katika gazeti la mwanaspoti kuna habari kuwa okwi aligoma kufanya mazoezi na klabu yake ya yanga siku ya jumanne akishinikiza amaliziwe fedha yake ya usajili. Okwi alisajiliwa kwa dola 100,000 lakini uongozi wa yanga haukumpatia fedha zote na walikuwa na makubaliano maalum. Walimpatia dola 60,000 kwa kuanzia (Mwanaspoti).
Sasa baada ya okwi kugoma kufanya mazoezi gazeti la mwanaspoti lilimhoji kiongozi mmojawapo wa yanga na akanukuliwa hivi:
Hivi tumpe dola 40,000 Okwi kwa kipi cha kutufariji alichotufanyia? Nataka nikwambie kama Okwi anataka fedha zake jibu ni rahisi sana, aonyeshe kwenye mechi aone kama atazikosa tena zitakuja bila ya kuomba na hilo si kwa Okwi pekee, bali ni kwa wachezaji wote, fedha tunazo lakini hawatutendei haki.
Tunatumia fedha nyingi kuwalipa mishahara mikubwa, lakini angalia mchezo wetu uliopita wanakubali kufungwa kirahisi na hata haiwaumi, tena kwa timu ambayo wanalipwa malipo madogo na tatu wakiwa pungufu, sasa wanakuja wachezaji hao hao eti wanadai fedha, hatuendi hivyo.
Sasa mimi ninachojiuliza kiongozi huyu anaongea hivi akijua fedha iliyobaki haikukubaliwa kimaandishi au anaongea kufurahisha mashabiki? kama fedha iliyobaki iko kimaandishi huyu kiongozi ataongeaje maneno kama haya!
Ninavyojua mimi fedha ya usajili ni tofauti na 'bonus' na mshahara, mshahara au bonus itategemea na perfomance ya mchezaji, nidhamu ya mchezaji, na mafanikio ya timu. Mshahara unawezwa katwa kutokana na nidhamu ya mchezaji kama ilivyoainishwa kwenye mkataba.
Je wadau eti inawezekana vipi fedha ya usajili ukahusisha na perfomance ya mchezaji? Je okwi anadai kile ambacho hakipo kwenye mkataba au kiongozi kasahau kusoma copy ya mkataba?