Warumi 1 : 26-32
1.26 Hivyo Mungu aliwaacha
wafuate tamaa zao za aibu, hata
wanawake wakabadili matumizi
ya asili kwa matumizi yasiyo ya
asili;
1.27 wanaume nao vivyo hivyo
waliyaacha matumizi ya mke, ya
asili, wakawakiana tamaa,
wanaume wakiyatenda
yasiyopasa, wakapata nafsini
mwao malipo ya upotevu wao
yaliyo haki yao.
1.28 Na kama walivyokataa
kuwa na Mungu katika fahamu
zao, Mungu aliwaacha wafuate
akili zao zisizofaa, wayafanye
yasiyowapasa.
1.29 Wamejawa na udhalimu wa
kila namna, uovu na tamaa na
ubaya; wamejawa na husuda, na
uuaji, na fitina, na hadaa; watu
wa nia mbaya, wenye
kusengenya,
1.30 wenye kusingizia, wenye
kumchukia Mungu, wenye jeuri,
wenye kutakabari, wenye
majivuno, wenye kutunga
mabaya, wasiowatii wazazi wao,
1.31 wasio na ufahamu, wenye
kuvunja maagano, wasiopenda
jamaa zao, wasio na rehema;
1.32 ambao wakijua sana
hukumu ya haki ya Mungu, ya
kwamba wayatendao hayo
wamestahili mauti, wanatenda
hayo, wala si hivyo tu, bali
wanakubaliana nao wayatendao.