Wenyeviti wa vyama pinzani wakutana

Wenyeviti wa vyama pinzani wakutana

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
Dodoma. Wenyeviti wa vyama vya Upinzani vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR-Mageuzi, jana usiku walikutana ili kutoa kauli ya pamoja, kutokana na hotuba ya ufunguzi wa Bunge kwa maelezo kuwa tayari Rais amevuruga
mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Wakati viongozi hao wakikutana, Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji, Christopher Mtikila alisema, Rais ameingilia mchakato na kutoa maelezo jinsi ya kuandika Katiba.

Wakizungumza na gazeti hili jana mara baada ya hotuba hiyo, Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Ibrahim Lipumba, walisema wameipokea kwa masikitiko makubwa hotuba hiyo.

"Tunakwenda kujadili hotuba ya Rais na tutatoa msimamo wetu," alisema Mbowe.

Awali Katibu wa muda wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Julius Mtatiro alisema Rais Jakaya Kikwete amevuruga mchakato wa
Katiba, kwani walitarajia angetumia mamlaka yake kama Rais kuwaunganisha.

"Rais tulitarajia angeongea kama mkuu wa nchi, lakini amezungumza kama Mwenyekiti wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo wa Muungano jambo ambalo hatukulitegemea," alisema Mtatiro.

Alisema kwa Rais kutoa msimamo ni sawa na mwongozo jambo ambalo limevuruga mchakato mzima.

Hofu ya kuvunjika Bunge Wakizungumza nje ya Bunge, baadhi ya wajumbe wameeleza kuwa hotuba ya Rais Kikwete kama ikitekelezwa uwezekano wa kupata Katiba Mpya utakuwa mgumu.

Mjumbe Luhaga Mpina alisema kwa jinsi rasimu ilivyoandikiwa na kama muundo wa serikali mbili ukipita basi rasimu ya Katiba itabidi iandikwe upya.

"Rasimu yote imetengenezwa kwa mfumo wa serikali tatu sasa hapa kuna hatari ya Bunge kukwama ," alisema.

Mtatiro kwa upande wake alisema sasa kuna hofu ya kushindwa kupatikana Katiba Mpya kwani Rais amewachanganya wajumbe na kama watapitisha maoni yake itabidi rasimu kuandikwa upya.
 
Hiyo n rasimu. wenye wajibu wa kutunga katiba ni wajumbe maalum wa bunge la kutunga katiba.
kikwete kazindua bunge kama mgeni rasmi.
Amewaasa muisome rasimu ukurasa kwa ukurasa. kifungu kwa kifungu. ibars kwa ibara neno kwa neno kusudi muielewe na muelewe mnachokijadili.
Tanzania tuna wana siasa njaa. Mnataka yenu tuuuu ndio yasikilizweee!
kawaambia jengeni daraja mkifanya masihara tutagawana mbao.
 
Dodoma. Wenyeviti wa vyama vya Upinzani
vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na
Chama cha NCCR-Mageuzi, jana usiku
walikutana ili kutoa kauli ya pamoja,
kutokana na hotuba ya ufunguzi wa Bunge
kwa maelezo kuwa tayari Rais amevuruga
mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Wakati viongozi hao wakikutana, Mwenyekiti
wa Chama cha DP Mchungaji, Christopher
Mtikila alisema, Rais ameingilia mchakato na
kutoa maelezo jinsi ya kuandika Katiba.

Wakizungumza na gazeti hili jana mara baada
ya hotuba hiyo, Freeman Mbowe, James
Mbatia na Profesa Ibrahim Lipumba,
walisema wameipokea kwa masikitiko
makubwa hotuba hiyo.

"Tunakwenda kujadili hotuba ya Rais na
tutatoa msimamo wetu," alisema Mbowe.

Awali Katibu wa muda wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa), Julius Mtatiro alisema
Rais Jakaya Kikwete amevuruga mchakato wa
Katiba, kwani walitarajia angetumia mamlaka
yake kama Rais kuwaunganisha.
"Rais tulitarajia angeongea kama mkuu wa
nchi, lakini amezungumza kama Mwenyekiti
wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo
wa Muungano jambo ambalo
hatukulitegemea," alisema Mtatiro.
Alisema kwa Rais kutoa msimamo ni sawa na
mwongozo jambo ambalo limevuruga
mchakato mzima.

Hofu ya kuvunjika Bunge
Wakizungumza nje ya Bunge, baadhi ya
wajumbe wameeleza kuwa hotuba ya Rais
Kikwete kama ikitekelezwa uwezekano wa
kupata Katiba Mpya utakuwa mgumu.

Mjumbe Luhaga Mpina alisema kwa jinsi
rasimu ilivyoandikiwa na kama muundo wa
serikali mbili ukipita basi rasimu ya Katiba
itabidi iandikwe upya.

"Rasimu yote imetengenezwa kwa mfumo wa
serikali tatu sasa hapa kuna hatari ya Bunge
kukwama ," alisema.

Mtatiro kwa upande wake alisema sasa kuna
hofu ya kushindwa kupatikana Katiba Mpya
kwani Rais amewachanganya wajumbe na
kama watapitisha maoni yake itabidi rasimu
kuandikwa upya.
hivi vyama pinzani navyo vinajua umuhimu wa katiba? mfano katiba ya cdm na mambo yanayoendelea.
sisi tumemuelewa rais wetu kwa uzalendo wake naamini tutashinda kila sehemu kasoro humu jamii forum maana kuna chagadema group.
 
Jk ndo alitakiwa aongee kama alivoongea juzi kingunge. Nilitegemea angesisitiza uchumi kukua na umuhimu wa katiba mpya, ila kwa kweli hakufanya hivo na si vizuri kwa position yake.
 
mbona mbowe aliishangilia sana hotuba ya rais

Walichokuwa wakikishangilia akina Lissu.mbowe. wenje. owenya. sakaya kiwia ni kitu gani?
wanasiasa bwana tabu sana. ngoja nibaki na shughuli za kilimo.
Hotuba ya makundi yote ndio maana wote walikuwa wanashangilia kwa zamu kwamba walikunwa haswa
 
Hapa ninayoyaona kwako ni mambo mawili tu,
Upeo wako ni mdogo sana au Unafanya makusudi
 
Walichokuwa wakikishangilia akina Lissu.mbowe. wenje. owenya. sakaya kiwia ni kitu gani?
wanasiasa bwana tabu sana. ngoja nibaki na shughuli za kilimo.
Hotuba ya makundi yote ndio maana wote walikuwa wanashangilia kwa zamu kwamba walikunwa haswa

Akili yako ndogo sana,
 
Hiyo n rasimu. wenye wajibu wa kutunga katiba ni wajumbe maalum wa bunge la kutunga katiba.
kikwete kazindua bunge kama mgeni rasmi.
Amewaasa muisome rasimu ukurasa kwa ukurasa. kifungu kwa kifungu. ibars kwa ibara neno kwa neno kusudi muielewe na muelewe mnachokijadili.
Tanzania tuna wana siasa njaa. Mnataka yenu tuuuu ndio yasikilizweee!
kawaambia jengeni daraja mkifanya masihara tutagawana mbao.

Inaonekana ni hayo tu ndo aliyoyaongea na mengine yote wanamsingizia. ACHA KUPOTOSHA
 
Jamani pingeni hoja msipinge tu kwa vile kazungumza Mwenyekiti wa CCM. Tatizo Wapinzani pamoja na Warioba mmejaribu kuonesha matamu tu lakini machungu hamjayaonesha alichofanya Rais kuzungtjmzia mapungufu ya hiyo Katiba na machungu yaliyomo humo. Tatizo ya Viongozi wa upinzani ni kwamba jambo hata likiwa jema vipi lakini kama limetoka kwa CCM hawalikubali hata kidogo hatuwezi kufika kwa njia hiyo kama Rais aliyosema si sahihi bishieni hoja tumewapa majukumu ya kutengeza katiba iwe serikali 3 au 2 lakini mzingatie mambo muhimu kuhusu hiyo katiba. Kama si hivyo semeni sasa hamuwezi mrudi sio mle laki 3/3 zetu hadi mwisho kisha mseme haikuwezekana itakua hapatoshi tutawaita nyie ni WEZI kama WEZI wengine.
 
Hiyo n rasimu. wenye wajibu wa kutunga katiba ni wajumbe maalum wa bunge la kutunga katiba.
kikwete kazindua bunge kama mgeni rasmi.
Amewaasa muisome rasimu ukurasa kwa ukurasa. kifungu kwa kifungu. ibars kwa ibara neno kwa neno kusudi muielewe na muelewe mnachokijadili.
Tanzania tuna wana siasa njaa. Mnataka yenu tuuuu ndio yasikilizweee!
kawaambia jengeni daraja mkifanya masihara tutagawana mbao.

Mimi naamini malalamiko mengi kuhusu muungano yanatoka zaidi Zanzibar kuliko Tanganyika. Hilo Kikwete hakuliona kabisa. Anazungumzia zaidi wapemba waliopo bara kwamba itakuwaje kukiwa na serikali ya Tanganyika maana itabidi kuwe na utaratibu wa wapemba kuja bara.
Ajabu haoni kuwa hilo ni tatizo. Yaani wapemba (watu wa Unguja na Pemba) kumiliki ardhi bara wakati watu wa bara hawana haki hiyo upande wa pili. Yaani wapemba wawe watanzania lakini watanganyika wabakie kuwa watanganyika wenye jina la watanzania.
Hili suala analiangalia kibinafsi zaidi au kikanda. Yeye ni mtu wa pwani anaona sawa wapemba kujitwalia ardhi bara. Lakini Kikwete huyo huyo anona taabu sana Warwanda na warundi kufanya hivyo kule Kigoma. Rais mwingine akitokea ukanda wa Kigoma anaweza kuwa na msimamo kinyume na huu wa Kikwete. Tunachotaka ni msimamo wa kudumu na muda mrefu wa kuangalia maslahi ya Tanganyika kwanza.
Haimwingii akilini kuwa kule Zanzibar upinzani unaweza kupata ushindi na kubadili kabisa mwelekeo wa muungano. Rasimu ya Warioba ni imekuja muda muafaka kuweka mustakabali wa nchi vizuri bila ya vurugu.
Najua haya mabadiliko makubwa mno na yanahitaji kiongozi jasiri na shupavu mwenye kuona mbali. Sio kiongozi anayedhani CCM itatawala milele. Bahati mbaya sana, aina ya viongozi hao hatuna kwa sasa. Ni business as usual.
Amos Wako keshatoa angalizo. Tuzingatie matakwa ya wananchi. Kwa viongozi wetu waliolewa madaraka ni wimbo wa kitoto.
Siku upinzani ama bara au Zanzibar ukishinda uchaguzi, hakutakuwa tena na fursa nzuri ya kurekebisha muungano kwa njia njia bora kama wakati huu.
Ni aibu Kikwete kufungua bunge maalum akiwa amevaa kofia ya mwenyekiti wa CCM na wala sio Rais wa nchi. Tofauti na Mkapa, huwa anashindwa kutofautisha kati ya urais na uenyekiti wa CCM. Ni sawa na anavyodhani kuwa bado ni waziri wa mambo ya nchi za nje. Angalau wingi wa safari zake nje ya nchi zinaashiria hivyo. Wanasema nchi wakati wote inapata viongozi inaowastahili. Sasa ndio haya yanatukuta.
 
hivi vyama pinzani navyo vinajua umuhimu wa katiba? mfano katiba ya cdm na mambo yanayoendelea.
sisi tumemuelewa rais wetu kwa uzalendo wake naamini tutashinda kila sehemu kasoro humu jamii forum maana kuna chagadema group.

Kumbe kuna mashindano?
 
Nchi hii kila mtu ajitawale tu ndo mpango, sio eti utawala kumbe wizi wa mali za wananchi
 
Well, sasa ndio nimeelewa ni kwanini ccm walitaka Jaji Joseph sinde Warioba ahutubie kwanza kabla bunge halijazinduliwa ili mzinduaje wa bunge badala ya kulizindua afanye kazi ya kujibu hoja za Warioba! Nchi hi ccm ni muhimu kuliko hata nchi yenyewe, ni suala la muda, naanza kuona kile kilichosemwa na Kakobe huenda kikatimia very soon!
 
hivi vyama pinzani navyo vinajua umuhimu wa katiba? mfano katiba ya cdm na mambo yanayoendelea.
sisi tumemuelewa rais wetu kwa uzalendo wake naamini tutashinda kila sehemu kasoro humu jamii forum maana kuna chagadema group.
Ndio hata wajinga kama nyie tunawasikiliza
 
hivi vyama pinzani navyo vinajua umuhimu wa katiba? mfano katiba ya cdm na mambo yanayoendelea.
sisi tumemuelewa rais wetu kwa uzalendo wake naamini tutashinda kila sehemu kasoro humu jamii forum maana kuna chagadema group.

Nonsense. Jenga hoja na acha kuangalia kila kitu kwa jicho la ukabila.
 
Back
Top Bottom