Western Wall Israel ina Historia gani?

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
886
Nimeona ziara ya Trump Israel, moja ya sehem alipotembelea ni WESTERN WALL. Kwa mwenye kujua naomba anielimishe, hiyo Western wall ina hadhi gani. Maana nimeona ni ukuta wa zamani ila unapewa heshima kubwa.
 
Western wall, rejea huko nyuma wakati wayahudi wanarudi kwa wingi toka ulaya walikokimbilia na kukuta nchi yao ya ki-hitoria inakaliwa na waparestina. Mwaka 1948 walianzisha taifa lao upya chini ya waziri mkuu Bwana David Ben GURION. Wakati huo Yerusalem mji wa Daudi (the city of David) ulikuwa ukikaliwa kwa pamoja na waparestina na hao wayahudi waliokuwa wakirudi kwa hasira kali baada ya vita kuu ya pili ambapo wayahudi zaidi ya million 6 waliuliwa na wanazi chini ya rais Adolf Hitler aliyetawala ujerumani nzima kabla ya kujengwa ukuta wa Belrin kuigawanya ujerumani ili isiwe na nguvu ya kuanzisha mavita mengine.

Ikaja wakati wa vita vya siku sita mwaka 1967 ambapo lengo kuu la vita hii ilikuwa ni kuifuta Israel katika uso wa dunia vita ilipangwa kutelelezwa na mataifa 13 ya kiarabu chini ya mbabe wao wa wakati huo Rais Gammal Abdul Nasser wa Misri. Kwa muda wa siku 6 tu waarabu wakawa wameshindwa vita vibaya sana katika vita hiyo na taifa moja dogo tu la Israel chini ya waziri mkuu Bibi Golda Meir.

Wakati wa vita hiyo waarabu walipokwa maeneo mengi kama Jangwa la sinai lote, milima ya kimbinu ya goran, ukingo wa magharibi wa mto Jordan na ukanda wa gaza.

Yerusalemu kwenyewe mji wa mfalme Daudi katika vita hii wanajeshi wa miavuli wa Israel (Israel par-trooper) waliuteka mji wote na zile sehemu zilizokuwa zinakaliwa na waparestina sehemu mojawapo ikiwa ni hiyo Western wall, kwa maana wayahudi waliikomboa Yerusalem yote mpaka western wall waparestina wakawa wamefurushwa kwenye mji huo moja kwa moja ukatangazwa ndio mji mkuu wa Israel badala ya Tel.Avivi.

Western wall ikawa ni sehemu ya ki-historia maana ilikuwa inakaliwa na waparestina baada kuuchukua mji wote wayahudi wakaufanya ukuta huo kama sehemu ya matambiko yao ambapo ni huhusu kuukamata tu ukuta huo, desturi hiyo ilianzia baada ya vita na imeendelea hadi leo mgeni maarufu yoyote akiingia Yerusalamu hupelekwa akauguse huo ukuta kama sehemu ya heshima ambayo wayahudi humpa mgeni wao huyo kuadhimisha Israel kukamata Yerusalem nzima.

Hii ni kwa kifupi tu mleta Mada.

Lakini ningeenda kwa undani zaidi muda hauniruhusu ningekueleza kwamba mji wa Yarusalem chini ya Mfalume Daudi miaka ya 70 B.C ulianza kujengwa na kukua lakini umepigwa na kupigwa na kuchomwa moto saa ingine, ni hiyo western Wall iliyobakia imesimama tangu enzi za mfalme Daudi sehemu zingine zimepigwa na kuharibiwa na kujengwa upya yenyewe hiyo westrn wall ipo tu mpaka leo.
 
Back
Top Bottom