Emily magnus
JF-Expert Member
- Apr 7, 2026
- 821
- 1,503
Ngoja mimi niendelee kuwa nyenyekea.Mimi sina watu ila kuna watu walifanya niwe wa kwao ila baadae nikatoroka nikakataa kwa sababu walitaka niwe wao huku wao hawakutaka wawe wa kwangu pia ili mzani u balance
Sasa hivi nina mtu/watu ila na wao wakileta ubinafisi nao nitawatoroka kwa amani
Soma vizuri usichanganyikiwe
Kama huna hela, hata uwalimie mashamba yao yote. Utabaki kuwa mtu wao.Jenga mahusiano imara, mkono mtupwi haulambwi, na jifunze pia kuwa mwenyewe just incase!
Sahihi kabisa.Ukipata shida ya gafla ukawa unahitaji 1M ya harakaharaka ,na wakati huo uko vibaya ndio utajua kama una watu au viatu.
Mke wangu ni mtu na nusuKikawaida kwenye maisha watu tunategemeana
Iwe kwenye afya au ugonjwa, kuna muda kila mmoja wetu huhitaji watu. Kuna msemo unasema watu ni mtaji
Lakini utakuta wengine wanasema, Mimi nipo kivyangu, sijui cha ndugu wala marafiki
Wengine huamini ukipata pesa watu watajitokeza wenyewe, kana kwamba pesa ni sumaku inayovuta kila kitu pesa subuni ya roho
Ukweli ni kwamba, watu tunahitajiana kwa namna nyingi sana
Unaweza kuwa umefungua mradi wako, lakini ili ufikie malengo lazima uwe na team ya watu wa kushirikiana nao
Kuna wakati unaweza kuumwa mpaka ushindwe hata kujisogeza hapo utahitaji watu wakusaidie
Ukiwa mahabusu, utahitaji mtu wa kukutolea dhamana
Ukiandaa sherehe, ili ifane na iwe na furaha lazima watu wajitokeze kulingana na mialiko uliyoitoa
Maana yake ni kwamba, watu tunahitajiana
Swali ni je, wewe una watu?
Una watu ambao ukiwaita wanaweza kuja?
Ukipata matatizo unaamini watakuwa pembeni yako, au ni watu wa misimu leo wapo, kesho hawapo?
Na moja ya watu tunaowazungumzia hapa ni ndugu
Ndugu zako ukiwaita watakuja? Au ni wewe ndiye unayewakimbilia kila wakati? ndugu vichomi
Hivi una mtu anayoweza kukukimbilia maji yakizidi unga?
Au upo kwenye kisiwa chako mwenyewe, lonely 🙁
ShesRise_1
Amen🤔🤔🤔🤔🤔
Kakweli Mungu awabariki sana nami anibariki nisiwaache wanaponihitaji.
HongeraMke wangu ni mtu na nusu
ExactlyIli ujue una watu ama watu ndiyo wana wewe pitia kwanza changamoto.
Hii ya kusema una watu muda wa kugonga glass🥂🍻 ❌❌
Noma mkuuKiukweli mimi sina watu na watu wenyewe hawana mimi kiufupi niponipo tu
Kwahiyo hata ukipata msala hutakua na msaada?Mimi sina watu.
Hongera pla Kwa kuwa na MUME BORAHongera
Nimeolewa kumbe 😆Hongera pla Kwa kuwa na MUME BORA
Kwahiyo hata ukipata msala hutakua na msaada?
Nakuelewa aisee wengi tupo hivyoMsaada napata kwa total strangers tu, ila sio ile kusema rafiki flani au Ndugu fkani hakuna hyo.