PostGE2025 Wewe ndiye umetutia doa baya kabisa!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,035
Reaction score
142,947
1. Kwa kuwafunga wapinzani wako wasishiriki uchaguzi.

2. Watu wanaokukosoa kutekwa. Hupendi kukosolewa.

Job Ndugai aliposema mambo ambayo yalionekana yanakukosoa wewe, ukamfukuza uspika.

Dokta Slaa aliposema mambo ambayo yalionekana kama yanaukosoa utawala wako, ukamvua ubalozi.

Humphrey Polepole yeye si tu ukamvua ubalozi, akatekwa kabisa na pengine ashauawa.

Gwajima alipoukosoa utawala wako, naye ukaanza kumnyanyasa.

Mdude Nyagali alitekwa na pengine ashauawa

Wakenya na Waganda walipokuja kuonyesha mshikamano kwenye kesi ya Lissu, wakatekwa wakaenda kuteswa na kufirwa.

3. Siku ya uchaguzi ilipofika watu wakakukataa. Hawakwenda kupiga na wengi wakaingia mabarabarani kukupinga.

Ukawatuma majambazi wako waende kuwaua watu kiholela.

Umeua maelfu ya Watanzania. Umeua hadi watoto wadogo.

4. Kwa maajabu, baada ya siku mbili tokea siku ya uchaguzi, tume yako ikakutangaza kuwa wewe ndo mshindi wa uchaguzi na eti ulishinda kwa 97.66% ya kura zilizopigwa ambazo ni milioni 32 na ushee.

Huna hata haya. Hakuna Watanzania milioni 31 waliokupigia kura.

5. Kama hilo halitoshi, ukaenda ukaapishiwa uchochoroni huko bila hata kuwapa fursa hao wapiga kura wako milioni 31 kusherehekea ushindi wako.

Halafu leo unajishebedua eti yaliyotokea yametutia doa!

Sikiliza wewe, wewe ndo umelitia doa taifa.
 
Loading........
 
Msikilize ikongo Anawachana TEC


View: https://youtu.be/B5pHrjsXXDM?si=pB_5aclLFa1DeqEB
 
When a clown moves into a palace, he doesn't become a king; the palace becomes a circus
 
Baba yako naamini yupo Proud sana kuwa na kijana mwenye akili nyingi kama wewe.

HONGERA SANA

InaumaSana/ItHasAForkVery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…