Wenyeviti wa vyama pinzani wakutana

Wenyeviti wa vyama pinzani wakutana

Vyama pinzani vyenyewe vinachakachua katiba zao!
 
Nilipokuwa namtazama Kikwete jana niliona Urais umemtoka kabisa kabaki na uenyekiti wa CCM; Hotuba dhaifu kwa jambo kubwa ambalo ndio mstakabari wa TAIFA LETU Maskini KIkwete, sina Uhakika kama Maraisi waliopita Nyerere, Mwinyi na Mkapa wangeongea hotuba ya hovyo kama hii kwa jambo nyeti la KATIBA.
Nilichokiona mimi ni kama vile KATIBA NI YA WAPINZANI na yeye kama mwenyekiti wa CCM anapambana na WAPINZANI akisahau kuwa mawazo yaliyomo katika Katiba ni ya WANANCHI. Ninajionea huruma kuishi wakati huu wa Watu walioweka maslahi yao mbele na kusahau Utaifa wao. kuuza/kusurrender UTASHI ni HATUA ya mwisho anayofanya mwehu. ninashangaa kuona watu wakishangilia nje ya utashi wao upuuzi kama huu. mfn. Rais anakuja na hoja ya vipindi vitatu havitoshi kwa Mbunge, hivi anadhani ni yeye mke wake na watoto wake ndo wamewekewa kututawala; hakuna utawala haramu uliowahi kudumu. YOTE YANA MWISHO na nchii hii ina watu 45 mil. wenye haki ya kuwa Wabunge; kwanza vipindi vitatu ni vingi. maskini Rais
falsafa zinasema macho ya sungura mjanja yanaposhindwa kupambanua giza na mwanga, yakatamani kuona mwanga na kusahau kuwa kuna gizani: Sungura mjanja hujikuta kaishia mdomoni mwa mlaji.
Hizi porojo porojo za Serikali hii; zimewapofusha kiasi cha kutokumbuka kuwa nchi hii ni ya watanzania wote; na kile Walioba alichokiwasilisha ndio hasa mawazo ya watanzania. Rais huyu ameshindwa kusimamia mawazo ya Watanzania na kuwa mjanja kama Sungura. mwisho wake unafahamika. yeye atapita mwakani nchi hii itaingizwa mdomoni mwa wajanja wengine.
How I long and wish MY True Humble President could be here. Viva Nyerere. Ulale salama Nyerere.
 
Hiyo n rasimu. wenye wajibu wa kutunga katiba ni wajumbe maalum wa bunge la kutunga katiba.
kikwete kazindua bunge kama mgeni rasmi.
Amewaasa muisome rasimu ukurasa kwa ukurasa. kifungu kwa kifungu. ibars kwa ibara neno kwa neno kusudi muielewe na muelewe mnachokijadili.
Tanzania tuna wana siasa njaa. Mnataka yenu tuuuu ndio yasikilizweee!
kawaambia jengeni daraja mkifanya masihara tutagawana mbao.

Mbona jana aliwajengea daraja lao CCM hukuona, sasa kama alikuwa na majibu yoote hayo aliunda tume yanini?
 
hivi vyama pinzani navyo vinajua umuhimu wa katiba? mfano katiba ya cdm na mambo yanayoendelea.
sisi tumemuelewa rais wetu kwa uzalendo wake naamini tutashinda kila sehemu kasoro humu jamii forum maana kuna chagadema group.

mwigulu.
 
Katiba bora hutungwa tu na watu wasio na maslahi na madaraka lakin wenye nia na madaraka hupenda katiba isiyowabana kufanya maovu.sasa kama tunataka katiba yenye kukuza uchumi na haki vipi tuseme sis hivi na wale hivi.du! Wansiasa bwana watu hatari sana, nashukuru sina kutokuwa mwanasiasa ,maana hawa ndio wachawi wa maendeleo na huduma mbovu ktk jamii zote duniani
 
Nilipokuwa namtazama Kikwete jana niliona Urais umemtoka kabisa kabaki na uenyekiti wa CCM; Hotuba dhaifu kwa jambo kubwa ambalo ndio mstakabari wa TAIFA LETU Maskini KIkwete, sina Uhakika kama Maraisi waliopita Nyerere, Mwinyi na Mkapa wangeongea hotuba ya hovyo kama hii kwa jambo nyeti la KATIBA.
Nilichokiona mimi ni kama vile KATIBA NI YA WAPINZANI na yeye kama mwenyekiti wa CCM anapambana na WAPINZANI akisahau kuwa mawazo yaliyomo katika Katiba ni ya WANANCHI. Ninajionea huruma kuishi wakati huu wa Watu walioweka maslahi yao mbele na kusahau Utaifa wao. kuuza/kusurrender UTASHI ni HATUA ya mwisho anayofanya mwehu. ninashangaa kuona watu wakishangilia nje ya utashi wao upuuzi kama huu. mfn. Rais anakuja na hoja ya vipindi vitatu havitoshi kwa Mbunge, hivi anadhani ni yeye mke wake na watoto wake ndo wamewekewa kututawala; hakuna utawala haramu uliowahi kudumu. YOTE YANA MWISHO na nchii hii ina watu 45 mil. wenye haki ya kuwa Wabunge; kwanza vipindi vitatu ni vingi. maskini Rais
falsafa zinasema macho ya sungura mjanja yanaposhindwa kupambanua giza na mwanga, yakatamani kuona mwanga na kusahau kuwa kuna gizani: Sungura mjanja hujikuta kaishia mdomoni mwa mlaji.
Hizi porojo porojo za Serikali hii; zimewapofusha kiasi cha kutokumbuka kuwa nchi hii ni ya watanzania wote; na kile Walioba alichokiwasilisha ndio hasa mawazo ya watanzania. Rais huyu ameshindwa kusimamia mawazo ya Watanzania na kuwa mjanja kama Sungura. mwisho wake unafahamika. yeye atapita mwakani nchi hii itaingizwa mdomoni mwa wajanja wengine.
How I long and wish MY True Humble President could be here. Viva Nyerere. Ulale salama Nyerere.
Kama ulijionea huruma kuish wakat huu ulichukua hatua gan? Jk ndo rais bora wa africa kwa sasa
 
Ni jambo jema waunganishe nguvu ili tuipime nguvu yao ambayo ni ya wananchi na ile ya ccm.
Nawashauri waje na mkakati mzito ili warioba hoja zake zisimezwe na ngonjera za jk
 
Dodoma. Wenyeviti wa vyama vya Upinzani vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR-Mageuzi, jana usiku walikutana ili kutoa kauli ya pamoja, kutokana na hotuba ya ufunguzi wa Bunge kwa maelezo kuwa tayari Rais amevuruga
mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Wakati viongozi hao wakikutana, Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji, Christopher Mtikila alisema, Rais ameingilia mchakato na kutoa maelezo jinsi ya kuandika Katiba.

Wakizungumza na gazeti hili jana mara baada ya hotuba hiyo, Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Ibrahim Lipumba, walisema wameipokea kwa masikitiko makubwa hotuba hiyo.

“Tunakwenda kujadili hotuba ya Rais na tutatoa msimamo wetu,” alisema Mbowe.

Awali Katibu wa muda wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Julius Mtatiro alisema Rais Jakaya Kikwete amevuruga mchakato wa
Katiba, kwani walitarajia angetumia mamlaka yake kama Rais kuwaunganisha.

“Rais tulitarajia angeongea kama mkuu wa nchi, lakini amezungumza kama Mwenyekiti wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo wa Muungano jambo ambalo hatukulitegemea,” alisema Mtatiro.

Alisema kwa Rais kutoa msimamo ni sawa na mwongozo jambo ambalo limevuruga mchakato mzima.

Hofu ya kuvunjika Bunge Wakizungumza nje ya Bunge, baadhi ya wajumbe wameeleza kuwa hotuba ya Rais Kikwete kama ikitekelezwa uwezekano wa kupata Katiba Mpya utakuwa mgumu.

Mjumbe Luhaga Mpina alisema kwa jinsi rasimu ilivyoandikiwa na kama muundo wa serikali mbili ukipita basi rasimu ya Katiba itabidi iandikwe upya.

“Rasimu yote imetengenezwa kwa mfumo wa serikali tatu sasa hapa kuna hatari ya Bunge kukwama ,” alisema.

Mtatiro kwa upande wake alisema sasa kuna hofu ya kushindwa kupatikana Katiba Mpya kwani Rais amewachanganya wajumbe na kama watapitisha maoni yake itabidi rasimu kuandikwa upya.

...............Binafsi nikiwa mtanzania mwenye akili timamu sina budi kutoa maoni yangu binafsi kutokana na kitendo ambacho rais Kikwete amekitenda jana .... imeniuma sana imenisikitisha sana... naona kabisa kwamba hakuna haja ya swala la bunge la katiba na kwamba bunge hilo halina kazi ... nilitegemea mkuu angeongea kwa kuainisha umoja na mshikamano kwa wajumbe, ninashangaa kwamba mkuu ile ni tume yake na alikuwa anamawasiliano binafsi na tume yake aliyoiunda yeye mwenyewe tena ni nje ya sera za chama chake.. nilitegemea kwa kuwa alikuwa na mawasiliano na tume basi angetoa ushauri na maoni yake huko huko yeye na kamati yake lakini amekuja kuichamua na kuichamba rasimu mbele ya kadamnasi na kuwafanya wale wote walioshiriki katika kuandaa rasmu hiyo kuonekana kama wamekula pesa ya taifa bure... maana ukiangalia kikosi cha tume ya rais yakuandaa rasimu ya katiba unakuwa huna wasiwasi kwamba ni watu wenye upeo na mwelekeo lakini wameonekana hovyo na hakuna walichokifanya.... imeniuma sana

 
Hiyo n rasimu. wenye wajibu wa kutunga katiba ni wajumbe maalum wa bunge la kutunga katiba.
kikwete kazindua bunge kama mgeni rasmi.
Amewaasa muisome rasimu ukurasa kwa ukurasa. kifungu kwa kifungu. ibars kwa ibara neno kwa neno kusudi muielewe na muelewe mnachokijadili.
Tanzania tuna wana siasa njaa. Mnataka yenu tuuuu ndio yasikilizweee!
kawaambia jengeni daraja mkifanya masihara tutagawana mbao.

Hahahahahahha, wewe ndo ulimwandikia hotuba au? Hivi kweli kwa akili zako timamu unaweza kusema kuwa ile ni hotuba ya kiongozi wa Nchi? Nitashangaa sana kama hakwenda kusaign kwenye pay role ya jana na kujichukulia posho yake ya kujikimu pamoja na ya kikao kwa kuwa aliongoea kama mjumbe wa bunge la katiba tena aliyetoka Chama Cha Mapinduzi. Hakupewa kazi ya kuchambua Rasimu kwa kuwa mamlaka hayo hayako kwake. Kiongozi wa nchi anao wajibu wa kuwa kiunganishi na siyo anajiunga na kundi fulani. Ni sawa sawa na refa kuvaa jezi za timu mojawapo anapochezesha mpira na hata kuisaidia timu hiyo aliyovaa jezi yake. Hilo ndilo alilolifanya Kikwete Jana. Ukweli washauri wake walimpotosha nadhani akasahau kutumia falsafa yake ya kawaida ya akili ya kuambiwa changanya na ya kwako. Naona jana hakuchanganya ya kwake.
 
Ugomvi wa kugombania sahani ili upange foleni ukachukue chakula mara zote huwa mkubwa na mpana kuliko ugomvi wa kupakua chakula chenyewe. Maana hata ukifikia kupakua ukakuta kimeisha hutamlaumu aliyetangulia wala ajaye nyuma yako maadam umekuta kimekwisha.waache wakazane na kugombania sahani watakapojitambua tutawasikia tu.
 
Nilipokuwa namtazama Kikwete jana niliona Urais umemtoka kabisa kabaki na uenyekiti wa CCM; Hotuba dhaifu kwa jambo kubwa ambalo ndio mstakabari wa TAIFA LETU Maskini KIkwete, sina Uhakika kama Maraisi waliopita Nyerere, Mwinyi na Mkapa wangeongea hotuba ya hovyo kama hii kwa jambo nyeti la KATIBA.
Nilichokiona mimi ni kama vile KATIBA NI YA WAPINZANI na yeye kama mwenyekiti wa CCM anapambana na WAPINZANI akisahau kuwa mawazo yaliyomo katika Katiba ni ya WANANCHI. Ninajionea huruma kuishi wakati huu wa Watu walioweka maslahi yao mbele na kusahau Utaifa wao. kuuza/kusurrender UTASHI ni HATUA ya mwisho anayofanya mwehu. ninashangaa kuona watu wakishangilia nje ya utashi wao upuuzi kama huu. mfn. Rais anakuja na hoja ya vipindi vitatu havitoshi kwa Mbunge, hivi anadhani ni yeye mke wake na watoto wake ndo wamewekewa kututawala; hakuna utawala haramu uliowahi kudumu. YOTE YANA MWISHO na nchii hii ina watu 45 mil. wenye haki ya kuwa Wabunge; kwanza vipindi vitatu ni vingi. maskini Rais
falsafa zinasema macho ya sungura mjanja yanaposhindwa kupambanua giza na mwanga, yakatamani kuona mwanga na kusahau kuwa kuna gizani: Sungura mjanja hujikuta kaishia mdomoni mwa mlaji.
Hizi porojo porojo za Serikali hii; zimewapofusha kiasi cha kutokumbuka kuwa nchi hii ni ya watanzania wote; na kile Walioba alichokiwasilisha ndio hasa mawazo ya watanzania. Rais huyu ameshindwa kusimamia mawazo ya Watanzania na kuwa mjanja kama Sungura. mwisho wake unafahamika. yeye atapita mwakani nchi hii itaingizwa mdomoni mwa wajanja wengine.
How I long and wish MY True Humble President could be here. Viva Nyerere. Ulale salama Nyerere.

Na kweli nakuunga mkono kwa asilimia mia. Nadhani huyo mheshimiwa alipiga umri wa mwanaye ambaye sasa anagombea ubunge akaona looo ! mbona atakuwa nje ya mfumo wa kula muda akiwa bado na umri mdogo. Akaona cha kufanya ni kupinga hoja ya kuwepo kwa ukomo wa wabunge. Yeye mwenyewe aliongoza Chalinze miaka 15 amewaacha maskini wa kufa na bado anadhani mtu aliyoongoza jimbo kwa zaidi ya miaka hiyo ana ndoto ya kuleta mabadiliko tena. Kaitetea familia yake tu na wala siyo maslahi mapana ya nchi.
 
Sitegemei hata mwana ssm kama anaweza kuiunga hutuba Ya jk alieitowa jana
 
Back
Top Bottom