Nadharia ya nchi kuitwa ya Magharibi au Mashariki iliamuliwa na matokeo ya vita vya pili vya Dunia ambapo Adolf Hitler akiungwa mkono na nchi za Austria Italy na Japan walishindwa vibaya na muungano wa nchi za kijamaa zilizoundwa na Urusi Yugoslavia Czechoslovakia Poland na Hungary. Mgawanyo wa WEST na EAST ulianzia katika mji wa BERLIN nchini Ujeremani ambapo majeshi ya kisoviet pamoja na washirika wake walikuwa wamefika kabla ya kutangazwa kusitishwa vita vya pili ya Dunia.
Mji wa Berlin kabla ya kisitishwa vita ulikuwa umeishatekwa nusu yake na ilibakia kuvuka mto tu kuingia upande wa pili kwa kuwa kwenye lango kuu lilikuwa limeisha shikiliwa na wasoviet. Kwa kuwa nusu upande wa mashariki mwa mto ulikuwa umeishatekwa na wasoviet nusu nyingine ya magharibi ilikuwa bado iko mikononi mwa majeshi ya wajeremani na washirika wao. Kwa namna hiyo Ujeremani hasa(BERLIN) ilijikuta ikigawanyika vipange viwili vya Ujeremani magharibi na mashariki
Mfumo wa utawala kwa maana ya uchumi na siasa za Ujeremani magharibi ulikuwa ni wa kibepari tangu mwanzo, kwa hiyo waliendelea kujiendesha kwa misingi ya uchumi wa viwanda na mitaji wakati Ujeremani mashariki walianza kujiendesha katika misingi ya ujamaa wa kikomunist. Baada ya kuisha vita USA ilikuja ingia Europa kama mfadhiri wa mradi wa kuijenga upya Europa uliofahamika kama ''Marshall Plan'', Na kwa kuwa America ilikuwa nchi ya kibepari ilifadhili sehemu ya magharibi kuanzia katikati ya mji wa Berlin kwenye ule ukuta maarufu na kwenda hadi maeneo yote yaliyoathirika na vita hadi kwenye pwani ya bahari ya Atrantic.
Nchi zote zilizoko magharibi ya ukuta wa Berlin kuanzia Baltic sea kunyoosha hadi kuipata Italia kwenye pwani ya Mediterranean sea bila kuiingiza nchi za kijamaa zilikuja kujiimarisha na kujijenga kiuchumi kama mabepari na hatimaye kuwa wafadhiri wakubwa wa dunia hii. Dhana hii ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na nchi zinazoendelea kutafuta misaada kwa kuangalia kama mfadhiri ni nchi ya kibepari au kikomunisti kwa maana ya WEST au EAST hadi siku ya leo.