Wenye viwanda watishia kuvifunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye viwanda watishia kuvifunga

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, Jan 23, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Wenye viwanda watishia kuvifunga Friday, 21 January 2011 19:53

  Raymond Kaminyoge
  Mwananchi

  WAMILIKI wa viwanda nchini, wametishia kufunga viwanda vyao kutokana na gharama kubwa za uendeshaji zinazotokana na mgao wa umeme unaoendelea.

  Walisema hayo jijini Dar es Salaam jana, kwenye mkutano wa wadau wa viwanda ulioandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), ili kutoa mapendekezo kwa serikali jinsi wanavyoweza kupata umeme wa uhakika.

  Walisema zaidi ya asilimia 30 ya gharama zote za uzalishaji kwenye viwanda, zinatumika kulipia umeme.

  “Hali ni mbaya, umeme umekuwa tatizo sugu nchi hii, kwa wiki zaidi ya saa 30 viwanda havifanyi kazi kwa sababu hakuna umeme, tutajiendeshaje wakati muda wote huo hatuzalishi,” alisema Arfil Kumar wa Kiwanda cha Kutengeneza Mabati cha Alaf.

  Kumar alisema asilimia 14 ya Watanzania ndio waliounganishwa na umeme wa gridi ya taifa, waliosalia hawana nishati hiyo.

  “Cha kushangaza ni kwamba licha ya idadi ndogo ya Watanzania wanaotumia umeme wa Tanesco, umeme wanaupata kwa mgao, asilimia 85 ya Watanzania wataunganishwa vipi umeme hakuna?” alihoji Kumar.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Uchumi, Jehovanes Aikael, alisema alitembelea viwanda 60 mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Iringa na Mwanza na kufanya mahojiano na wamiliki.

  Aikael alisema kwenye mahojiano hayo, alibaini kwamba mgao wa umeme ni tatizo kubwa tofauti na inavyoonekana.
  Alisema hata pale umeme unapopatikana, wenye viwanda hivyo walimweleza kuwa, haukuwa na nguvu ya kuendesha mitambo.

  “Kwa hiyo kutokuwa na umeme wa uhakika ni kikwazo kikubwa kwa wawekezaji wa viwanda, kwani wanashindwa kufikia malengo yao waliyojiwekea,” alisema.

  Alisema baadhi ya wenye viwanda wanaonyesha kukata tamaa kutokana mitambo yao kutofanya kazi kwa kukosa umeme, licha ya kuinunua kwa gharama kubwa.

  Kwa upande wake, Juma Isevya, mmiliki wa kiwanda cha kusindika maziwa, alisema serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka ili umeme wa uhakika uweze kupatikana.   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wakome!!! Wafunge wasifunge watajua wenyewe kwani ni nani aliewambia wachangie zaidi ya billion 5 pale white sand hotel siju Girafe kwa ajili ya kuhakikisha serikali inarudi madarakani? Kwa nini wasichangishe tena wanunue jenereta? Watoe unafiki hapa. Wengine walitoa hadi elkopta kabisa kuhakikisha wananchi wanadanganywa na ahadi 79 ambazo ni hewa.
   
Loading...