Wenzangu wa Arusha wanajuta

Wenzangu wa Arusha wanajuta

Nilipokuwa katika viunga vya Bungeni Dodoma kufuatilia nyendo za Wabunge wetu wa CCM na hotuba za Bajeti, nilipokea ujumbe wa kichama ulionitaka kwenda Arusha kwa ajili ya mapambano ya kisiasa kuhakikisha kuwa CCMinaibuka na ushindi wa kishindo katika Kata zitakazofanya uchaguzi wa Madiwani jijini humo.

Kwa kuisoma haliya mkoa wa Arusha,nikagoma kwenda Arusha kidijitali(#Siendi Arusha). Wenzangu wakanidhihaki.Wakanicheka. Wakanitambia na posho zao za karibu miezi miwili ya kuwa Arusha. Sasa, mambo ni tofauti. Hali ya kisiasa jijini Arusha haiwapi raha makada wenzangu wa CCM. Wanabanwa mbavu mno.

Kiukweli, CCM iko katika hali mbaya na inafifia katika kupata ushindi wa angalau Kata moja ya Arusha. Kila mbinu,za kipropaganda na kiintelijensia,inagonga mwamba Arusha.Sasa napongezwa na wenzangu wa Arusha. Wananiona kama muona-mbali. Wao wako nafasi finyu kujinasua.Wametakiwa kuhakikisha kuwa 'wanapata' hata Kata moja.

Wanajuta kuwa huko wakiisubiri Jumapili ya tarehe16/6/2013 kwa hofu,tashwishwi na matumaini!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Eti umelipwa per diem ya siku ngapi? Na ni kiasi gani kwa siku? Bila shaka hii fedha ndiyo inazuzua wengi. Nijibu tafadhali.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hahahahahahahaha kiongozi wewe ni Bandia tupu. Hata aibu huna, si ungejenga propagandur yenye muelekeo hii Ovyo na haina hata taste . Very Very Cheap Politics. kelele za nini na jumapili iko hapo corner, ukweli utalipuka wenyewe.

Mimi nitaunga mkono yoyote yule atakayeshinda kihalali. Ila Jambazi Lema lazoma aondolewe kwa kila hali na mali. Hatufai wana Arusha
Wana Arusha walikuteua lini uwe msemaji wao?
 
pressure inapanda, pressure inashuka.

Muda sio mrefu hapa Arusha CCM mkoa Nape Nnauye kaitisha kikao cha wagonjwa wa ccm kupeana matumaini.
kila mjumbe wa kikao hichi cha CCM Mkoani Arusha usiku huu kalipwa Tsh.10,000/= ya chai na kama kianzio, pia jumamosi jioni wajumbe husika watakutana kupanga njama ambazo zitafail kwasababu ni za kitoto na tumeshazijua.

CCM kwenye Mabango, CHADEMA kwenye mioyo yetu.
 
Back
Top Bottom