EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,108
Kumekuwa na namna nyingi ya watu kusherehekea sikukuu, wengine hunywa pombe mpaka kuzimika, wengine hutoka na familia zao na kwenda sehemu mbalimbali, wengine huenda makanisani na misikitini na kumshukuru muumba wao. Wengine hutoka na wapenzi wao na kuishia kupeana nanihii. Kwa wale wa Dar wengine hujazana Coco Beach utafikiri siku nyingine bahari huwa imehamia Kimara Korogwe na siku hiyo tu ndio inarudi. Ila kila mtu husherehekea kwa namna yake. Je wewe roho yako huwa inasuuzika ukisherehekea vipi sikukuu?