Wakuu niko nchi fulani huku majuu. Nina rafiki yangu Mnigeria, kanisimulia kwamba rafiki yake alikuwa ameoa mke mzuri tu na wote walikuwa waajiriwa wa serikali. La ajabu ni kwamba, majukumu yote ya nyumba aliachiwa baba tu mfano ( kulipia pango, ada za shule kwa watoto na chakula). Huku nyuma kumbe mke alikuwa akitumia mshahara wake kujenga,na alifanikiwa kujenga nyumba mbili chini ya umiliki wake.
Wakati huo nyumba ya familia iliyokuwa ikijengwa na mumewe haikuweza kukamililkka kwa wakati kwa sababu ya majukumu niliyoyabainisha hapo juu. Sasa kwa kuwa walikuwa wamepanga na baada ya mke kukamilisha ujenzi kisirisiri alimshawishi mmewe wahamie katika nyumba mpya eti aliyoiona inafaa, kwa bei sawa na ile waliyokuwa wamepanga. Kwa kuwa nyumba ilikuwa mpya mmewe akashawishika kuhamia bila kujua kuwa ni nyumba ya mkewe. Na kodi aliendelea kulipa kama kawaida kupitia mwakilishi bandia aliyewekwa na huyo mama. Jamaa alikuja kugundua kuwa nyumba ile ni ya mkewe baada ya miaka minne. Yeye aliamua kumuacha mkewe wakati huohuo. Wewe je ungefanyake? ukichukulia kuwa tayari mna watoto?