Nilipokuwa katika viunga vya Bungeni Dodoma kufuatilia nyendo za Wabunge wetu wa CCM na hotuba za Bajeti, nilipokea ujumbe wa kichama ulionitaka kwenda Arusha kwa ajili ya mapambano ya kisiasa kuhakikisha kuwa CCMinaibuka na ushindi wa kishindo katika Kata zitakazofanya uchaguzi wa Madiwani jijini humo.
Kwa kuisoma haliya mkoa wa Arusha,nikagoma kwenda Arusha kidijitali(#Siendi Arusha). Wenzangu wakanidhihaki.Wakanicheka. Wakanitambia na posho zao za karibu miezi miwili ya kuwa Arusha. Sasa, mambo ni tofauti. Hali ya kisiasa jijini Arusha haiwapi raha makada wenzangu wa CCM. Wanabanwa mbavu mno.
Kiukweli, CCM iko katika hali mbaya na inafifia katika kupata ushindi wa angalau Kata moja ya Arusha. Kila mbinu,za kipropaganda na kiintelijensia,inagonga mwamba Arusha.Sasa napongezwa na wenzangu wa Arusha. Wananiona kama muona-mbali. Wao wako nafasi finyu kujinasua.Wametakiwa kuhakikisha kuwa 'wanapata' hata Kata moja.
Wanajuta kuwa huko wakiisubiri Jumapili ya tarehe16/6/2013 kwa hofu,tashwishwi na matumaini!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam