Wewe muongo,unabisha?

Wewe muongo,unabisha?

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Upendo maana yake ni kumkubali mwanadamu mwenzako bila kumlinganisha au kumpa sharti lolote,unamkubali kama alivyo
'
Kwa maana hiyo ndogo tu unaweza tu kugundua kuwa hujawahi kumpenda yoyote hata mwanao
'
Lakini katika wakati ambao unaishi bado unahitaji upendo,kumbuka upendo sio ngono!
'
Hata ujifyatue akili kiasi gani unatamani upendwe tu,cha ajabu wewe hauko tayari kumpenda mtu kwa maana hiyo hapo juu,lakini unataka upendwe hivyo!
'
Ulishawahi kupenda?Sidhani,hata huyo ulie nae unamdanganya tu!
 
::
Je,wale wanaofikia hatua ya kujiua kwa ajili ya kupenda,,
Eiyer unawaweka kundi gani?
=
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo me, nisie wahi kupenda ni mkweli enheeeee?
 
Tetra kama nilivyosema mwanzo,upendo hauna uhusiano na ngono,halafu kupenda hakuna limit,kwamba unampenda mmoja kuliko mwingine
'
Ukishaingia kwenye hali kama hiyo ujue hauko kwenye upendo,hauko kwenye upendo kwa kuwa kanuni ya upendo haielekezi kubagua,huyu umpende kwa kiasi hiki huyu kile
'
Huyo anaejiua na yule anang'ang'ania kwenye ndoa au uhusiano unaomuumiza na kumdhalilisha,ambae ni katili kwa mwenza wake,au anavunja mahusiano hovyohovyo hawana tofauti,ni wagonjwa
'
Ukikagua utagundua kwenye malez yao kuna tatizo la upendo
'
Binadamu yoyote anahitaji upendo,akiukosa either atakuwa katili sana au atakua zezeta sana kwenye suala la mahusiano na maisha kwa ujumla
'
Ukatili utakuja pale mtu huyu atakapokua anafanya ukatili huo kwa kulipiza kisasi kwa kunyimwa upendo na wazazi au walezi wake
'
Uzezeta unakuja pale mtu huyu atakaponyimwa upendo kwenye malezi kitendo kilichomfanya akose kujiamini na ajione bila mpenzi hajakamilika na ndipo kujiua kunapokuja
'
Kumbuka aina zote za watu hao hufanya hayo huku wakiamini wako sahihi!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom