar wamekuwa wanasubiri uamuzi wa Serikali ya Muungano na kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikiulizia suala hilo.

  Aliongeza kuwa, hivi sasa jambo hilo limekuwa mojawapo ya kero kubwa za Muungano zinazoshughulikiwa na Kamati ya pamoja ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi.

  Rais Kikwete alisema, kwa mujibu wa muundo wa Serikali ya Muungano kila kero ya Muungano ina Wizara yake inayohusika nayo kushughulikia.

  Alifafanua kwamba suala hilo ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ndiyo inahusika na kwamba serikali imeamua kufanya utafiti wa jambo lenyewe itakapokamilisha itatoa ushauri kwa serikali zote mbili.

  Hata hivyo, alisema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haijakamilisha kazi yake ya utafiti na hivyo haijawasilisha Serikalini matokeo ya utafiti huo.

  Aidha, alisema baada ya kukamilika kwa utafiti huo, serikali ipewe nafasi itafakari kwa utulivu ili ifanye uamuzi ya hekima yatakayojenga na kuhakikisha taifa linakuwa na umoja.

  Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi kuwa serikali itafanya maamuzi mazuri katika kujiunga na OIC ili kuepuka kuvuruga mambo na kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa nchi na watu wake.

  Malipo ya walimu

  Rais aliagiza uhakiki wa madai ya walimu ufanywe kwa shule moja hadi na mwalimu mmoja na mwingine na sio kuangalia mafaili yao.

  Aidha, aliwashangaa walimu kwa kuendelea na mpango wao wa mgomo uliozuiwa na mahakama kati kati ya mwezi uliopita.

  Madai hayo yanafikia Sh.bilioni 16.4,bilioni 12.2 kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na bilioni 4.2 kwa walimu wa shule za sekondari na vyuo vya walimu.

  Alisema serikali ilikimbilia mahakamani ili kunusuru janga ambalo mfumo wa elimu ungelikuta nchini kwa mgomo huo ambao ungekuwa wa aina yake.

  Alisema haiwezekani kila alichokuwa akidai mwalimu kilipwe, hivyo hilo ni jambo gumu kwa kuwa kuna ushahidi wa kuwepo kwa stakabadhi za kughushi.

  Alisema uhakiki huo utasaidia kung�oa mzizi wa fitina na kudaidai kusikoisha au kuchukua muda mrefu.
  Alisisitiza kuwa serikali inawajali walimu ndiyo maana katika bajeti ya mwaka huu imeongezwa.

  Aliongeza kuwa Aprili, 2008, serikali iliwalipa walimu Shs. 7.2 bilioni, sehemu kubwa ikiwa ni madeni ya nyuma.  SOURCE: Nipashe
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2008
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je ni hicho Watanzania,Wafadhiri na wanaharakati wapenda maendeleo walichokuwa wanakisubiri kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu.
   
 3. M

  Mkora JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa niaba ya wanabaraza WA JF napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wale wote waliochukua pesa za epa na kuzirudisha kwani ni kitendo cha mfano kinachohitaji kuigwa na jamii.

  Kama kila mtu atafanya hivi hatutakuwa na jela hii itaifanya tanzania kuwa nchi ya mfano duniani
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I don't see why we need to stand by and watch Tanzania go down due to the irresponsibility of a number of people. The issues are much too important for these few bandits to be left to decide on ther own!Lets take actions and liberate our nation.
  What JK is doing with his fellow bandits is running public opinion polls and not being responsible for their actions something which is detrimental to the very existence of these state as well as its people.
  JK should willingly stand alone and only alone and very firm otherwise the existing system will be quickest and most radically overthrown by its opponents.
   
 5. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi na wewe tutajuaje kama hela hiyo imerudishwa kuna ushahidi gani,
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Vipi yule mwizi wa kuku kule Kunduchi atumikiaye kifungo cha miaka 3 pale Ukonga ambaye alikamatwa akiwa katika harakati za kukimbia na kuku wa wizi!!
  Japo kuku alirudishwa kwa mwenyewe, mbona yeye hakuachiwa?

  Vipi yule jamaa aloshikwa na pochi ya wizi!!
  Vipi yule Muhasibu alo iba akarejesha fedha kisha akufungwa jela!
  Kumetokea nini! Sheria ya makosa ya jinai iko likizo?!?!
  Tunaweza mtofautisha Rais Kikwete na Wezi wa EPA?????
  Our president has PRIZE TAQ????


  Ukiachia Mabwege wawe vinara wa siasa matokeo yake ni kama haya.
  Huu ni mfano hai kwamba ukiiba iba fedha nyingi za kutosha, rais yuko nyuma yako tayari kupindisha sheria. Ukiiba fedha kidogo jela inakusubiri.
   
 7. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kama sikukosea sheria za jinai zipo isipokuwa humtaka mwizi kurudisha mali alioiba baada ya kumaliza kifungo.
   
 8. Tonga

  Tonga Senior Member

  #8
  Nov 1, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tutahakikishaje kwamba hizo pesa zimerudi na sio KIINI MACHO? jambo hili linatakiwa ufuatiliaji wa karibu sana watz tunaridhika na kitu kidogo sana; huu sio wakati wa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa!
  Pamoja na hao wezi kurudisha fedha hizo, je hukumu nyingine inafuata au ndio imekwisha? hii sheria ni ya wapi na inatumikaje? kwamba ukiiba unapewa siku za kurudisha mali then kesi kwisha? kwanini hao vinara na vigogo wanahukumiwa tofauti na sheria za Tanzania? kama walichukua hizo pesa kwa njia za udanganyifu basi wana kesi ya kujibu pamoja na kuzirudisha. Wanatakiwa kusimama mahakamani na kusomewa mashtka kama wezi wengine!!! tuache kulegeza sheria pale inapowagusa "waheshimiwa"au wafanyabiashara maarufu, sheria ibakie kuwa msumeno ukatao pande zote; mbona JK anazidi kuonyesha udhaifu kila kukicha? hakuna haja ya kuwatia moyo wananchi fedha zimerudi ilhali kuna mambo kibao yamefunikwa katika saga hili. Tunahitaji kujua for sure hizo pesa kama zimerudi na ziko wapi na pili watuhumiwa wachukuliwe hatua za kisheria.
  " Ukitaka kumuua Fisadi usimwangalie usoni"
   
 9. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2008
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Alisema haiwezekani kila alichokuwa akidai mwalimu kilipwe, hivyo hilo ni jambo gumu .........................kwa kuwa kuna ushahidi wa kuwepo kwa stakabadhi za kughushi. ............si awapeleke mahakamani walioghushi na wale wenye madai halai wakalipwa. hapo tungemuelewa..........lakini sasa tunaona kama zuga tu ya serikali......,
   
 10. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwenye sheria kuna kitu kinaitwa precedent(maamuzi yaliowahi kutolewa huko nyuma) sasa kama Raisi kaisha tuonyesha ukirudisha ulichokwepua hushitakiwi mnaonaje tutumie hii precedent kuchanga hela na kuwalipia wote walio mahabusu na jela(tuanze na wenye kesi zisizozidi laki 1).Nawahakikishieni watabaki mahabusu na wafungwa wachache sana huko jela na gharama za magereza kushuka mno.
   
 11. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2008
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tarehe 31 mwezi wa kumi, Mheshimiwa Rais alihotubia taifa kama ilivyoad yake, ila kwa hotuba hii mambo yalikuwa tofauti kidogo, wananchi wengi kwa mara ya kwanza walipata kiu ya kutaka kumsikia Rais wao kipenzi atasema nini mwezi huu. Si kwasababu niwasikilizaji wazuri wa hotuba zake bali waliamini kuwa siku hii ilikuwa muhimu kwani wangejua mustakbali wa nchi yao.

  Yapo mambo makubwa matatu ambayo yaliwapekelea kutega masikio yao. Moja ni suala la Akaunti ya Madeni ya Nje yaani EPA. Siku hii ndiyo ilipangwa kujua hatma ya wale wote waliotuhumiwa kuhusika katika ukwapuaji wa fedha kwenye akaunti hii. Suala si kutaka kuwajua bali kujua wamechukuliwa hatua gani...ndio hapa hoja ni hatua kwani hadi mtoto mchanga anajua nani kahusika na ukapuaji huo, shida ni namna watakavyoshughulikiwa hasa ukizingatia wengine ni "MARAFIKI WAKUBWA WA MHE."

  Pili, ni suala la mgomo wa walimu...bahati mbaya hili nililipa kisogo kwa kuwa niliamini walimu wako makini kufuatilia MHE. atasema nini hivyo kwangu halikuwa muhimu sana kwanza hoja ya msingi inafahamika haina ubishi yaani wapewa CHAO HAKUNA UJANJA UJANJA katika hili hata kama serikali iende mahakama ya kimataifa pale Arusha lazima mwisho wa siku watoa cha watu..nani kakwambia ualimu wito huku wengine wananeemeka kirahisi...??

  Jambo la tatu ni suala la Richmond (hili sikumbuki alitoatamko gani) maana sikulipa umuhimu sana, ndio nani asiyejua kuwa Bosi wa Mawaziri alihusika eeh nawachia waheshimiwa wabunge pengine wao watakuwa makini kuhakikisha maamuzi yao yatatiliwa mkazo kwa kuwa hayafuti yako kwenye kumbukumbu za hansard (sijui ndo hivyo maana kimombo kinanipa shida kidogo). Hapa tuliambiwa wadau walihusika walishawajibika inatosha maana si mchezo kutoka kwenye uwaziri hadi ubunge wa back bench inauma japo wengine mnachukuliwa kirahisi ,nyie waulize wale waliomaliza muda wao iwe kwenye ubunge au hata mashindano ya umiss utaona wanavyohaha kurudi kwenye hadhi yao hata ikiwa kwa kuwahonga waandishi wa udaku wawatoe frontpage bila kujali ni habari gani.

  Hee kumbe natoa hotuba, ngoja nimalizie hapa kwa kusema "SIJARIDHISHWA NA NAMNA MHE. ANAVYOSHUGHULIKIA MATATIZO YA NCHI....kama ataendelea na staili hii ataandika historia mpya ya kutawala kipindi kimoja toka tupate uhuru." HABARI NDO HIYO, WAPAMBE FIKISHENI KAMA ILIVYO.
   
  Last edited: Nov 1, 2008
 12. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Duuu sijui mahakimu wangapi watahitajika na prosecutors wangapi watahitajika na kesi zitadumu miaka mingapi?mimi nadhani kunahitajika subira.Nadhani wizara ya elimu ndiyo ni wizara kubwa kuliko zote imagine kila kijiji kina shule moja ya msingi ambapo kuna waalimu wasiopungua watano.Na sasa karibu kila kata kuna shule ya sekondari ingawa .ingawa baadhi zina mwalimu mmoja.
   
Loading...